Siku hizi mashetani na wachawi ndiyo wanaohubiri injili. Injili yao ni kavu haina mvuto

Siku hizi mashetani na wachawi ndiyo wanaohubiri injili. Injili yao ni kavu haina mvuto

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Zamani ukienda sehemu za injili ya Kristo iletayo wokovu ilipokuwa inahubiriwa palikuwa na mvuto na upako kiasi kwamba ulikuwa unataka uendelee kusikiliza.

Shida ilikuwa ni pale walipokuwa wanaita wale waliotayari kuokoka waje mbele ndo vita inaanza ya kukuzuia. Wale waliokuwa wanaishinda ndo walikuwa wanatoka mbele na mtu aliyekuwa anaokoka kwa njia hiyo alikuwa ni mlokole kwelikweli.

Sasa siku hizi ukiwaangalia hao wahubiri kwa mizania ya neno la Mungu unaona chenga tu ni tiamajitiamaji hatakama hiyo huduma itakuja na nguvu za kifedha. Neno la Mungu linalohubiriwa kwanza halina upako wala mvuto wa kumfanya mtu aache shughuri zake kusikiliza.

Kwenye makanisa watu ambao ni vimbelembele kujifanya watumishi kwenye kwaya, uzee wa kanisa, kuhudumia madhabau ukiwaangalia wamepagawa na mapepo ya mizimu ya kwao! Ofcourse huwezi kuwafanyakitu kwasababu wana mdomo na kujihesabia haki sio kawaida.

Hila kwa upande mwingine wanazuia na kusababisha sana watu wakimbie makanisa na mikusanyiko ya neno la Mungu! Kwenye magroup ya WhatsApp ya kiroho wanajifanya kuposti "aya" za Biblia wakati ni mashetani kabisa!
 
Zamani ukienda sehemu za injili ya Kristo iletayo wokovu ilipokuwa inahubiriwa palikuwa na mvuto na upako kiasi kwamba ulikuwa unataka uendelee kusikiliza! Shida ilikuwa ni pale walipokuwa wanaita wale waliotayari kuokoka waje mbele ndo vita inaanza ya kukuzuia. Wale waliokuwa wanaishinda ndo walikuwa wanatoka mbele na mtu aliyekuwa anaokoka kwa njia hiyo alikuwa ni mlokole kwelikweli! Sasa siku hizi ukiwaangalia hao wahubiri kwa mizania ya neno la Mungu unaona chenga tu ni tiamajitiamaji hatakama hiyo huduma itakuja na nguvu za kifedha. Neno la Mungu linalohubiriwa kwanza halina upako wala mvuto wa kumfanya mtu aache shughuri zake kusikiliza! Kwenye makanisa watu ambao ni vimbelembele kujifanya watumishi kwenye kwaya, uzee wa kanisa, kuhudumia madhabau ukiwaangalia wamepagawa na mapepo ya mizumu ya kwao! Ofcourse huwezi kuwafanyakitu kwasababu wana mdomo na kujihesabia haki sio kawaida! Hila kwa upande mwingine wanazuia na kusababisha sana watu wakimbie makanisa na mikusanyiko ya neno la Mungu! Kwenye magroup ya WhatsApp ya kiroho wanajifanya kuposti "aya" za Biblia wakati ni mashetani kabisa!
Yaani unasali kaniaa mwezi mzima hujasikia neno Msamaha, Toba wala Kitubio.
 
Nenda makanisa ya Kilutheri angalia safu ya watu vimbelembele kujifanya wa kiroho wengi ni nyumba za mizimu ya koo na familia zao
 
Muziki uchezwa kulingana na mdundo wake.
Watu wenyewe wa kuhubiria injili ya mvuto wapo wapi?
 
Yaani hata hamu ya kwenda makanisani imeisha! Wengi wanaowaweka kuwa mbele katika huduma unakuta wamepigwa na mizimu stroke, wengine vilema wa mikono na miguu! Hatusemi vilema na viwete hawatakiwi kumtumikia Mungu, lakini maandiko katika agano la kale ukitaka kupeleka sadaka ya mnyama sharti ikaguliwe na makuhani. Hiyo sadaka ikionekana ina ulemavu wa aina yoyote hata kiungo ilikuwa inakataliwa. Sasa fanya utafiti kanisani kwako watu waliombelembele kujifanya ndo wenyewe kumsaidia/kumuwakilisha mchungaji ni wa tu wa aina gani?
 
Safari ya mbinguni ni ya mtu mmoja, siyo ya kundi fulani, jikague wewe mwenyewe, mahusiano ni ya mtu na Mungu sio watu na Mungu, Jitafute na ujikague wewe mahusiano yako na Mungu yakoje, usiangalie fulani kafanyaje au kawaje maana kanisani kila mtu anaenda kwa malengo yake na mahitaji yake

Kuna mwingine anaenda na hitaji la kuolewa huyo ataenda kwa namna yake, mwingine anahitaji kukutana na Mungu wake ataenda kwa namna alivyojiandaa kutoka nyumbani kwake
 
Zamani ukienda sehemu za injili ya Kristo iletayo wokovu ilipokuwa inahubiriwa palikuwa na mvuto na upako kiasi kwamba ulikuwa unataka uendelee kusikiliza.

Shida ilikuwa ni pale walipokuwa wanaita wale waliotayari kuokoka waje mbele ndo vita inaanza ya kukuzuia. Wale waliokuwa wanaishinda ndo walikuwa wanatoka mbele na mtu aliyekuwa anaokoka kwa njia hiyo alikuwa ni mlokole kwelikweli.

Sasa siku hizi ukiwaangalia hao wahubiri kwa mizania ya neno la Mungu unaona chenga tu ni tiamajitiamaji hatakama hiyo huduma itakuja na nguvu za kifedha. Neno la Mungu linalohubiriwa kwanza halina upako wala mvuto wa kumfanya mtu aache shughuri zake kusikiliza.

Kwenye makanisa watu ambao ni vimbelembele kujifanya watumishi kwenye kwaya, uzee wa kanisa, kuhudumia madhabau ukiwaangalia wamepagawa na mapepo ya mizimu ya kwao! Ofcourse huwezi kuwafanyakitu kwasababu wana mdomo na kujihesabia haki sio kawaida.

Hila kwa upande mwingine wanazuia na kusababisha sana watu wakimbie makanisa na mikusanyiko ya neno la Mungu! Kwenye magroup ya WhatsApp ya kiroho wanajifanya kuposti "aya" za Biblia wakati ni mashetani kabisa!
Injili imeingiliwa na majambazi tuwe makini sana.
 
Safari ya mbinguni ni ya mtu mmoja, siyo ya kundi fulani, jikague wewe mwenyewe, mahusiano ni ya mtu na Mungu sio watu na Mungu, Jitafute na ujikague wewe mahusiano yako na Mungu yakoje, usiangalie fulani kafanyaje au kawaje maana kanisani kila mtu anaenda kwa malengo yake na mahitaji yake

Kuna mwingine anaenda na hitaji la kuolewa huyo ataenda kwa namna yake, mwingine anahitaji kukutana na Mungu wake ataenda kwa namna alivyojiandaa kutoka nyumbani kwake
Kumbuka hiyo ni madhabahu! Shetani anaweza kuweka kiti chake cha enzi kwenye madhabahu ya kanisani ndivyo maandiko yanavyosema(ufu 2:13)
 
Wanaojiita wakristo wamekuwa hovyo sana miaka hii. Karibu makanisa yote yana watu wa ovyo sana. Ujuaji mwingi kujifanya yupo kidijitali anafungua bible yake kwenye simu, hakuna unyenyekevu wa ibada, kupenda pesa ndio usiseme..kuanzia viongozi mpaka waumini wa mwisho, makanisani show offs ni nyingi, ubaguzi kwa walionavyo na akina sie uko wazi kabisa.. ki ufupi makanisa yamekumbwa na miroho gani sijui! Nyimbo zinazotungwa ni za kuimba wuuuh wuuuh wuuh kuanzia RC hadi makanisa ya Kipentekoste.. upako hakuna.
 
wewe ni mkristo?
 
Kumbuka hiyo ni madhabahu! Shetani anaweza kuweka kiti chake cha enzi kwenye madhabahu ya kanisani ndivyo maandiko yanavyosema(ufu 2:13)
Ufunuo wa Yohana 2:13-17
[13]Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

[14]Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

[15]Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.

[16]Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

[17]Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

Nadhani utakuwa umeelewa mkuu
 
Back
Top Bottom