kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Takwimu za tume ya Taifa ya uchaguzi zinaonyesha wapiga kura waliopiga kura upinzani ni takribani milioni tatu kati ya milioni kumi na tano waliojitokeza na kati ya milioni 29 walioandikishwa.
Pamoja na watanzania hawa kuwa wachache kwa msingi wa tume ya uchaguzi ila mtaani inaonekana nguvu yao ni kubwa kuliko wale waliopiga kura chama tawala, hii nikutokana na nguvu yao iliyopelekea hadi sasa mawasiliano hayapo sawa kwa siku tano, wanavishughulisha vyombo vya dola, wanawashughulisha hata wale waliopitishwa na tume.
kwa nguvu hii walionayo wanaonekana wameshikilia uchumi na nyanja nyingine jambo linaloonyesha wazi kuwa si wakupuuzwa. Nafika wakati najiuliza ukiangalia ukubwa taifa leo kieneo ukalinganisha na mtawanyo wa hawa watu milioni tatu hatuoni kwamba kila kijiji wapo wapinzani wasiozidi mia ukilinganisha na maelfu ya wafuasi wa chama tawala? Hofu yetu tulioshinda ni nn? Kwanini tusiwaache waandamane sisi milioni hamsini na saba tukawalinda wafike wanapoelekea? Maana wakiandamana kwenda ofisi za tume kila wilaya naamini awatakua na nauli wote na wale waliopo mjini awatazidi elfu moja kwa wilaya na kati yao bado si wote watakaoandamana. Kati ya milioni tatu, toa watumishi wa umma, wafanyabiashara, wagonjwa, watu wenye ulimavu nk utagundua nchi nzima hawazidi milioni mbili, tuwaache wazungukezunguke wakipeana joto mjini kisha warudi wakapumzike sisi tuendelee kupiga kazi. Tunakosaje mawasiliano kwa ajili ya watu wachache?