Sikiliza video hii, uthibitisho kuwa Rais anapitia JF

Natamani rais ajae awe dikteta, yani dikteta wakweli, wanaomdhihaki mama huyu sijui wataonyesha wapi sura zao.
 
Angemuiga jiwe tu ile style yake ya kutafuna mahindi njiani.mwenzie hata kama alikua na madhaifu yake lakini alikua akiongea kila mtu anakua na hamu ya kumsikiliza
Sio kila mtu,labda wewe na familia yako.
 

Kipi Cha ukweli alichoandika hapo, kwani wewe huoni namna mh Rais anavyofanya kazi huko kwa wananchi, unataka aje hapo ulipokaa ndio ujuwe anafanya kazi, Rais anakwenda moja kwa moja huko waliko wananchi ambako ndiko alipita kuomba kura

Ndio maana unaona namna anavyo pokelewa na umati mkubwa Sanaa wa watu walio na kiu ya kumsikiliza Rais wao na kupata majibu ya baadhi ya kero zao

Sasa wewe endelea kulalamika hapa na kupinga pinga kila kitu wakati watanzania wanaendelea kuridhishwa na utendaji kazi wa Mh Rais wetu

Changamoto zilizopo anaendelea kuzitatua na kuzimaliza na zinazobakia zinaendelea kuwekewa mipango ya kibajeti kisera na kisheria
 
Yah walau tutakuwa na hamu na taarifa ya habari tena. siyo huyu bibi
Mh Rais bado yupo sanaaa tu madarakani maana watanzania tunaridhishwa na utendaji kazi wake, ndio maana unaona namna nchi ilivyo tulia
 
Rais wa nchi anao Uwezo Mkubwa.

Ndiye mtanzania anayepokea taarifa nyingi zihusuyo nchi hii kuliko mwingine; Lakini pia na yeye ni binadamu, anazo hisia.

Tuwe na heshima na sio kutoa kejeli hizi.
Wamemiss kupotezwa na wasiojulikana.

Neema mpaka ikuondokee ndipo utakapoijua thamani yake.
 
Huko FB, INST, TWEETER watu hawajasema kuwa hajazi? Isije ikawa tunajimwambafy japo inapendeza iwe hivyo.
 
Kwa bavicha waliojazana humu. Hata angekuwa Nani angejiunga humu
Hapana siyo wote. Mimi ni CCM damu, sina chembe ya upinzani, ni muhimu kumsaidia Rais Samia ili atambue vitu vya kufanya kwa ajili ya watanzania. Sisi ni wananchi wa kawaida wenye maslahi mapana na nchi. Rais Samia tunampenda mno tena sana sisi wana CCM ila linapokuja suala la maslahi kwa taifa na maisha ya watanzania ni lazima tusimame na watanzania kumuuma masikio Rais wetu ili ajue jinsi hali halisi huku mitaani
 
Kupokea taarifa ni jambo moja; uwezo wa kuzichakata na kuzifanyia kazi taarifa hizo ni jambo jingine tofauti.
Ni Rais gani kwa dunia ya sasa hajawahi kujibu hoja za mtandaoni?

Hapa nchini marais wote waliotawala enzi za mitandao ya kijamii tuliwasikia wakijibia/kutolea ufafanuzi hoja mbalimbali za mitandaoni, wote JK na JPM. Kwa nini iwe nongwa kwa SSH?
 
Ni Rais gani kwa dunia ya sasa hajawahi kujibu hoja za mtandaoni?
Hoja mitandaoni kumhusu rais ni nyingi sana, hawezi kupata muda wa kuzitolea majibu zote.

Ni mtazamo wangu kuwa hii aliyoitolea majibu haikuwa na umuhimu wowote. Labda kama ni umbea kama alivyosema mwenyewe.

Wananchi wanataka majibu ya hoja nyeti zinazojadiliwa humu zinazogusa maisha yao directly.
 
Dikteta aongoze familia yake,sio nchi.

Sindio baadhi yenu mnachokitaka!! Huyu mama na upole wake lakini anaonekana bado hafai, na among them hawampendi kutokana na imani yake na vile vile ni mzanzibari, na ana ndugu zake oman.

Ndiomaana nikasema hii nchi dawa kupata dikteta mtu anaeleta ujinga apotezwe, labda wanatamani iwe hivyo,,,,hapo ndipo watammis huyu mama mwenye huruma na utu.
 
Raisi hachaguliwi ili awe mpole au dikteta, raisi anachaguliwa kuleta maendeleo.

Raisi akikosea atapingwa, iwe hadharani au sirini. Ingekuwa sifa ya uraisi ni upole wala kusingekua na haja ya kufanya kampeni na kuwaahidi watu mambo mengi.

Kuhusu dini na uzanzibar hiko ni kichaka Cha kutaka watu wasimkosoe, haiwezekani atakosolewa tu. Nyerere alikuwa mtu wa bara na mkristo alipingwa kwa nguvu zote, mwinyi alipibgwa kwa nguvu zote, mkapa alipingwa kwa nguvu zote , JK na Magufuli walipingwa kwa nguvu zote. Hivyo hata huyu atapingwa tu tena kwa nguvu zote. Hii hali ya umaskini uliopo hakuna namna watu wataacha kutukana viongozi.

Mwisho ukitaka usipingwe Wala kutukanwa, acha uongozi
 
Siamini macho yangu! Ni wewe huyo au account imedukuliwa
 
Hayo mafuriko ya mchongo tunajua yanavyopatikana.
 
Ninyi ndo mmeikuza hii habari hata kuleta hii thread; Mngeipuuza hiyo habari kama mlivyotaka yeye apuuzie, kisha mkaleta hayo unayoita ya msingi ambayo anaendelea kuyatolea ufafanuzi akiwa na mawaziri wake huko kwenye ziara ili tuyajadili.

Huoni tumepoteza muda mrefu kujadili hili jambo ambalo lilikuwa kijisehemu tu cha hotuba yake iliyozojaza mambo mengi ya nchi hii? Vipi, tungejadiliana kuhusu elimu, afya, kilimo, uchumi, miundombinu nk?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…