Sijui wako wapi wale rafiki zetu wa shule ya msingi

Sijui wako wapi wale rafiki zetu wa shule ya msingi

Daaha kwa mimi niliyesoma shule za msingi kama tano inakua ngumu hapo
1-2 Inyala Iyunga Mbeya
3-4 Mapinduzi Forest Mbeya
5-6 Majimatitu Mbagala DSM
6-7 Kivinje Kilwa Lindi

Hapa kuwakumbuka ni shighuli sana an daaah
 
Wengine walisha tangulia mbele ya haki,

Wapo ambao wamekua walevi wakupindukia,

Wapo ambao wanapigania uhai wao kwa maradhi,

Wapo ambao wamekua matajiri au kua na vyeo vikubwa,

Wapo ambao wana watoto mpaka wajukuu,wapo ambao hawana uzazi,

Life is a journey.
 
Nasoma huu uzi huku roho inaniuma,nimepoteza rafiki zangu wa karibu watatu,amebaki mmoja sasa. Hao watatu wametangulia mbele za haki huku vifo vyao vikiwa vya kutatanisha na mmoja maiti yake haikuonekana alizama Bwawa la Mtera wakati wakiwa kuvua samaki usiku.

Mwingine aliugua ugonjwa hata haueleweki,mwingine mambo ya mirathi,watu walidhulumu mali za baba yake na alikuwa mtoto wa pekee kwa baba yake.

Ila Wakinga sio watu wazuri kabisa, hao jamaa zangu wote Wakinga na wameshatangulia mbele za haki. Roho inaniuma sana nikenda home nikisimama nje naangalia upande wa pili wa barabara,naangalia tu nyumba za wazazi wao zilivyofuatana
 
Nasoma huu uzi huku roho inaniuma,nimepoteza rafiki zangu wa karibu watatu,amebaki mmoja sasa. Hao watatu wametangulia mbele za haki huku vifo vyao vikiwa vya kutatanisha na mmoja maiti yake haikuonekana alizama Bwawa la Mtera wakati wakiwa kuvua samaki usiku...
Pole sana mkuu. Mimi nimepoteza rafiki yangu wa utotoni mwaka jana. Mpaka leo nikimpigia simu mama yake analiaga kama mtoto.

Amebakiza picha yetu ya utotoni, huwa nikienda kumuona hatakagi niondoke 😭.

Inshort, jamaa alipata mental problem kwa kipindi cha miakw miwili, mbaya sana alikuwa hali. Yani kilichomuua ni njaa. Maana ni chizi halafu hali. Sasa mtu mzima unamlishaje?
 
Maisha yanatufanya tusambaane aise yani marafiki wa primary wote wapo ila maisha yanatenganisha nikikumbuka nabaki nafurahi tu .

Kuna jamaa wakuitwa juma huyu jamaa alikuwa mwizi balaa kila tukio la wizi lazima atahusika yeye.Pia jamaa alikuwa mkorofi yani alikuwa kila ugomvi alikuwa hakosi kuwemo.

Kuna mwingine anaitwa shabani huyu alikuwaga mtu wa vichekesho darasani yani siku akitoroka shule darasa lina poa hadi walimu walimjua kwa vituko vyake.jamaa sasahivi ni mwalimu sijui wapi.

Haya kuna mwingine alikuwa anaitwa omari huyu huyu alikuwa mzee wa chabo kila mtihani yeye alikuwa anapiga chabo tu.

Mmoja yupo kenya anaitwa opio huyu ndio alikuwa toka utotoni tumeiba nar sana mapera huyu jamaa alikuwa na matege basi bwana siku moja tumeenda kuiba mapera tuko juu ya mti mimi nikaruka haraka nikakimbia huyu opio na matege yake anakimvia kama anarudi nyuma.Alikamatwa alichezea kichapo huku ananitaja mimi.

Matukio ni mengi muda mchache.
 
Pole sana mkuu. Mimi nimepoteza rafiki yangu wa utotoni mwaka jana. Mpaka leo nikimpigia simu mama yake analiaga kama mtoto.

Amebakiza picha yetu ya utotoni, huwa nikienda kumuona hatakagi niondoke 😭.

Inshort, jamaa alipata mental problem kwa kipindi cha miakw miwili, mbaya sana alikuwa hali. Yani kilichomuua ni njaa. Maana ni chizi halafu hali. Sasa mtu mzima unamlishaje?
Asante Mkuu,pole na wewe.Yaani hao jamaa zangu tulikuwa huru sana tukiamua leo walale kwetu wanakuja,siku nyingine tukalale kwa akina F tunaenda,siku nyingine kwa akina J tunaenda. Urafiki ulikuwa shuleni hadi mtaani
 
Back
Top Bottom