Sikia kauli hii ya msemaji wa Simba

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
HAJI MANARA.
"Watanzania wameona kiwango cha Yanga
walichoonesha Tunisia ni kiwango cha hali ya juu
sana,kwa kiwango kile sioni sababu ya kufungwa
na Azam ambayo ni timu mbovu ambayo sisi
tumeifunga. Naiomba viongozi wote wa tff na kamat ya nidhamu wawepo uwanjani kesho (leo)
kuona mchezo mchafu wa Yanga. Tena
nakuhakikishia sisi Simba tutachukua video ya
mechi hiyo na ikitokea Yanga akafungwa..tuta
pelekea Fifa ichukuliwe hatua ya kushushwa
daraja. Tena wachague wenyewe kushinda wawe na amani au wafungwe washushwe daraja.
Nawaonya pia tumepata taarifa Tambwe,msuva,
na ngassa wapo fiti ni lazima wacheze...wasif
anye ujanja ujanja wowote na wala hashangiliwi
mtu".
 
hahaha ...ila bongo soka letu haliendelei sababu hii utakuta yanga keshakua bingwa halafu anauza mechi kwa azam ukiangalia nje chelsea ni bingwa lkn hata kama unashuka daraja ukikumbana nae usubiri kipigo lazima ushinde kwa jasho lako sio kubebwa lkn huku afrika mambo ni tofauti kabisa mechi zinauzwa nje nje
 
hahaha bongo mona
 
Simba haina bahati ya viongozi, hivi walitumia vigezo gan simba kumpatia usemaje huyu Haiji Kung'ara?!
Jamaa poyoyo sana akili zake kama anakunjuliwa malinda.
 
Simba haina bahati ya viongozi, hivi walitumia vigezo gan simba kumpatia usemaje huyu Haiji Kung'ara?!
Jamaa poyoyo sana akili zake kama anakunjuliwa malinda.

mkuu lugha yako si nzuri ukiendelea hivi jiandae kulipa laki 7 kila siku ile sheria ikisainiwa
 
Simba haina bahati ya viongozi, hivi walitumia vigezo gan simba kumpatia usemaje huyu Haiji Kung'ara?!
Jamaa poyoyo sana akili zake kama anakunjuliwa malinda.
Haki sawa kwa wote
 
mkuu lugha yako si nzuri ukiendelea hivi jiandae kulipa laki 7 kila siku ile sheria ikisainiwa
Tatizo lake huyu jamaa ni mlopokaji sana, anatafuta umaarufu kila kukicha tena mara nyingine hatumii busara katika kutoa taarifa zake.
 
Ngoja niongee na Uongozi wa Yanga,Benchi la ufundi La Simba ndio wapange kikosi Cha Yanga.

Mikia mnahangaika sana, kuliko kumbeba Simba bora Azam atufunge tu, wa boti waendelee kupanda Boti tu Na wa ndege waendelee kupanda ndege.
 
Lakini viongozi wa simba wamesema wanajenga timu hivyo hawapo tayari kushiriki michuano ya kimataifa, sasa kuna ubaya gani kwa azam kufunga yanga ili watuwakilishe kwenye michuano ya kimataifa.
 
Lakini viongozi wa simba wamesema wanajenga timu hivyo hawapo tayari kushiriki michuano ya kimataifa, sasa kuna ubaya gani kwa azam kufunga yanga ili watuwakilishe kwenye michuano ya kimataifa.

Timu tulikua tunajenga msimu huu unaoishia. Msimu ujao tunaingia kamili, ndo mana lengo letu kuu ni kuchukua kila kitakachokua mbele yetu.. Hivyo hata tukishiriki shirikisho ni kama bonus tu.
NOTE: Tupo Tayari.
 
Ngoja niongee na Uongozi wa Yanga,Benchi la ufundi La Simba ndio wapange kikosi Cha Yanga.

Mikia mnahangaika sana, kuliko kumbeba Simba bora Azam atufunge tu, wa boti waendelee kupanda Boti tu Na wa ndege waendelee kupanda ndege.

Naunga mkono hoja.
 
hahaha bongo mona

Wenzetu hawapotezi mechi hovyo wanaweka historia,sisi tunakomoana
haiitaji akili sana kumjua mshabiki wa simba
 
Hahahahahaaaaa....endeleeni kuweweseka...mbona nyie kwenu haikuwa lazima kushinda mechi zote za ligi kuu?? Kama mngelazimisha ushindi kwenu katika mechi zote kama mnavoilazimisha yanga basi mngekuwa mna pointi 75 mnasubiri mechi ya mwisho mfikishe 78.
 
Umewaona Bayan Munich baada ya kuchukua ndoo kawaachia vitimu vidogo wamfunge ili visishuke daraja na cc tutakuwa na roho ya kiungwana kwa timu tutakazokutana nazo baada ya kuchukua ubingwa... alafu kwa nini tuwaumize kwa kuwafunga wakati watatupa heshima yetu kama mabingwa wakati wa kuingia uanjani...mtu akikuheshimu na wewe mheshimu bhana.
 
lakini anajua kwamba matokeo ya leo hayana maana yoyote kwao iwapo Azam atashinda mechi yake ya mwisho?
 
dah ah ah ha aha ha ha Haji mbona kanifanya nicheke mie.....

Kwa taarifa yake Msuva leo hayupo uwanjani, na hawana budi kutushangilia leo.

:glasses-nerdy:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…