Mkuu
kcamp ni kweli soko la muziki linategemea concept ya demand and supply, lkn kiuhalisia demand ambayo ndiyo hadhira inategemea sana suppliers ambao ndiyo wasanii hapa namaanisha huwezi ku demand kitu ambacho hakipo sokoni, so wasanii wana uwezo mkubwa wa kubadilisha akili ya hadhira hasa wasanii wakubwa mana hawa wadogo wanaangalia nn wakubwa wanafanya, kwa mfano kuna mziki umeibuka kwa ss mziki wa singeli japo ulikuwepo kwa mda kdg lkn ulikuwa unaonekana km mziki wa kihuni usio na maadili na ni wa uswahilini, lkn ghafla umeanza kupewa credibility baada ya wasanii wakubwa kuanza kuuimba, hii inaonesha nguvu ya ushawishi waliyonayo wasanii wakubwa na pengine niseme kitu kimoja, ni kwamba huu mziki wa matusi ya wazi wazi muasisi ni Diamond pamoja na kundi lake la WCB japo ni kweli matusi yalikuwepo huko nyuma lakini c kwa kiwango cha ss, huko nyuma ilikuwa nyimbo ikiwa na tusi hata kwny redio stesheni ulikuwa unafinywa kimtindo lkn kwa ss imeshaonekana ni kitu cha kawaida maana utafinya nyimbo ngp ilihali asilimia kubwa ya nyimbo za ss zinafanana, mm mwenyewe ni mpnz wa nyimbo za Mondi na kundi zima la WCB na huu ndio ukweli wenyewe kwmb kupitia wao wasanii wengine wakaona hii ndio direction na mpk ss tunapoelekea ni kubaya zaidi km hii perception ya wasanii wanaimba kulingana na uhitaji itaendelea kugonga ktk vichwa vya wasanii.
Recommendation
Wasanii wakubwa wanapaswa kujuwa wajibu wao kwmb mbali na kuburudisha pia waangalie namna ya kutoharibu maadili yaliyopo katika jamii kwn wao wanaweza kuamua ni mziki gn wa kuimba na hadhira itasikiliza na kupenda itake isitake