Siku hii Dream itakapotimia: JF Members SACCOS LTD

Hii kiadia ni nzur ila kiutekelezaji maxima iwe shughuli haitaki uvivu hata kidogo afu inahitaji member wakujitoa haswa kusiwe na wababaishaji
Nimekuelewa sana; haitaki uvivu hata kidogo, inahitaji kujitoa na kusiwe na ubabaishaji.
 

Mkuu nimekuandikia hapo juu. Naamini kwenye utekelezaji wa wazo linapokuwa la moto Kama hili. What’s way forward so far.
 
Mkuu nimekuandikia hapo juu. Naamini kwenye utekelezaji wa wazo linapokuwa la moto Kama hili. What’s way forward so far.
Way forward ni kutafutana wawili watatu tunaoamini katika hili wazo, halafu tunapanga mikakati namna ya kusonga mbele.
 
Jf haina member laki 4 lakini inazo I'd laki 4
na ndani ya hizi I'd wapo waliokufa,wapo watoto na kila sampuli ya watu!

kuchukua I'd zote hizo ni mzigo,na kitu kikiwa.na watu wengi ni mzigo mbeleni.

Tuanze na watu wachache ambao wataweza kujitoa muhanga!.

tukiwa na watu 100/200 ni kianzio tosha
Mf tuchukue watu 100 na kila mtu akitoa elfu 100,000
100,000×100=10Million
Hiyo pesa inaweza kuzungushwa vizuri kwenye biashara ya kuelekewa na ikazalisha zaid ya hiyo!.

Mimi naweza kuwasaidia Jinsi ya kuzalisha pesa na ku plan biashara kwa Mtaji mdogo.

ujue katika wengi,kuna migingano mingi!.
Au tungeanzisha Jf zone Hapo sawa.
kuliko ku conclude member wote!
Na hili swala litakuwa ni 'HIYARI'



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa, umeeleweka vizuri sana. Ngoja tuendelee kusikilizia wengine.

Ila pia ingependeza aidha unitumie PM ama hapa unaweka ni namna gani ama aina gani ya biashara zinaweza kufanyika kwa mtaji mdogo Genius Man
 
IDEA yako nzuri sana. Naomba uongozi wa JF uliangalie hili wazo kwa maslahi mapana ya Jukwaa letu. Normal is real boring

JF lisiwe tu jukwaa la Great Thinker pia liwe jukwaa la wajasiriamali na matajiri wajao wenye fikra na mawazo pevu.



Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Mkuu TheLobbyist kama tumekubaliana wazo ni zuri pasi na shaka, napendekeza tukutane this Sunday Saa 8. Venue chagueni ila maeneo ya sinza, wenge au kijitonyama are more convenient
 
Mkuu TheLobbyist kama tumekubaliana wazo ni zuri pasi na shaka, napendekeza tukutane this Sunday Saa 8. Venue chagueni ila maeneo ya sinza, wenge au kijitonyama are more convenient
Sawa kabisa, ngoja tuendelee kuona wadau wanasemaje
 
Sawa, umeeleweka vizuri sana. Ngoja tuendelee kusikilizia wengine.

Ila pia ingependeza aidha unitumie PM ama hapa unaweka ni namna gani ama aina gani ya biashara zinaweza kufanyika kwa mtaji mdogo Genius Man
Ngoja kwanza,tuangalie hili varangati linaendaje
Na pia Tucheki,muhamko wa wadau humu.hata ukija kupata member 50 lakini wenye Nia na udhubutu! Tutatoba na saccos Yetu

Tuangalie kwanza idadi ya member ambayo,itakuwa ndani ya plan yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa member wa jf ni baraka tosha kwangu, am ready to that.

Ila ili wazo gumu kutekelezeka ilo alipingiki Luna jamaa hapo juu kuongea kitu sensitive kuhusu kuform jf zone na kuwa na watu 100 tu, hapa naona ili wazo liwe rahisi litokee kwenye jf zone.

Iko hivi
JF zone wa Temeke wapo 100 wameungana wamechanga pesa 10M wanazalisha hivyohivyo Ilala, Kinondoni then baada ya mafanikio ya zone mfano kila zone imeweza kumake mtaji wa 100M wakiungana ni 300M so DSM tu ina 300M kwa watu 300........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja yako inataka kuingilia uhuru wa jukwaa.
Huwezi kuwa mwana hisa ktk uwekezaji kama huu bila kuwa na taarifa sahihi za wadau.
Nahisi unachotaka ni identity .
Dhumuni la JF ni platform huru ya mawazo mtambuka.
Be warned!
Liache jukwaa libaki kama jukwaa tena huru.
Lakini kuligeuza jukwaa bank, haileti afya, it's a kind of threatening tool I guess.

Unadhani kwa nini bank zina disclose taarifa za wadau wao kwenye vyombo vya kiutawala?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…