Zabron Hamis
JF-Expert Member
- Dec 19, 2016
- 7,093
- 11,377
Nimetulia mbele ya kioo cha TV nikasema leo nisikilize nyimbo za injili ili kuiandaa ibada ya jumapili. Kama mnavyojua walevi na wapenda starehe huanza kujiandaa siku ya ijumaa hivyo nami nikasema sio vibaya nikafanya kwa upande wangu. Sina tatizo na ulevi ama starehe ya mtu, ni mfano tu nimetumia.
Nimesikiliza nyimbo nyingi hatimaye nikafika katika wimbo uitwao El Shaddai kutoka kwa vijana wa Kenya waitwao Hart the Band. Huu wimbo nimekuwa nikusikiliza tangia umetoka lakini leo nikasema nitazame video yake[emoji2296][emoji2296][emoji2296][emoji2296] maudhui ya audio yanaeleweka, lakini video yake kusema kweli haina funzo kwa wakristo na badala yake wameonesha jinsi ufuska (kudanga) kwamba Mungu anaweza kutumia kama mbadala wa kumpatia mtu mahitaji.
Katika kipande kimoja anaonekana mwanamke amelala na mwanaume na baada ya hapo akalipwa pesa ikiwa na maana kwamba amehongwa kwa kujiuza. Na kesho yake ada ya mwanae ikalipwa. Upande mwingine anaonekana mzee anahubiri kwenye matatu lakini sadaka haipatikani na matokeo yake anafika kwenye nyumba aliyopanga, anakuta kufuli. Anaishia kupiga magoti na kulia. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba, mmoja kati ya waimbaji ambao wote ni wakiume, ameweka kipini puani jambo ambalo linatia ukakasi hasa kijana wa kiume kujiremba kuliko dada zake na wakati huohuo biblia imeonya mahali pengi kutofuatisha namna ya dunia.
Huo ni mfano mmoja kati ya mingi jinsi wafuasi wanaojiona ama kujiita wanampenda Mungu kuwa na vitendo viovu kuliko hata wale wasiosali katika nyumba za ibada. Leo hii ni rahisi kukuta migogoro katika nyumba za ibada kuliko kwenye vicoba. Watu waovu wamejazana makanisani kiasi kwamba hata wale wenye nia njema kuogopa kushirikiana nao. Si ajabu kukuta binti muimba kwaya akiwa amevaa suruali ya kubana ama sketi fupi kuliko hata chupi aliyovaa.
Yupo pia msanii anayesemakana kuwa ni kijana wa Rose Muhando, huyu naye si haba. Kuanzia sauti mpaka aina ya uchezaji wake ni wa kike kike japo ni kijana wa kiume. Kuna wimbo wachezaji (stage shower/dancers) wa kike wamebana makalio na visuruali nikashangaa. Pengine ni ushamba unanisumbua lakini ndugu zetu Waislam wako makini sana kutokopi na kupaste ya ulimwengu kuyapeleka kwenye nyumba za ibada.
Mungu atusaidie sana.