Sijui nimembemenda

Sijui nimembemenda

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
1,726
Reaction score
314
Kubemenda nasikia ni kitendo cha mtoto kushindwa/kuchelewa kutembea ambako kunasababishwa na wazazi wake kufanya mapenzi mara kwa mara aidha wao wenyewe au kutoka nje ya ndoa.
Mtoto wangu ana mwaka sasa hatembei na ni kweli tunafanya mapenzi kila baada ya siku moja ila anawezakusimamia kitu nakutembeakwa kujishikilia katika meza au sofa au hata akishikwa mkono.

Jamii imeanza kuninyoshea vidole na baadhi yao wamefikia hatua ya kunishauri chakufanya ili atembee ila sijaanza kufuata ushauri wao kwa sababu bado siuamini sana mfano wengine wameniambia eti mke wangu atumie chupi yake kumkanda miguu na wengine eti kitambaa kinachotumika kujifutia baada ya kufanya mapenzi kitumike kumkandia miguu mtoto.

kiukweli sijui nini cha kufanya lakini naamini JF ni kila kitunitapata ushauri na msaada wa kila aina na maanisha ushauri wa kisayansi na ule usio wa kisayansi.

nawasilisha
 
Acha hofu mkuu, hakuna umri kamili kwa mtoto kuanza kutembea, mwaka mmoja bado hajachelewa sana ila unachotakiwa kufanya ni kumtengenezea kile kigari cha miguu mitatu na kuhakikisha anafanya mazoezi ya kutembea mara kwa mara.
 
Suala la mtoto kutembea hutegemea sana mazingiza/wazazi, watoto huwa wanakuwa na woga ,hivyo mzazi au yaya anatakiwa kuwa makini katika kumfanyisha mazoezi na kumtia moyo, ndo maana kunakuwa na zile nyimbo za watoto" kasimama peke yake", simama dede nk.
 
Ila poti na wewe umezidi kutomba kila baada ya siku moja ww unapanda stejini? Nadhani hata mtoto muda wa kunyonya hata itakuwa unanyonya hata maziwa ya mtoto ndio maana hata nguvu za kutembea hana mwache mama apumzike bwana
 
Achana na ushauri huo waliokupa.kama walivyosema waliotangulia watoto hutofautiana na kama ni mtoto wa kwanza mara nyingi uchelewa. huyo hajachelewa ,kwa mazoezi zaidi mnunulie kigari atatembea.
 
Ila poti na wewe umezidi kutomba kila baada ya siku moja ww unapanda stejini? Nadhani hata mtoto muda wa kunyonya hata itakuwa unanyonya hata maziwa ya mtoto ndio maana hata nguvu za kutembea hana mwache mama apumzike bwana
Mnhhh, michango mingine naogopa hata kusoma.
 
Hayo mambo ya kumpaka mtoto janaba lenu sio yenyewe kabisaa! Kwani hamuendi clinic? Mngepata majibu sahihi kabisa. Kila mtoto ana ratiba yake, kuanzia kutembea, kuota meno, kuongea, kubalehe, kuota ndevu/manyonyo etc. Hakikisha mtoto ananyonya vya kutosha na kupata lishe bora kila wakati. Achana na imani za ajabu ajabu!
 
Kwa kuwa wewe ni kichwa ngumu cjui kama utatekeleza ushaur wowote. Anyway Punguza kupanda afu mwambie mama ajisafishe matiti yake kabla hajanyonyesha
 
Back
Top Bottom