Siku hizi za karibuni henzerani imerudi tena kuadhibu watu wanaotuhumiwa kwa makosa

Siku hizi za karibuni henzerani imerudi tena kuadhibu watu wanaotuhumiwa kwa makosa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Niko Zanzibar kiasi cha miaka miwili mitatu hivi na ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hoteli niliyopanga iko karibu sana na pwani.

Inakaribia Maghrib wakati wa adhana na kufungua.

Nikaona itapendeza kwangu kutoka nje nikasimama pwani na kuangalia wavuvi wanarudi kutoka baharini na nikaisikiliza adhana kutoka msikiti wa jirani.

Nimesimama pwani akanijia kijana mdogo labda miaka 25 hivi akanitolea salamu nikaitika.

Huyu kijana akaniuliza kama mimi ni Mohamed Said.

Akaniambia kuwa ananisoma sana na anapendezwa na niandikayo.

''Kuna kisa nimepata kukusikia ukikieleza kuhusu bwana mmoja ambae baada ya mapinduzi alichapwa viboko hadharani Pemba kiasi alipomalizwa kupigwa hakuweza hata kusimama ikabidi abebebwe kurudishwa kwake.''

Nikamjibu kuwa nimepata kueleza kisa hicho.

''Hukutaja jina la huyu mzee aliyepigwa wala yule aliyemuadhibu.''

Nikamjibu ni kweli sikumataja na nilifanya vile kwa makusudi.

"Huyu mzee aliyepigwa viboko ni babu yangu na aliyempiga ni fulani."

Akanitajia jina la babu yake.

''Babu yangu kwa fedheha ile aliyotiwa hakutoka ndani hadi siku alipotiwa ndani ya jeneza kwenda kuzikwa.''

Nimezoea kusikia mikasa kama hii katiika historia ya Zanzibar lakini hii ni mara yangu ya kwanza kuhadithiwa na kijana mdogo.

Nilimwangalia na kwa hakika tuliangaliana macho kwa macho.

Niliiona ile hamaki na ghadhabu iliyokuwa ndani ya moyo wake katika sura yake.

Niliinamisha uso wangu chini kukwepa kuuangalia uso wa huyu kijana.

Tukaagana lakini aliniacha na fikra nyingi.

Siku hizi za karibuni henzerani imerudi tena kuadhibu watu wanaotuhumiwa kwa makosa.

Historia hujirudia.
 
Mohamed Said,

..naomba kuuliza, Henzerani maana yake ni nini, ni jina la mtu?

..yanayoendelea yanafikirisha sana. sijui mwisho wake ni nini.

..je, watawala wataishia kuchapa viboko tu, au wataongeza na adhabu nyingine za namna hiyo?
 
Mohamed Said,

..naomba kuuliza, Henzerani maana yake ni nini, ni jina la mtu?

..yanayoendelea yanafikirisha sana. sijui mwisho wake ni nini.

..je, watawala wataishia kuchapa viboko tu, au wataongeza na adhabu nyingine za namna hiyo?
JK,
Henzerani ni kiboko.
 
Mi nafikiri badala ya kulalamika tuanze kuhamasishana watu wasikubali kuchapwa viboko maana hawa watu tunawaendekeza sana ziwe ama zao ama zetu adabu itarudi
Rod...
Unaweza kusababisha madhara makubwa.
Taratibu za kisheria zinafaa zaidi.
 
Rod...
Unaweza kusababisha madhara makubwa.
Taratibu za kisheria zinafaa zaidi.
Kama mahakama zipo, polisi wapo watu wanaolipwa kwa kodi zetu wanaamua kujichukulia hatua na wala hatusikii wakikemewa nini maana yake.
Maana yake tuna wakolono weusi wote tunajua tabia hujenga mazoea sasa hivi kuna watu wanajiona wao ndio wenye nchi na wengine hamna kitu, kwa dunia ya sasa kama kijiji kila kinachofahamika pamojq nq mapungufu ya kiuchumi na tofauti zetu sasa hivi tunajenga nchi ambayo haina amani
 
Rod...
Unaweza kusababisha madhara makubwa.
Taratibu za kisheria zinafaa zaidi.

Mohamed Said,

..mimi niko radhi kuchapwa viboko, hata kama ni kwa uonevu, kuliko kuonewa na mahakimu wa zama hizi.

..kuliko kuwekwa mahabusu, halafu nisumbuliwe miaka mitatu mahakamani, niingie gharama za kuweka wakili, halafu nifungwe kishenzi na hakimu wa ccm, ni afadhali nichapwe viboko niendelee na maisha yangu.

..tena baada ya kufungwa kishenzi na hakimu wa ccm, unapofikishwa gerezani lazima uonyolewe nywele, na uvuliwe nguo na vijana wadogo askari magereza wa ccm.

..Think about it. Henzerani kurudi inaweza kuwa a blessing in disguise.
 
Kama mahakama zipo, polisi wapo watu wanaolipwa kwa kodi zetu wanaamua kujichukulia hatua na wala hatusikii wakikemewa nini maana yake.
Maana yake tuna wakolono weusi wote tunajua tabia hujenga mazoea sasa hivi kuna watu wanajiona wao ndio wenye nchi na wengine hamna kitu, kwa dunia ya sasa kama kijiji kila kinachofahamika pamojq nq mapungufu ya kiuchumi na tofauti zetu sasa hivi tunajenga nchi ambayo haina amani
Nimesoma hii thread nikacheka kweli kweli. Siyo kama nafurahia watu kudhalilishwa kwa viboko lakini ni jinsi mwenye thread alivyowasilisha mada yake. Ni kweli imerudi henzarani imerudi lakini acha irudi kwani watanzania wamezidi ukondoo.
 
Serikali yetu inatumia nguvu kubwa kuvutia wawekezaji lakini hawajui mwekezaji anaangalia nini kabla ya kuja kuwekeza kwenye nchi husika, kitu cha kwanza anaangalia utawala nqa namna nchi inavyoendeshwa.
Wawekezaji makini hawawezi kuja kuwekeza kwenye nchi ambayo hawazingatii utawala bora ambayo kiongozi ndiye mwendesha mashitaka na hapohapo ni hakimu.
Kiongozi hawezi kuwekeza kwenye nchi ambayo masuala ya kodi badala ya kujadiliwa tra mkuu wa wilaya anamwita nq kumsweka ndani kwa aina ya utawala huu wawekezaji badala ya kuja watazidi kukimbia
 
Kwa Africa inakuja phase ya pili ya kudai Uhuru, kipindi hiki kinaweza kuwa kigumu na kibaya kuliko kile cha kudai Uhuru kitoka kwa mtu mweupe. Ila jiandaeni, kinakuja.
 
Nadhani hata yale makofi tukiyajua kama (kelbu )kisha unasindikizwa na maneno blaliful (bloodfool)pia ingekuwa vizuri yakarudi maana waqt ule yalikuwa pamoja kama chanda na pete.
 
With Ref.
.DC Arusha
.Naibu Waziri
Nakwambia kama Tanzania wangekuwa wanaishi binadamu hai wanaojitambua na siyo hawa wanaosikiliza muziki wa mondi kutwa nzima na kusikiliza vipindi vya kuchambana kupitia fm radios . Nchi ingewaka moto na wale wachapa viboko wangeshafungwa sanyingi.
Ni rahisi KUTAWALa Tanzania kuliko wilaya moja huko Tarime
 
Back
Top Bottom