Bigirita
Platinum Member
- Feb 12, 2007
- 16,039
- 7,465
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii inahitaji Verfied user. Make hapo wewe mfano nani atakuamini? Si una jua now day?Updates:
Kwanza, naomba kuwashukuru mapenzi wanaounga mkono mchakato huu na wale wanaonyesha dalili za kuunga mkono safari hii. Ahsanteni sana kwa niaba ya JF Members SACCOS.
Nitakuwa naweka updates kwa kadri ninavyozipokea na kuona zinafaa, lengo ni kuonyesha muelekeo wa hili wazo. Hata tukianza wawili tutajaribu kwa nguvu zetu zote kuona hili linafika wapi.
Kuna member mmoja ameniuliza inbox. Je, ni lazima ID yake itambulikane kwa umma wa JF?
Nikamjibu:
Nionavyo mimi kwa sasa (japo sijui wanachama wengine watakuja kuonaje baadaye) ni ngumu ku monitor ID za wanaJF. Naona tu maadam mtu ni mteja wa JF kwa maana ana visit JF awe kama member ama guest huyo tayari anafaa kuwa mwanaSACCOS
Mkuu mimi katika ili sioni tatizo na kwasababu kutakua na sheria na taratibu mimi sion tatizo mimi nakubaliana na wewe na moja kwa moja mimi niwe member no 2 kutoka wewe kwa vyovyote vile itakavyokua tafadhaliDunia inaenda kwa kasi sana, watu wanazidi kuongezeka na uzalishaji wa chakula unazidi kupungua. In fact gharama ya chakula inazidi kupanda siku hadi siku.
Kama haitoshi, tatizo la ajira linazidi kuwa sugu kila kunapokucha. Maelfu kwa maelfu ya vijana kwa wazee wanazidi kupoteza nguvu kazi kwa ku bet, kukaa vijiweni, kujadili Yanga na Simba, nk. Huku matatizo ya kijamii yakizidi kuota sugu kila kukicha, vijana kwa wazee wanakosa nguvu za kushughulikia, hawana uwezo hasa financial support.
Kama members wa JF, ambao ki msingi jamii inawatambua kama 'The Home of Great Thinkers' wakaamua kuumiza akili namna njema ya kutengeneza ajira na kuzalisha mitaji ili vijana na wazee wajiajiri.
Kuna eneo mathubuti sana la kutengeneza AJIRA za uhakika na KUZALISHA MITAJI kwa vijana na wazee nalo ni eneo la kilimo. Hapa vijana wetu, na wazee wetu watazalisha chakula na pia watazalisha mitaji yao kwa ajili safari ya maisha yao ya kujiajiri.
WanaJF wanaanzisha SACCOS itakayokuwa Limited.
Hii SACCOS inapewa jukumu moja tu: Kubuni mbinu za kutengeneza ajira za uhakika na kuzalisha mitaji kwa ajili ya wanachama wake.
Uhakika nilionao ni kuwa ukiwa na mtaji wa kutosha TZ kila biashara (almost) inalipa. Isitoshe hakuna biashara yeyote mpya duniani, ni kuiga tu biashara profitable na kuwekeza pesa then usimamizi mzuri maisha yanaenda.
> Tuna target kwenye kilimo
> Uagizaji wa bidhaa toka nje
SACCOS hii ikifanikiwa kuzalisha mtaji mzuri inaanzisha JF Members Community Bank ambapo kadri inavyozidi kufanya vizuri na kuwa na mtaji mzuri inakuwa JF Members Commercial Bank, ambapo hapa ndio mwisho wa matatizo.
Kila kitu huanza na moja. Akitokea mwanaJF mmoja then wawili then watatu, nk waka take serious commitment with very high drive baada ya miaka kadhaa inazaliwa JF Members Commercial Bank - JMC Bank yenye mafanikio makubwa sana.
Hesabu inakuwa hivi:
JF kwa sasa ina members zaidi ya 479,000 assume actual members ni 400,000 pekee.
Wakaamua kuchanga kila JF member:
Members 400,000 x sh. 1,000/- = Sh. 400,000,000/-
Au
Members 400,000 x Sh. 2,000/- = Sh. 800,000,000/-
Au
Members 400,000 x sh 3,000/- = sh. 1,200,000,000/-
Au
Members 400,000 x sh. 4,000/- = Sh. 1,600,000,000/- (Huu ni mtaji wa Community Bank)
Au
Members 400,000 x sh 5,000/- kila member = Sh. 2,000,000,000/- (Sh. Bilioni Mbili - Huu ni mtaji wa Community Bank).
Hao Members wanaweza kuzidi kwa sababu kuna watu pia ni guests wakiona idea inasimamiwa vema, nao watapenda kuwa members rasmi.
Kwa nini ni rahisi zaidi hii SACCOS kufanikiwa?
> Ni rahisi kwa sababu humu kuna kila aina ya watalaam, wabobezi na wazoefu wa kila aina ya biashara na kila aina ya kilimo kiasi kwamba ni ngumu sana kufanya jambo la kubahatisha. La muhimu ni kutengeneza miundo mbinu mizuri namna ya kunufaika nao na itakuwa rahisi mno kufanikiwa kwa haraka sana.
Mfano kama tukiamua kufanya biashara ya mchele, humu kuna members ambao wana supply mchele hivyo watarahisisha biashara kwa ku supply SACCOS yetu mchele mzuri, hivyo mambo yatakuwa mepesi zaidi.
Kwa maneno mengine kila biashara tutakayofanya kuna 'mentorship' ya kutosha kwa hio hatufanyi lolote kwa kubahatisha. JF platform tunatumia kupeane updates za mara kwa mara kwa business za SACCOS.
> Members pia ndio wateja wa kwanza wa kile SACCOS yao inachozalisha. Hii pia ni boost kubwa sana kibiashara kwa sababu biashara inaanzishwa na tayari customer base ipo tayari ikisubiri huduma tu!
Fikiria kwa mfano mdogo tu:
SACCOS inauza mchele kwa bei ya rejareja let say kilo moja sh 2,000/- sawa na bei ya soko.
Kila member popote alipo akanunua kilo 1 tu. Hivyo inakuwa Kilo 1 x sh. 2,000/- = sh. 2,000/- kwa kila member.
Members wapo 400,000/- x sh. 2,000/- = Sh. 800,000,000/-.
Kwa mwaka kila JF Member akanunua kilo 3 tu, sawa na kilo 3 x sh. 2,000/- = Sh. 6,000/-.
Members 400,000 x sh. 6,000/- = Sh. 2,400,000,000/- yaani sawa na sh. bilioni mbili na milioni mia nne. Tayari tuna mtaji wa kutosha kuanzisha JF Members Community Bank (gharama zitakuwa calculated). Tukipiga round kadhaa hivi tunabadili jina na kuanzisha JF Members Commercial Bank.
Hii Bank sasa inakuwa kama bahari kila member aogelee kwa kadri awezavyo kwa sheria za bank ila yeye kama founder na owner wa bank!
Hizo biashara za SACCOS zinaendeshwaje?
Zinaendeshwa sawa tu na branches mbalimbali zinavyoendeshwa mfano branches za bank.
Mfano:
Kunakuwa na JF Members SACCOS HQ, halafu
JF Members SACCOS - Dsm Wing
JF Members SACCOS - Arusha Wing
JF Members SACCOS - Dodoma Wing
Kila Wing inakuwa na uongozi, let say title yake ni Wing Director / Manager ambaye moja kwa moja atawajibika kwa JF Members SACCOS HQ.
Kutakuwa pia na kitengo kikuu cha 'Compliance and Auditing' ambacho kinatazama mwenendo mzima wa SACCOS kuanzia A to Z.
Kila siku, kila Wing kinafanya tadhmini ya business na kutuma report HQ bila kumis. Kitatuma business report na mambo mengine yanayohusiana na Wing yao.
Kila wiki bila kukosa, SACCOS HQ kinatoa kwa members wake a compiled report ya operations za Wings zake zote.
Naendelea hapo chini:
Members wananufaikaje?
Kuna members 400,000.
Ndani ya hawa members 400,000 tukatengeneza groups 400 kila group likiwa na members 1,000.
Jukumu la SACCOS likawa ni kuhakikisha inapiga kazi masaa 24 (wateja wapo so ni kuhakikisha tu quality za business na logistics zote zinaenda sawa as zilivyopangwa, so muhimu ni usimamizi tu) ili kila group ipate sh 20,000,000/-
Sawa na kutafuta jumla sh. 20,000,000/- x 400 groups = sh. 8,000,000,000/- (bilioni nane).
Sh. 20,000,000/- za kila group nao wanaumiza akili wafanye biashara gani ambayo itawaingizia kipato (Tunaweza kuweka sheria kuwa kikundi kilicho ndani ya SACCOS kisianzishe biashara ambayo SACCOS inafanya ili kuepusha conflicts of interest).
Hizi pesa zinasimama kama mkopo kwa kikundi hiki, ila hauna riba. Mkopo huu utarejeshwa ndani ya muda tutakaokubaliana.
Baada ya kurejeshwa hizo pesa, tunahakikisha kila kikundi tunagawa tena katikati, na kuzaliwa kikundi kingine
Yaani kwa sasa kunakuwa na vikundi 800 kila kikundi kikiwa na wanachama 500.
Kila kikundi kinaachiwa sh. 20,000,000. Utaratibu ni ule ule wa mkopo bila riba, nao utarejeshwa kwa muda maalum utakaopangwa.
Baada ya mkopo kurejeshwa kila kikundi kinagawanywa tena, hapa sasa tuna vikundi 1,600 kila kikundi kina watu 250. Kila kikundi kinaachiwa sh. 20,000,000/- kwa utaratibu ule ule mkopo bila riba na utarejeshwa kwa muda maalum.
Baada ya mkopo kurejeshwa kikundi kinagawanywa tena, na sasa kuna vikundi 3,200 kila kikundi ina wanachama 125. Utaratibu ule ule wa mkopo wa sh 20,000,000/- unaendelea.
Maximum vikundi vya JF nchi nzima ni 5,000 kila kikundi kikiwa na wanachama 80 hadi 100 tu.
Kazi kuu ya SACCOS ama JF Members Commercial Bank ni kuhakikisha ustawi wa vikundi vyake alias wanakikundi. Ustawi wa hivi vikundi ndio ustawi kamilifu wa JF Members SACCOS ama JF Members Commercial Bank.
Faida itokanayo na JF Members Commercial Bank - JMC Bank inaenda moja kwa moja kwenye vikundi ambapo ndipo wanachama na wenye benki wanapoishi.
Namna ya kufanikisha hili:
Commitment + Inner Drive.
Naombeni mnipinge!
NB:
Kama kuna mtu anadhani anaweza ku push hiki kitu iwe jua iwe mvua anicheki pm (Its only for JF Members). Kila dream iliyotimia sasa ilianza hivi hivi.
Then, tutafunga safari hadi ofisi za JF, tutaomba ID verification halafu tunaendelea na safari yetu ya JF Members SACCOS LTD to JF Members Commercial Bank.
Slogan yetu ya kututia nguvu itakuwa hii: We never negotiate with poverty.
Tukimaanisha kwamba sasa tupo tayari kufanya lolote kuondoa umaskini Tanzania. Sasa muda wa kujadiliana na umaskini umekwisha. Hatujadiliani na umaskini tena.
Jamani Elli wajua nakumiss miss...
Mliishia wapi?Jamani Elli wajua nakumiss miss...
Happy New Year too my dear...
Halafu tutafutane buana
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mie nimestack sijui tuko wapi na tumeishia wapi tehMliishia wapi?
[emoji849][emoji849][emoji849]
Bado tuko kwenye right track mama... Tunaendelea kulisongesha[emoji849][emoji849][emoji849]
Sio na eli bwana, kale kampango kenu kama haka.
Hahaha Ontario nomaWazo zuri sana hili tatizo kuna kina ONTARIO watajifanya wajanja wa kutaka kuwapiga wengine
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaaaaa....Jamaaani umenichekeshaaa..!!
Aisee hii hatari mnosio kwamba kuna member laki ine ila kuna id laki ine
20 zinaweza kuwa za mtu mmoja