Siku 30, halafu? Serikali ije na mikakati thabiti ndani ya siku 30

Siku 30, halafu? Serikali ije na mikakati thabiti ndani ya siku 30

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, hii ikiwa ni pamoja na kufunga shule zote, na ligi ya mpira kwa siku 30 kuanzia Machi 17, 2020

Hakuna uhakika kwamba ndani ya siku 30 ugonjwa huu utaondoka, inawezekana ukawa na nguvu zaidi ya ulivyo sasa au ukadhibitika ndani ya siku hizo. Kama hautadhibitika ndani ya siku 30 hizi je tutaongeza siku nyingine 30?

Zinahitajika hatua za haraka ambazo zitatufanya kupunguza maambukizi bila kuathiri sana uchumi. Serikali yapaswa kusimama kwenye matamko ya sera ya afya ya mwaka 2007 kuhusu magonjwa ya kuambukiza na mlipuko.

Inapaswa kuwa wazi kusema juhudi itakazozifanya ndani ya siku hizi thelathini, ili ijulikane kama ugonjwa utaendelea, ni kwa namna gani shughuli nyingine zitaendelea. Siku 30 sio mgomo wa nchi dhidi ya ugonjwa, bali ziwe ni siku za kujipanga kwa mikakati thabiti ya afya ambayo itahusisha wadau wote wa afya nchini.

Serikali inapaswa kuja na maazimio ndani ya siku hizi thelathini ili kutoathiri uchumi kwa kusitisha shughuli ambazo ni muhimu kwa jamii. Waliokuwa wanawauzia chakula wanafunzi hadi sasa tayari wako matatani.

Hizi siku thelathini sio kuwa zitawacost raia peke yao bali hata serikali pia, wataendelea kuwalipa wafanyakazi wote stahiki zao, japo hii sio likizo.

Wauza vyakula kwa wanafunzi watakosa cha kufanya na wataumia pakubwa kiuchumi.

Masuala ya ligi pia yatawaathiri walikuwa wanafaidika kwa ligi hizo.

Nchi zilizoendelea zikipiga chafya, Afrika inapata mafua. D Trump alisema, kwa hili tuende kwa muono mkubwa kuliko kuwa mafala, ugonjwa ukaondoka na ukwasi kidogo tulionao.

Signed

Oedipus
 
Unauliza maswali mepesi sana.

Hizo siku 30 ni za kutazama mwenendo wa ugonjwa kama utazidi kuwa mkubwa ujue bado mikusanyiko shule zitaendelea kufungwa.
 
Is the only way to appear like we are doing something. Ila kiukweli yametufika hapaa. Hakuna cha plan a wala b. Umy mwenyewe kaishia kucheka tu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unauliza maswali mepesi sana.

Hizo siku 30 ni za kutazama mwenendo wa ugonjwa kama utazidi kuwa mkubwa ujue bado mikusanyiko shule zitaendelea kufungwa.
Weka 30 mara tatu halafu niambie matokeo yake kiuchumi kwa nchi inayoendelea kama hii
 
Weka 30 mara tatu halafu niambie matokeo yake kiuchumi kwa nchi inayoendelea kama hii
Kwahiyo tumependa maisha hayo au? Hiyo ni dharura kama vita uwe unaendelea au huendelei utapaswa kuingia kwenye tahadhari.
 
Sisomi hayo mapendekezo ila ujue hii ni kama vita hadi siku tushinde mapambano hayo.
VITA! chukua hii strategy ya vita... knowing yourself and knowing your enemy, in hundred battles you will never be in a peril. Sun Tzu
 
Back
Top Bottom