Sikia Shilole na Sinta wanalumbana katika Take one

Shilole alipotoka safari yake ya Marekani alijipaisha sana siku ya amplifier by Millard Ayo, ila leo tena nimejiridhisha kua huyu dada ni limbukeni. Pamoja na kwamba Sinta ana vituko vyake lakini Shilole kazidi kujikweza kupita kiasi hadi anakera.

Shilole ukipitia humu jf nakushauri uzingatie sana maelezo ya Sinta.
 


"Mimi nimefika hadi marekani, nimerikodia pale pale fifti santi anaporikodia, kuimba na jenifa ro(lo)pezi ndio nitashindwa?wewe sinta wewe, unikome kabisa" hahaha wadada wa dsm hao, wakijua tu kutongozwa na mapedeshee basi mtaani hatukai.
 
Ndio mastaa wa bongoland hao jamani.
 
ahahhaha ila sinta kaongea ukweli.....ahahahhahaha aisee alikua anatembea na taulo alipofika kule ahahahah
 
vituko vya mastaa uchwara wa bongo
 
Jenifa ROPEZI hilo ni jina tu kutaja inakuwa kazi

Kama sikosei tamasha lilikuwa ni la utamaduni wa kiswahili.

Aliyechaguliwa kuwakilisha kati ya watanzania milioni arobaini, ndio huyo hata kutamka hicho kiswahili ni mbinde.

Kweli Tanzania tuna kazi..........................labda kama kuna maelezo tofauti ili nisishawishike kufikiria kwamba rushwa imechukua mkondo wake.
 
Hii ishu tunaikuza bureeeee, ngoja nitumie uzoefu wangu wa kutatua migogoro ya nyumbani.

mmmmmh...tukio la karibuni pale nyumbani ilikuwa ni....mkid wangu wa miaka mitatu aliona ndege (aeroplane) ya KLM kwenye TV, akaniambia "baba ninunulie ndege" nikamuuliza "nikikununulia utaweza kuiendesha " akaniambia ataweza kuiendesha.....basi nikamwambia nitakununulia. Kaka yake aliyekuwa pembeni (miaka 10) akamzomea huku akimwambia kuwa hajui kuendesha hata baiskeli, mtoto akaanza kulia, ikabidi nianze kazi ya kumbembeleza.

Kwa hiyo tukirudi kwenye ishu......Shilole nyamanjha mwaya....tema mate nimpige shinta........utaimba kolabo mwaya na J Lo, Jay Z, Beyonce, Rick Rosee..(nisaidieni kuongeza wengine)

..................You see..........so simple....
 
Msikieni MA HOLDER.............J WAKE LO

"Ukifungua gazeti la babkubwa toleo
jipya ,kurasa ya katikati
utakutana na kichwa cha habari
MASTAA Ambao shule imelala
kichwani, seriously kuna siku mdau
alinitumia comment maana mimi na
magazeti ni hasi na chanya,
kilichoandikwa ni ukweli mutupu
jamani khaaa sasa mtu mwenye MA
apigizane kelele na mashoroko
mageni aaaah wapiii??
though babkubwa mmejichanganya
sana maana mmeandika ndivyo sivyo
one n only CEO anayetambulika ana
MA International Relations and
Diplomacy naomba ieleweke hivyo,
sijui kwa wengine mliowaja kama ni
sawa ama ila me mmenimixia sana
na ma post graduate ya nini mieee?
CEO's
MA International Relations n
Diplomacy
BA Public Administration and
Management (kwa wale ambao mme
cram BA hamkawii kusema Business
Admin khaaaa ni Bachelor of Arts in
PAM muelewe sasa.
hope tumeelewana ila sivibaya
nikawataja na wenzangu ambao tuna
hadhi ya kipekee (sio mchezo,,
sonyaa, kwanini ilikushinda kama ni
rahisi?? ukipata jibu utakuwa
umenielewa chezeyaa kufanya
research weweee)
Mwegelo Jokate
Black Rhino
Dj Fetty
Nikki wa Pili
Hamisi Mwinjuma
Ally Remtullah
na mwenyewe CEO wa ukweeeh
UJUMBE
unaweza ukawa kama hao hapo juu
ila acha majungu, umbea, fitina,
hela unazozipata kama ni
mwanadada usijipeleke kununua
lace wig, sijui Galaxy zichange
mdogo mdogo ujitupe kile chuo
kinaitwa V*** fasta .
The roots of education are bitter,
but the fruit is sweet.
okay byeeee..
Swaum Maqbul" Sintah
 

Na pale alipisema kiswahili kinataka kufanywa lugha ya taifa kwa mataifa yote ulipaelewa? nadhani alitaka kusema kiswahili kinakuzwa kiwe kwenye level ya kimataifa lakini sio kuwa lugha ya taifa kwa mataifa yote. Sijui nani alimteua dada poa kuiwakilisha nchi, ina maana hakuna wasanii waliopevuka kidogo kiakili na kishule hadi Tanzania iwakilishwe na mtu ambae hata yaliyojadiliwa hawezi kuyawasilisha???
 

Yaani hii bongo yetu kila kitu ni dili na ujanja ujanja, utakuta timu inajiandaa na mashindano nje ya nchi, wanahojiwa siku chache kabla ya kwenda unawasikia wanavyolalamikia maandalizi duni, sasa cha kushangaza safari ipo pale pale na wasindikizaji wa kumwaga. wanarudi mikono mitupu na ole wenu muwaite watalii...wanakunja ngumi...sio riadha, sio volley ball,sio football.........walah tuna laana.
 
pamoja na kwamba sintah ananiboa sana ila kwa hili shilole alivyojielezea dah yan kwenda America si mchezo kila la heri kwao wote peace and:love:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…