Siku hizi mashemeji hawaaminiki tena

Siku hizi mashemeji hawaaminiki tena

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
✍️Mhadhara (79).
Kama ulikuwa hujui nakuibia hii siri, sikuhizi mashemeji wanatafunana sana. Wanaitana "shemeji" mbele yako, lakini hilo sio jina lao pindi wakikutana wawili.

Utafiti wa uongo uliofanywa hivi karibuni na Mr. Right Marker umegundua sababu mbalimbali za mashemeji wengi mjini kutafunana. Baadhi ya sababu hizo ni;

1. Kukosa usiri wa chumbani au mahusiano:
Utafiti huu wa uongo umegundua kuwa ukosefu wa usiri katika mahusiano unaweza kumvuta "shemeji mtu" kwenye mahusiano yako. Kwa mfano mipango ya kifedha, maendeleo, ununuzi wa zawadi, raha za mapenzi, n.k; ambayo unafanya na mwenza wako yakimpata "shemeji mtu" yanaweza kumpa wivu wa maisha hatimaye na yeye kujisogeza.

2. Ushauri wa mahusiano na ndoa:
Utafiti wa uongo umegundua kuwa rafiki yako au ndugu yako ambaye mara kwa mara anapenda sana kushauriwa na mwenza wako, au kutoa ushauri kwa mwenza wako kuhusu masuala ya mahusiano na ndoa. Hiyo tabia inaweza kumvuta "shemeji mtu" kwenye uhusiano wako.

3. Kuishi pamoja na rafiki au ndugu ambaye amefikia umri wa kujitegemea:
Kuna wale wanaochukua marafiki au ndugu ambao wamefikia umri wa kujitegemea kisha kuishi nao pamoja. Utafiti wa uongo umegundua kuwa mtu unayeishi nae ndani kwako ambaye amefikia umri wa kujitegemea lakini hapendi kujishughulisha anakuwa na muda mwingi wa kuyajua na kuyathamini mapenzi kwasababu hana kazi ya kufanya. Hivyo muda wowote kinaweza kuumana na mwenza wako ambaye ana upweke dhidi ya ubusy wako.

4. Lifti za usafiri kati ya mwenza wako na marafiki zako (mashemeji zake):
Kama mwenzi wako kila akienda kazini ni lazima aombe lifti au ampe lifti rafiki yako, sio wote wanaweza kujisogeza kwa mwenzi wako lakini ni sababu kubwa ya "shemeji mtu" kuwa mume mwenza wako au mke mwenza wako.

5. Kusifu mara kwa mara mambo au vitendo vya mwenza wako - au vya rafiki yako:
Utafiti wa uongo umegundua kuwa mwenza wako anaweza kushikwa na tamaa au hamu ya kutaka kupata, kuona, kugundua, au kujua vitu vya rafiki yako au mpenzi wako ambavyo unavisifia kila mara.

RIGHT MARKER
Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom