singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Nimeandaa dume la ngombe, Oktoba 31, mwaka huu. Ukija hapa siku hiyo nakukaribisha katika sherehe kubwa nitakayoiandaa
nitachinja dume na kuwaaga viongozi wa Chadema watakaokuwa wamechaguliwa kushika dola kusherehekea ushindi.
Hiyo ni kauli ya matumaini. Ni kauli inayotoka mdomoni mwa Muasisi na Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Edwin Mtei, akielezea jinsi anavyoona na matarajio yake kwa Uchaguzi Mkuu ujao.
Nakukaribisha siku hiyo na huu ndio mwaliko wako, uje kusherehekea ushindi wa Chadema hapa nyumbani, kabla ya viongozi hao kwenda kuapishwa Dodoma.
Alikuwa akizungumza na mwandishi wa makala hii nyumbani kwake eneo la Shangarai, wilayani Tengeru, Mkoa wa Arusha.
Kauli ya Mzee Mtei imekuja siku chache baada ya Katibu wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, mwishoni mwa mwezi ulipita kuwa chama hicho kimeandaa mikakati ya kutwaa dola Oktoba, mwaka huu.
Golugwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, anasema hawataki tu kuwa na chama maarufu ila kuchukua dola, tena sio miaka mingi ijayo ila Oktoba mwaka huu.
Akiweka msisitizo, Mtei anasema uchaguzi mkuu ujao ndio utadhihirisha matakwa ya demokrasia.
Anasema Chadema itachagua mgombea makini mwenye maadili na sifa ya kuongoza nchi. Mtu mwenye upeo na mawazo ya maendeleo kwa wananchi na taifa.
SOURCE Nipashe