Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Niko Zanzibar kiasi cha miaka miwili mitatu hivi na ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hoteli niliyopanga iko karibu sana na pwani.
Inakaribia Maghrib wakati wa adhana na kufungua.
Nikaona itapendeza kwangu kutoka nje nikasimama pwani na kuangalia wavuvi wanarudi kutoka baharini na nikaisikiliza adhana kutoka msikiti wa jirani.
Nimesimama pwani akanijia kijana mdogo labda miaka 25 hivi akanitolea salamu nikaitika.
Huyu kijana akaniuliza kama mimi ni Mohamed Said.
Akaniambia kuwa ananisoma sana na anapendezwa na niandikayo.
''Kuna kisa nimepata kukusikia ukikieleza kuhusu bwana mmoja ambae baada ya mapinduzi alichapwa viboko hadharani Pemba kiasi alipomalizwa kupigwa hakuweza hata kusimama ikabidi abebebwe kurudishwa kwake.''
Nikamjibu kuwa nimepata kueleza kisa hicho.
''Hukutaja jina la huyu mzee aliyepigwa wala yule aliyemuadhibu.''
Nikamjibu ni kweli sikumataja na nilifanya vile kwa makusudi.
"Huyu mzee aliyepigwa viboko ni babu yangu na aliyempiga ni fulani."
Akanitajia jina la babu yake.
''Babu yangu kwa fedheha ile aliyotiwa hakutoka ndani hadi siku alipotiwa ndani ya jeneza kwenda kuzikwa.''
Nimezoea kusikia mikasa kama hii katiika historia ya Zanzibar lakini hii ni mara yangu ya kwanza kuhadithiwa na kijana mdogo.
Nilimwangalia na kwa hakika tuliangaliana macho kwa macho.
Niliiona ile hamaki na ghadhabu iliyokuwa ndani ya moyo wake katika sura yake.
Niliinamisha uso wangu chini kukwepa kuuangalia uso wa huyu kijana.
Tukaagana lakini aliniacha na fikra nyingi.
Siku hizi za karibuni henzerani imerudi tena kuadhibu watu wanaotuhumiwa kwa makosa.
Historia hujirudia.