Siku ilipozama MV Bukoba

Shagiguku

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
409
Reaction score
138
Tarehe na mwezi kama wa leo (21. May. 1996) Tukiwa kama familia, tulikuwa tukivuna mpunga katika majaruba yaliyopo maeneo ya airport mwanza.

Ghafla kupitia kijiradio kidogo cha mkononi (philips) tulichokuwa nacho hapo tukasikia matangazo ya radio moja (radio one) yanakatizwa na mtangazaji kuanza kutoa taarifa ya kusikitisha na kuhuzunisha.

Ni ajari, ajari kubwa ya majini ilikuwa imetokea alfajili hiyo kilometa zipatazo 56 kutoka bandari ya mwanza mjini.

Meli kubwa ya mv bukoba iliyoundwa mwaka 1979 na iliyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilikuwa imezama umbali wa mita zipatazo 25 kutoka ufukoni mwa maji na zaidi ya watu watanzania 1,000 walikuwa wamepoteza maisha baada ya KUTOBOLEWA kwa meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17 tu.

Leo tarehe 21. 05. 2013 watanzania "tunasherehekea" miaka mingine 17 tangu kuzama kwa meli hiyo. Tarehe kama ya leo mwaka 1996 mji wa mwanza uligubikwa na simanzi ya kutisha, uwana uliozoeleka kwa shughuli za michezo wa nyamagana ukageuzwa kwa muda kuwa uwanja wa kupokelea miili ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo.

Nakumbuka siku hiyo hata zoezi letu la kuvuna mpunga liliishia hapo, na sisi kurudi nyumbani na kuelekea uwanja wa nyamagana kwaajili ya zoezi la kutambua miili ya watu waliofariki.

Baadhi ya maswali ya kujiuliza kwa watanzania wote leo, tunapo "sherehekea" ajari hiyo ni haya hapa:

1: Je, tulijifunza jambo lolote kutokana na ajari hiyo?

2: Kama kuna jambo tulijifunza, je tumefanikiwa kulifanyia kzai ipasavyo jambo hilo?

3: Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu leo??

4: je, tumekwishajijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu leo??

5: Je, taarifa/ripoti ya uchunguzi wa ajari hiyo ilifanyiwa kazi ipasavyo??

6: je, ni ajari ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo?? na kwa nini kama kuna jambo tulijifunza viendelee kuzama vyombo vingine majini??


Naamini wananzengo wengine mtakuja hapa na maswali mengine mengi tu, ambayo pia yanakaribishwa. Haya tupia swali ulilonalo kuhusu hii kadhia ya kuzama kwa vyombo vya usafiri majini.


View attachment 94600
 
Wengine tulikuwa wadogo sana hebu tueleze sababu ya kutobolewa kwa hiyo meli
 
Ni moja za ajali mbaya za meli lkn imekuja kufunikwa na islander spice ambayo iliua takriban watu buku 3.
 

Tunasherehekea!!!! labda hujamaanisha hili neno.
 
chanzo cha kutobolewa kwa meli ilikuwa ni mawasiliano yaliyokuwa yakifanywa na abiria ndani ya meli (wahindi) na wenzao nchi kavu wakiwataka wafanye kila wawezalo kuwaokoa na hapo likawa limetangazwa dau nono. hivo basi wakaitwa mafundi wedini na gesi zao na kuanza kuitoboa meli.

Kile kitendo tu cha kuitoboa kikasababisha hewa kuingia ndani na hatimaye meli kuzama yote huku wakiibuliwa watu wawili (wa bongo) tu kutoka katika hilo tundu lililotobolewa.
 
Tunasherehekea!!!! labda hujamaanisha hili neno.


Na ndo maana lipo katika funga na fungua semi, waandishi wa habari wanafahamu maana yake.

Lakini pia kama waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia sheria katika nchi hii watakuwa bado hawajaweza kutusaidia watanzania kujibu hayo maswali hadi leo, basi hilo neno "tunasherehekea" litakuwa na maana kubwa kama lilivo na si vinginevo, kwa maana kwamba kama ajari za majini bado zinaendelea kutokea hadi leo kwa uzembe wa watu waliopewa dhamana juu ya kusimamia sheria hizo, na kwamba tangu kuzama kwa meli ya mv bukoba hadi leo hakuna mabadiliko, tukibaki kuambiwa sababu zile zile na watu wale wale basi tutakuwa "tunasherehekea" ajari hiyo, lakini pia tunaendelea "kusherehekea" matukio mengine yanayofanana na hilo.
 
Wengine tulikuwa wadogo sana hebu tueleze sababu ya kutobolewa kwa hiyo meli

kumbe na wewe ni wa yale matokeo yaliyofutwaa?hope akili yako imeshakomaa tayari coz watoto wa siku hizi viherehere kweli.
 
Nakumbuka nilikuwa mkubwa kiasi, nakaribia kumaliza form four huko mbeya, wakati ule nakumbuka tulishawishiwa kuamini utawala mpya ulikuwa unafanya kafara ili wafanikiwe katika utawala hasa baada ya kuteswa sana na A.Mrema mwaka 1995, leo siwezi kuamini ujinga ule lakini ulinifanya niendelee kuiona ajali ya mv bukoba kama moja kati ya mambo mabaya sana kuwahi kutokea hapa tanzania, poleni wote mlioathiriwa kwa ukaribu na tukio hilo la kuzama kwa mv bukoba
 
Hizi ajali za kupangwa na wachawi mlio waweka madalakani. Hamtaendelea milele kwa kukumbatia uchawi
 
Ni moja za ajali mbaya za meli lkn imekuja kufunikwa na islander spice ambayo iliua takriban watu buku 3.

Kitu kama ilishika world record kwa ajali ambazo zimewahi kutokea ziwani (yaani ukiondoa zile za baharini)
 
Wengine tulikuwa wadogo sana hebu tueleze sababu ya kutobolewa kwa hiyo meli
sababu ya siasa kusimamia kila kitu baada ya mawasiliano ya wahindi, jerumani mmoja (genji) alishauri kabla ya kuitoboa meli ivutwe kuelekea nchi kavu hadi iguse chini,lakini watawala wakaona itachukua muda mrefu na wapendwa wao wanaweza poteza maisha vilevile waliona kwa kuivuta meli maiti zita sambaa ziwani bila,kuzingatia principle za archimedis meli ilitobolewa na air pocket iliyokuwa inasababisha meli kuelea ikaescape chombo kikazama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…