Mara nyingi wananchi hasa watanzania wamekuwa na hamu sana kusikia au kujulishwa kuwa CHADEMA tukichukua nchi na kuunda serikali kama chama tawala nini tutafanya kwenye hili taifa. Kwanza kabisa wananchi watanzania watanufaika na uhuru wao na haki za binadamu. Kila mtanzania atakuwa huru kutoa maoni, kulalamika, kukosoa, kushauri, kupinga na hata kumzodoa kiongozi atakayekuwa ameshindwa kutimiza wajibu wake.
Kuhusu Katiba na Utawala wa Sheria. CHADEMA tukiingia madaraka, nchi itakuwa na Katiba mpya. Kila mtu atakuwa chini ya sheria mama ya nchi. Hakuna mtu atakayekuwa na kinga ya kutoshitakiwa mahakamani. Kuanzia Rais, atakuwa anawajibika kwa wananchi na mwananchi (raia) au taasisi itakuwa huru kumshitaki Rais mahali popote kama mtu na kiongozi wa nchi.
Mamlaka ya Rais yatapunguzwa mfano Rais atakuwa sio wa mwisho wa kutoa amri kwenye vyombo vya dola, Rais hatakuwa na mamlaka ya kuteua mtu kwenye nafasi yoyote bila ridhaa ya Bunge na Kamati ya Kimahakama ya uteuzi.
NI BAADHI YA MAMBO AMBAYO CHADEMA TUTAFANYA TUKIWA KAMA CHAMA TAWALA.
Wadau wengine ongezeni ili watanzania wajue.