Sijui nimtulizeje Maana nahofia naweza kuja kufa kwa sonona, Mliofanikiwa katika hili nipeni siri mlifanyaje?

Sijui nimtulizeje Maana nahofia naweza kuja kufa kwa sonona, Mliofanikiwa katika hili nipeni siri mlifanyaje?

Sonko Bibo

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2019
Posts
957
Reaction score
1,493
Niliambiwa,

Bro, kummudu huyo yataka moyo.

Nikajiwazia tu, shujaa hatelezi anapanda milima mingi mpaka kufika kilele, hawa waniache.

Nikamtafuta kweli nikaanza kummiliki taratibu japo hakuwa mwingi kwangu.

Jamaa na ndugu walipoanza kuniona nae tu, wakaniijia haraka na maswali yenye bashasha.

Kwa hiyo umeanza kumpata?

Nikawa nawajibu tu, niko nae lakini sio kwa sana.

Wakaniambia uanaume ni kukaza pia wakanipa hongera nyingi.

Sasa sijui kama hongera zao zina dhamira ya dhati? Sielewi.

Kitendo cha ndugu na jamaa kujenga ukaribu na mimi baada ya kuwa nae kilinipa faraja sana.
Hata mabinti kwa mashoga inaonekana aliwahamasisha waanze kuniwinda kwa uwazi na kimya kimya.

Heshima nayo ilitaradadi sana kwangu, nikaonekana nina nyota kali sana ila ukweli nimeujua kuwa sikuwa na nyota wala cha nini.

Wapo waliokuja bila kificho na kutaka kumuondoa kwangu iwe kwa diplomasia ama kinguvu.

Nikiri tu kuwa, kuna muda aliteleza na kuwasikiliza kisha akanitenga.

Nami nilibaki kulaani lakini nikifanya kila jitihada kumrudisha kwenye himaya yangu.

Ajabu mama kila nikimwambia kuwa nateseka kupitia huyu binti, mama hunionea tu huruma na kuniambia ndio ukubwa mwanangu pambana umrudishe.

Kwanza una bahati, ujue wengine hawajawahi hata kuliona tabasamu lake. Basi hapo nitafarijika na kuongeza mori.

Nampenda sana lakini yeye ndio kwanza hajali wala hajawahi kuonesha kama ananipenda wala kunijali.

Akirudi kwangu huwa ni kwa juhudi kubwa sana kama za watumwa au prisoner of war.
Anaponimaliza ni pale, akiondoka kwangu nakuwa mpweke, natengwa na ndugu na majamaa wote.

Ila akirudi, anakuja nao wote na nyongeza ya marafiki wapya yaani ni kama vile huwa anawaambia kuwa narudi kwa mwamba.

Huyu kiumbe ni mzuri sana na ukimuangalia anakusisimua sana, halafu kingine watu wote tunamuona hazeeki.

Niliambiwa kuwa anawanyima watu wengi usingizi kabisa kiasi wakiniona ama kusikia niko nae wananiheshimu sana kinafiki huku deep down wanamlenga yeye tu.

Utasikia karibu sana mheshimiwa, mara broo unajitunza sana huyo wifi yetu anafaidi sana.

Lakini ni kuinyume, ukweli ni kwamba mimi ndio nafaidi sana kwa huyo wifi yao.

Anapendwa sana na wanaume ila wanawake wanamtaka sana wamkamate wamuweke karibu yao, awasaidie mambo mengi.

Hivyo nikagundua kuwa wanawake hunifuata wakimvizia yeye, mara wampeleke kwenye vikundi na vikoba vyao. Kifupi wanampenda sana na sijui wanataka kumtumiaje maana kwa wanaume sina swali najua wanataka wamfanyie nini.

Uajabu wake ni kuwa hakatai nikimtuma, hata nikimtuma mara mia anaenda na analeta nilichomtuma.

Hata kama ni kibaya au kitanidhuru yeye ananiletea tu hana wivu na mimi bali hilo jukumu kaniachia mimi niwe na wivu nae.

Ananitesa hadi naliona kaburi hili hapa lakini sina ujasiri wa kumuacha na sisemi kaniroga ila najua mimi ndio namhitaji kuliko yeye anavyonihitaji.

Ananichanganya pale ambapo ukimuwekea mikakati mizuri tu anakuja kwako bila kubagua dini wala tabaka, awe mzee au kijana mdogo aliebalehe yeye anaenda.

Cha kushangaza kwanza ni bubu lakini anaongea kwa ishara na wote tunamuelewa, hatujawahi kusikia sauti yake ila tunajua anaongea na ukiwa nae wewe piga kelele zote watu hawakusikilizi kamwe, wanamsubiri yeye tu atoe ishara.

Kuna wanaojisifia kuwa wanammiliki zaidi yangu nawakubalia tu kwasababu namjua hawezi kukaa kwako bila nguvu na akili nyingi.

Hivyo nabaki nasema, "Atatuua huyu maana sio kwa kutupelekesha huku."

Akija kwangu haji peke yake, ataambatana na wenzake wengi wa kariba yake.

Ila wote hao wanamuhitaji yeye ili waendelee kuwa wazuri daima.
Akiondoka huyu tu, na wao wanafubaa na kuanza kuondoka kwangu taratibu hadi nabaki na fadhaa.

Historia yangu na yeye ni tawili sana.

Akija ananiletea manukato na marashi kutoka dunia ya mbali, nguo nzuri pia ananibadilisha tabia, ananipa utulivu wa nafsi akikuelewa sana yaani ile sana anakuletea magari hata nyumba ukiamua anakupa.

Ukiugua anakubali kuhamia kwa daktari ili wewe utibiwe unakuwa hupendi lakini inakubidi umruhusu aende tu ili upone.

Viongozi wakubwa wa nchi wanampenda mno wanaenda hadi kwa waganga ili awape funguo ya milango inayoelekea kwake tunakutana kwenye mahakama za siri na tunakula viapo vya maagano pamoja na wachungaji na masheikh. Wote tunamtaka yeye tu.

Akitaka kuondoka kwangu, hatoi taarifa bali anaonesha dalili tu mara naona hayupo nabaki kutapatapa.

Nikiwa nae najiamini sana mpaka sijui kati yangu na yeye nani atamuoa mwenzake maana siwezi hata kumkoromea, maisha gani haya sasa?

Watu wakiniona niko nae, wanasema nimetumia mzizi, hawako mbali na ukweli maana nimebakiza tu kusaini mkataba na LUCIFER ili nikae nae hadi nakufa.

Haijalishi miaka yangu itapunguzwa kwa ufupi gani lakini sipo tayari kuishi bila yeye.
Ndugu, marafiki na maadui zangu wote wanamuwinda yeye tu, wanataka wajue kile nachopata kwake. Yeye ndie chanzo cha furaha yangu ananipa vyote navyohitaji viwe visafi na vichafu ananipa, sijui aliumbwaje yaani.

Yaani akiwa na wewe unajikuta kashakuzidi nguvu anaanza kukucontrol, mara sitaki utembee kwa miguu tena. Anakupandisha boda na haya ma uber.

Anakusababishia magonjwa ya kisukari na presha maana anakuhamasisha ule mahanjumati mengi yaani edible materials kibao, mara mikeki michocoleti, mibiskuti na minyama ya kopo.

Ukimuuliza kwanini anakujibu hizo ndio ishara za uwepo wake kwako.
** * ****

Kwasasa kanikimbia japo nimeanza mahusiano nae miaka kumi na mbili iliyopita, lakini najipanga tena nikamchukue sipo tayari kumkosa.

Japo nahisi kukata tamaa maana mpaka sasa sijui yuko wapi na yuko na nani ingawa najua yupo tu anawaburudisha wengine.

Nifanyeje jamani? Ananizeesha mimi kwa mawazo hata hamu ya kula imekata.

Kasababisha hadi mama watoto wangu kanitenga japo najua kuwa nikimpata lazima na huyo mama watoto atarudi tu.

Maana nae anamvizia huyu huyu mpenzi wangu maana mimi na mpenzi wangu tulianza mahusiano kabla hata ya kufahamiana na mke wangu.

So najua mke wangu alimfuata huyu mpenzi wangu. Japo mke wangu mara kadhaa amekuwa akikanusha vikali sana ila huo ndio ukweli nilioubaini
Acha nimalizane na LUCIFER kwanza ili aniozeshe huyu demu mazima nataka kurasimisha ndoa na yeye( kumbuka ndoa ni agano)

So usiwaze kuwa ni ndoa ya maigizo kama hizo zenu na hii ya huyu mke wangu alienikimbia, no hii ni ndoa haswa itakayomfanya huyu binti awe mke wangu jumla nampenda sana eti na sijiwezi bila yeye.
Sonko Bibo.



Nataka siku moja nikae niufurahie huu wimbo nikiwa na huyu binti.


 
Back
Top Bottom