Shagiguku
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 409
- 138
Tarehe na mwezi kama wa leo (21. May. 1996) Tukiwa kama familia, tulikuwa tukivuna mpunga katika majaruba yaliyopo maeneo ya airport mwanza.
Ghafla kupitia kijiradio kidogo cha mkononi (philips) tulichokuwa nacho hapo tukasikia matangazo ya radio moja (radio one) yanakatizwa na mtangazaji kuanza kutoa taarifa ya kusikitisha na kuhuzunisha.
Ni ajari, ajari kubwa ya majini ilikuwa imetokea alfajili hiyo kilometa zipatazo 56 kutoka bandari ya mwanza mjini.
Meli kubwa ya mv bukoba iliyoundwa mwaka 1979 na iliyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilikuwa imezama umbali wa mita zipatazo 25 kutoka ufukoni mwa maji na zaidi ya watu watanzania 1,000 walikuwa wamepoteza maisha baada ya KUTOBOLEWA kwa meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17 tu.
Leo tarehe 21. 05. 2013 watanzania "tunasherehekea" miaka mingine 17 tangu kuzama kwa meli hiyo. Tarehe kama ya leo mwaka 1996 mji wa mwanza uligubikwa na simanzi ya kutisha, uwana uliozoeleka kwa shughuli za michezo wa nyamagana ukageuzwa kwa muda kuwa uwanja wa kupokelea miili ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo.
Nakumbuka siku hiyo hata zoezi letu la kuvuna mpunga liliishia hapo, na sisi kurudi nyumbani na kuelekea uwanja wa nyamagana kwaajili ya zoezi la kutambua miili ya watu waliofariki.
Baadhi ya maswali ya kujiuliza kwa watanzania wote leo, tunapo "sherehekea" ajari hiyo ni haya hapa:
1: Je, tulijifunza jambo lolote kutokana na ajari hiyo?
2: Kama kuna jambo tulijifunza, je tumefanikiwa kulifanyia kzai ipasavyo jambo hilo?
3: Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu leo??
4: je, tumekwishajijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu leo??
5: Je, taarifa/ripoti ya uchunguzi wa ajari hiyo ilifanyiwa kazi ipasavyo??
6: je, ni ajari ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo?? na kwa nini kama kuna jambo tulijifunza viendelee kuzama vyombo vingine majini??
Naamini wananzengo wengine mtakuja hapa na maswali mengine mengi tu, ambayo pia yanakaribishwa. Haya tupia swali ulilonalo kuhusu hii kadhia ya kuzama kwa vyombo vya usafiri majini.
View attachment 94600