Siku gani ulichacha hutaisahau?

Siku gani ulichacha hutaisahau?

Ameeennn....

Hiyo ilikuwa budget ya leo, kesho na kesho kutwa! Ndo maana nikatembea mpaka kituo cha bus, kuna mwendo wa 1.5 km!
hela ya nauli mbona husemagi

Yani mpaka ukutwe na bwana Pepsi njiani kama hivi.
 
Kuna siku nilichacha siwezi kuisahau maishani. Nilibakiwa na 10,000/- mfukoni. Sasa nilikuwa najisikia vibaya nikaenda kupima malaria nikawa ninayo. Nikawa njia panda, ninunue dawa au chakula maanake huwezi kunywa dawa bila kula ikabidi ninunue msosi tu nikala nikalala na malaria yangu. Kesho nikapiga mishe nikapata hela ya dawa na chakula
ko kubaki na 10000 n kuchach bro?labd km matumiz yak n zaid ya hyo pesa per day

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2015 nikiwa na mshikaji wangu mmoja, kazini kulikuwa na mambo ya ajabu hivyo pesa ilikuwa haipo.

Imefika tarehe 24 Des hakuna msosi ndani hata wa panya kula, nikamuuliza mshikaji vipi tunafanyaje na hali hii. Akasema sisi ni wanaume hatutakufa njaa kwa siku moja hivyo tuvumilie. Tukafanya maajabu jioni tukapata unga na mboga tukala.

Des 25 Asubuhi tunaamka wote kama kima hakuna mwenye wazo la kwenda kazini ila kila mmoja anawaza atakula nini, wazo likaja kuna mama mmoja ni rafiki yetu huwa anatuuzia sana mboga na muda mwingine anatukopesha kama hatuna cash, yeye alikuwa anatuita Magufuli na Lowasa kwani kipindi hicho hayo majina yaliteka nchi sana na pia muda wote tulikuwa tukiongozana na yule mshikaji.

Tulienda hadi gengeni hiyo ilikuwa saa 6 na pale tulipokuwa tunaishi walitutambua kwa sababu ya ucheshi wetu, majirani asubuhi wanauliza mbona hakunukii huko kwenu sisi hatuna muda nao njaa imeanza ku-take off kwenye runway. Wakati tunaondoka kwenda kwa yule mama kukopa mboga huku nyuma tukaacha vumbi, tuliwaambia majirani pikeni ila sisi tukirudi hapa tutafanya kufuru [emoji23] [emoji23] [emoji23].

Tumesogea hadi gengeni ili tupate mboga kwa yule mama ila hatukuamini tulichokiona pale gengeni. Yule mama hakuwepo na walikuwepo tu wauza nyanya, nikiwa bado najaribu kushirikisha moyo wangu nilichokiona ghafla nikaona demu wangu anatoka salon na rafiki yake pamoja na mtoto wa huyo rafiki yake.

Demu wangu alikuwa anakaa mtaa mwingine na rafiki yake alikuwa anaishi mtaa ule hivyo alikuja kwa rafiki yake siku ile ili wajiandae kwenda beach. (sikuwa na maelewano mazuri na yeye wakati huyo)

Akaniita na kuniuliza mbona mko hapa mchana huu mnafanya nini, nikamjibu tumekuja kununua nyanya tukapike mboga , akauliza mmepika nini nikamjibu KUKU. Wakaaga na sisi tubaki na maswali tutakula nini mtegemezi wetu hayupo (yule mama).

Mshikaji akasema oooh nimekumbuka nina shangazi hapa mjini, akapiga simu kwa shangazi yake kumuuliza kama yupo nyumbani na akasema yupo akamtania mshikaji njoo leo kwangu basi. Oooh alitania pasipo na dakika hiyohiyo tukaondoka na kwenda kwake, alikuwa kajiandaa vya kutosha tulikula na kusahau shida zetu na jioni ikafika sasa turudi kulala.

Majirani wakati huo wanasubiri kishindo chetu kumbe mikwara tu hatuna hata nyanya, tulifika kila mmoja akaingia ndani kwake kimya na kulala, haujapita muda mshikaji akanigongea oya leta sufuria kubwa, nikampa kumbe majirani wametuchagia chakula kama wahanga wa kimbunga. Aisee kile chakula kilikuwa kingi tukala siku mbili kingine tukamwaga maana kilituzidi.

Chakula mseto: nyama ya bata humo humo, ya kuku, ya ng'ombe, ya mbwa, ya bundi.
Ha haa mzushi wewe eti ya bundi
 
ko kubaki na 10000 n kuchach bro?labd km matumiz yak n zaid ya hyo pesa per day

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma vizuri utaelewa. Weka hio 10,000 pembeni, concentrate on the situation.
Unaweza kuwa na 200,000/- mke wako kajifungua hospitali wanadai 200,000/- ili uende nae nyumbani. Ukitoa hio 200,000 unaishiwa Hadi nauli ya daladala kuwafikisha nyumbani,bado hamjala,hujanunua bitu vya mama na mtoto etc. Sasa hapo utasema huyu hajachacha kisa ana 200,000? Fikiria situation
 
Kwasisi malegendary kuchacha siyo issue tena, mana tushakuwa na episodes na experience za kutosha sana za kuchacha sana, achana na hii kuchacha sjui huna ela ya kula alafu upo mwenyewe achana nayo hy, kuna ile unachacha alafu una familia ya watu kadhaa na pmj na watoto wadogo alafu wewe ndy sterling....!! Acha tu!

Ila katika experience zangu za 'kufulia', ambayo sitikuja niisahau ile ya mzazi wangu wa kiume aliposimamishwa kazi wakati yeye akiwa tegemeo kwa familia yake, ulitokea kipindi nimemaliza form 4 miaka zaidi ya 23 iliyopita na matokeo yakatoka nimefaulu, na mama yangu kipindi hicho ni mjamzito, tumepanga chumba kimoja kwe zile nyumba za national housing za kizamani zinazopatikana ilala, kinondoni na magomeni. Chumba kimoja watoto wakubwa 3, baba na mama wanalala humo humo.

Hakuna siku nilitoa machozi kama siku baba alivyoniambia 'mwanagu siwezi tena kuhudumia familia sina tena kipato', mzazi hakuwa na elimu ya juu, hata kazi aliyokuwa akifanya ni kama 'office attendant' tu, kwahy hata kipindi anapata mshahara ulikuwa hautoshelezi, sasa unaweza emagine maisha bàada ya kusimamishwa kazi yalikuwaje. Nikiwa kama mtoto wa kiume ilibidi niumize kichwa kweli kweli, ni namna gani nitaweza isaidia familia...nilifanya kazi ambazo sikuwa na ujuzi nazo hata kdg na za risk kama 'fundi umeme. Story ni ndege na ya kusikitisha.

Lakini nashukuru yote kwa niliweza enda advance sec. Na kumaliza kwa kupata division one, japo nilisoma kwa shida mnoo. Leo napoandika uzi huu alhamdulah nimepiga hatua kidogo kibongo bongo, ni msomi wa chuo kikuu, own house, nasukuma beautiful SUV, own some business, nina familia nzr, na mmb mengine kibao, kitu ambayo unapaswa ujuena ujifunze kutokana na matatizo ya kifedha ni kuwa " Unajifunza namna nzr ya kukabiliana na changamoto, na pia hukusaidia kujua marafiki wa kweli a wenza wa kweli, watu wamepoteza wenza wao na marafiki kutokana na masuala haya, lkn, pia kuna watu imewaunganisha zaidi....ILA bado suala la kupigika lipo pale pale, kuna kipindi unakosa pesa mpka unakufuru Mungu.
 
Inspiring story
 
Pole sana....! I feel you, lkn mkuu ukiona unasuasua au unajibana sana kulipa ada ktk hizo shule, basi jua kuwa uwezo wako ni mdogo, usijilazimishe (huu ni ukweli mchungu), hata mimi binafsi suala la ada kwa mtoto huwaga changamoto, ila nimepanga na mwenzangu kukaa na kureview upya......ni kweli tunapenda watoto wetu wasome shule bora kbs, lkn ukweli ni kwamba uwezo wetu kutokana na majukumu ni mdogo, ada zimekuwa too much nowdays. Na hili nakuhakilishia siyo wewe tu, wapo wengi mnoooo, ambao wanashindwa na ada za hizi shule....ni vile tu hujapata wasaa wa kuona list ya wanaodaiwa wenzako.

Zamani Kulikuwa na option ya kuwapeleka watoto shule za serikali za English medium kama Olympio, diamond etc. Kwa hapa Dar, lkn hv sasa hizo shule hazina tofauti na za kayumba za kawaida, na kwa hali ilivyo hivi sasa mtoto kusoma shule ya English medium siy tu fashion, Bali ni lazima sana, sababu huko mbele mfumo wa ajira na elimu utabadilika sana, so ukimpeleka mwanao shule za kayumba tulizosoma sisi, utakuwa umemnyima fursa nyingi sana kwa kizazi chao huko mbele.

Mwisho lengo la kukuambia ukae na wazazi wenye same problem, ilikuwa uweze kupata faraja au hata utatuzi wa shida yako. As you know penye wengi pana mengi, unaposkia mtu mwengine ana tatizo kama lako, unapata psychological relief, na inakusaidia kuona ur not alone.
Sasa mkuu tutajadili nini? Wenyewe wanatuambia Kama huwezi muhamishe mtoto, unashindwa maana shule Ina vigezo vyote ambavyo unavihitaji kwaajili ya mtoto wako. Labda serikali iingilie Kati hizi shule binafsi kitu ambacho naona Ni ngumu kidogo.
 
noted hata usijali nimeliona; au tukakae down town in lemutuz voice tuwe jirani na le akili kubwa, tusipate shida ya usafiri.
Hahaha hahaha
Usijali kabisaaa babaa, mie nishazoea kuchanja mbuga nauli ikikosekana..
 
Hahaha hahaha
Usijali kabisaaa babaa, mie nishazoea kuchanja mbuga nauli ikikosekana..
Utaanzaje anzaje kuchanja mbuga tena kwa mfano, labda watu wasiojulikana wanichukue. Kuchanja mbuga tuachie sisi pastoralists.
 
Kipindi baada ya kumaliza chuo kabla sijapata pa-kujishikiza. Niliondoka home mkoa nikaja mjini kupambana maghettoni na masela ambao bado hawajamaliza chuo kipindi hiko.

Nilifulia ile mbaya, tunapika mara moja tu kwa siku mpakani mwa jioni na mchana, tena wali mkavu na mara moja moja tukipata basi ni majani.

Ponapona yangu siku moja "dogo" alitoka mkoa akaweka pause mjini daslam,kuja magetoni kunicheki akaona hali ilivyo mbaya, kesho yake kamalizia safari kurudi home akawapa feedbck hali aliyonikuta nayo sio njema. Mzee kwa huruma akanitumia 250k kwanza inisaidie katika harakati za kuzungusha bahasha na kupunguza ukata.

Dah siwezi kusahau kile kipindi ingawa home mambo yalikua yanaeleweka ila niliamua nipambane kivyangu na mimi nipate nuru. 1 year (later) now since then, my hero has passed away but namshukuru mungu nimeshaanza "kusimama dede" ko hakuna kinachoyumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom