Siku Heche akirudisha posho alizolipwa akiwa mbunge nitakubalia na unafiki wake

Ameanza kupinga tangu akiwa bungeni acha porojo
 
Mbona mtoa mada nimemuelewa hoja yake mnamshambulia kwa maneno tatizo lipo wapi hapa tujenge hoja
 
Alikokosoa labda ka hukua unafuatilia,alikosoa Hadi while kuwa viongozi watoto wao wanasoma international,watanzania mmelogwa na hamtopona,hasa wewe
 
Wajinga ni wale wanaozitoa heche ata wakilipa 2m anapokea Wajinga ndo waliwao mleta mada wewe ndo mnafiki mkubwa.ukiamjiri fundi kujujengea nyumba badala ya kumlipa posho halili labda ya shs 30,000 kwa kutwa ukamlipa 200,000 yeye hawezi kukataa.mjinga ni mtoaji sio mpokeaji .
 
Wewe sio CCM hakuna mwanachama hata mmoja mwenye kadi ya tangu 2000

Zilishabadlishwa hakuna hata mwanachama mmoja kadi yake inasoma hiyo miaka
Uelewa wako mdogo sana mkuu. Alichokosea heche pale ni nini? Speaker aliyefukuzwa ndugai alisema serikali inakopa sana? Siyo kweli? Mbona hajasema alipokuwa speaker? Jk alishawahi sema watu huko ccm hawaachiani hata glass za maji! Siyo kweli? Mbona hakuyatamka hayo alipokuwwa mkt!?
 
Wote wachumia tumboni,hypocrite,
Hawana tofauti na wale wanaowatuhumu.
Tofauti yao na wale hawajapata nafasi.
Tunataka mgombea binafsi tuwapime wao kama wao sio visingizio kupitia vyama.
 
Heche hajasema kama aliwahi kurudisha posho hizo kwa katibu wa bunge kuupinga ni kubwa. Huu ni unafiki inaonesha kesho akirudi bungeni atazifurahia.
Watu mna argument za kitoto unajua eeh? Sasa Heche akirudisha posho zake ndio zitainua mishahara ya walimu?

Heche anachotoa hapa ni analogue, sijui kama unaelewa maana yake, kwamba marupurupu yamelenga kufaidisha watu wachache huku wengine kama walimu wakisahauliwa, sio kwamba anapinga wabunge kupewa posho. Anachosema ni kwamba wakati wabunge wanafaidika na posho kama hizo, walimu wanakuwa wamesahaulika kitu ambacho sio sawa. Wafanyakazi wote, uwe mbunge, uwe mwalimu, uwe askari magereza nk, wana umuhimu sana kwa Tanzania.

Miaka ya 1980 Nyerere alikuwa akikataa wafanyakazi wa NBC kujilipa bonus kwa sababu NBC ilikuwa ikitengeneza faida kubwa sana. Alikuwa akiuliza na walimu wao bonus zao zitatoka wapi, maana nao ni wachapa kazi hodari kuliko hata nyie watu wa NBC

Hivi wengine mlienda shule gani? Tuambie, umesoma hadi kiwango gani unakurupuka kuwaita watu wanafiki bila kuelewa point zao? Na wewe ukiitwa poyoyo wa kuelewa mambo utafurahi? Maana hii thread yako inaonyesha kiwango kikubwa kwamba huna akili ya kuelewa arguments za watu.
 
Moja wapo ya ahadi ya mwana TANU ni "Nitasema ukweli Daima,fitina kwangu mwiko" na Leo Nitasema ukweli kama mwanaCCM unafiki sitaki.

MwanaCCM umeamua kutumia ahadi za mwanaTANU! Ahadi inakutaka useme kweli daima, wewe umeamua leo ndio useme kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…