Kiangazii ya mwezi wa Saba Mwaka huu, kulitokea msiba Mtaani, siunajua tena mizizi ya ujamaa wa mwalimu Nyerere Bado imeshikamana kiaina.
Hivyo kuhudhuria, kuwafariji wafiwa haina budi, Mtu asipotia mguu katika msiba kwa Sababu mbalimbali, Bado ataonekana roho katili,roho isio na utu,roho ya hovyo,Ujamaa ni udugu.
Katika msiba, tukawa na jamaa mmoja tunazungumzia, mifumo ya ujamaa, ubepari, na historia ya Nchi Toka harakati za TAA &TANU (Sykes &Jk Nyerere).
Sasa Kuna wazee wastaafu wakawa wanatega masikio, nikazungumzia habari ya kambona Oscar &bibi titi na ushiriki wao katika Kujenga TANU, Kambona alivyokimbia Nchi, na Ujamaa wa mwalimu Jk Nyerere (Faida na hasara za Mfumo wa kijamaa zilizoletwa na Jk Nyerere).
Wazee wastaaafu baadhii Yao Jina la kambona Oscar halikuwa geni, haswa na nyimbo zilizoimbwa miaka ile, kambona kakimbia Ulaya, wivu wa mkereketa, Mwizi na nk.
Mzee mstaafu mmoja akanambia kijana unaonekana umesoma historia (Yeye mzee akimaanisha historia kama somo darasani,) nakamjibu Mzee yule, Hapana, Mimi nilisoma fizikia (Physics) & Hesabu (Mathematics).Lakini kwa sababu ninakiu ya kutaka kufahamu Africa na Watu wake, kwanini Nchi zinginee Duniani ni tajiri kwanini Nchi zinginee ni masikini (Jigsaw puzzle),na Tanzania/Tanganyika kwanini tuko hapa, tumetoka wapi na tunaelekea wapi, hivyo inanifanya nitatufute taarifaa na maarifa Kwa wingi.
Hiyo interview ya Oscar kambona , nadhani alikuwa Nigeria, anazungumzia Muungano wa Afrika haoni ukifanikiwa (Nchi zinamfumo tofauti kidogo ya Uendeshaji haswa, TANZANIA Ujamaa) na ikawa hivyo East Africa ilivunjika 77'.Oscar anasema TANZANIA kwa sasa ipo katika hali ya udiketa chini ya Mwalimu Jk Nyerere, inategemea pia wananchi watavumilia hali hiyo ya udiketa mpaka lini.
Rest in peace Jk Nyerere & Oscar kambona.