Vijana mnaobahatika kusoma hapa jifunzeni, tupo zama za unafiki, watu wanajua njia ila hawakuoneshi sasa kwakuwa unajiongoza uwe na hekima ujifunze kutokana na uzoefu wa mapito yako. Watu wazima wanakuwa wanaona unaelekea shimoni ila hawakwambii wanakuacha upotee wakucheke waseme tulijua. Hakuna wa kukunasua, maisha haya hata ndugu hawana huruma na wewe. Ilifikia kipindi wakikutana demu mgumu wananipasia namba nimle maana nilikuwa sitongozi mara mbili, wanajua kwa mwendo huo sitoboi ila wakawa wananisifia tu nipotee zaidi, kuwa makini sana ukiona unatenda uovu kisha unasifiwa na kupongezwa ujue anguko lako li karibu na ni furaha kwao, usianguke badili gia angani uwashangaze kwa kuwa mtu mkamilifu mwenye maadili yake. Have some manners