You want my take? Mr Mwinyi is a good principled man. He is his own man and he will do his own things in his own time as required by the law and what he considers are his priorities. Ni mtoto wa Mwinyi, yes, kwani wewe huna baba? Ni CCM, yes, ndiyo sheria nIinavyosema. UAMSHO hakuwafunga yeye, wala baba yake, wala Magufuli, walifungwa enzi za Kikwete kwa misingi ya kisheria kadiri alivyoona inafaa. Hawa ni magaidi, treatment yao si ya kawaida. Uamsho tangu amani nao walitoka Pemba huko huko walilipua Ubalozi wa Amerika enzi za George Bush na Ben Mkapa, wako gerezani Guantanamo mpaka leo. Baadaye wamehamia Kibiti Lindi ni Msumbiji, ni nani anataka watu waangwmizwe na magaidi? Mwacheni Rais atekeleze Ilani za Chama chake. CUF na CHADEMA na tundulissu waliahidi kuwa wangewaachia Uamsho mara moja, mbona kura kazikutosha? Jibu ni kwamba Uamsho si priority ya wapigakura hivi sasa, quite to the contrary!
LGF,
Nimesoma jibu lako kuhusu Rais Mwinyi lakini mimi nataka nichangie kwenye suala la ugaidi peke yake.
Mwaka wa 2006 niliwasilisha mada ''Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience: "Islam, Terrorism and African Development.''
Nimeeleza katika mada hiyo kuwa suala lolote nchini petu likihusishwa na Uislam na Waislam tayari patakuwa na matatizo.
Uislam nchini petu ni suala nyeti sana na hili tatizo linakua kila miaka inavyozidi kusonga mbele kwa jinsi Waislam wanavyowekwa nje ya serikali na vyombo vyote vya maamuzi hivyo wao kuwa wachache katika uendeshaji wa nchi.
Hili limewaathiri sana Waislam.
Huu uchache ni katika kila kitu kuanzia nafasi za elimu katika vyuo vikuu hadi ndani ya serikali yenyewe na Bunge.
Uchache huu wa Waislam ndani ya Bunge ndiyo uliwezesha Sheria ya Ugaidi kupita kirahisi.
Kuna walioona kuwa hii ni njia moja ya kuzidi kuudhibiti Uislam nchini.
Vipengele vingi vya sheria hii ni vya uonevu na dhulma kubwa.
Hadi hii leo mahakama Tanzania haijaweza kumtia hatiani mtu yoyote kwa kosa la ugaidi.
Kuhusu hilo suala la Rufiji na Kibiti laiti kesi za watuhumiwa wa ugaidi hao zingekwenda mahakamani tungenufaika na mengi na kubwa ni kule kuwatambua hao ''magaidi'' na kusikiliza utetezi wao kuhusu shutuma hizo.
Uamsho si magaidi na hadi leo mwaka wa nane upande wa mashtaka hawajaweza kuleta mahakamani ushahidi wa tuhuma hii.
Hii nini maana yake?
Maana yake ni kuwa vyombo vya sheria vimekamata kwa ushahidi wa ''hearsay.''
Kwa kukosa ushahidi wa kuwa masheikh hawa ni magaidi ndiyo hadi leo kesi mwaka wa nane haijazungumzwa.
Masheikh wamewekwa rumande kinyume cha sheria.
Hili ndilo alilosema Nguruvi3.