Sikio la kufa daima halisikii dawa.

Sikio la kufa daima halisikii dawa.

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam

Nimesikiliza interview ya Ezekiel Wenje iliyofanyika wasafi fm nikagundua kuwa huyu mtu ni nusu mfu na anachowaza ni ruzuku tu na madaraka. Asema eti Abdul ni mtu muungwana sana na mkarimu, kweli leo ccm wamekua wema kwake na chadema? Tangu lini? Ukimwangalia anavyoongea unaona kabisa haamini anachoongea na anawaza pesa za Abdul.

Pili inashangaza mpaka sasa hakuna mwanachadema aliejitokeza kugombea nafasi ya makamo mwenyekiti anayogombea wenje hii ina maana mbowe amedhamiria achukue uenyekiti kisha huyu wenje awe makamu mwenyekiti, kwa muktadha huu ina maana wenje nimgombea pekee ktk nafasi hyo.

Mwisho kama chadema itakuwa na makamu mwenyekiti km wenje ni dhahiri mwenyekiti anaenda kuwa mbowe na hapo ndo kitatokea kifo cha chadema maana haitawezekana lissu awe mwenyekiti halafu makamu awe huyu dalali wenje. Kwa ufupi chadema imeshakufa bado mazishi yake tarehe 25/01/25
 
Ngoja wale ruzuku za mwishomwisho naona kila mmoja ameamua aondoke na fito zake
 
Back
Top Bottom