Siku kama hii 1990

Siku kama hii 1990

prs

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
2,642
Reaction score
3,373
Kwanza kabisa salam Wakuu
Siku kama ya leo 9 September 1990 aliyekua Kiongozi wa Liberia Samuel doe alisulubiwa na kuuawa kikatili ..

Ni moja ya Dikteta ambaye alikua Mkabila, akijificha kwenye mwamvuli wa kupambana na Ufisadi..

Tarehe 12 April 1980 aliua Mawaziri wote wa Serikali ya aliyekua Rais(William), Walipigwa Risasi hadharani kwenye fukwe za Bahari..

Lakini nae Mwisho wake haukua Mzuri baada ya kujikuta kwenye mikono ya prince Johnson.

Nimeona tujadili kutokana na aina ya Viongozi tulionao kwa sasa. Je kwa mfumo tunaoenda nao Tanzania (ndiyo mzee ) kwa kila kitu, hakuna hatari ya kuzalisha kina Doe wapya?

Angalizo : hii mada haina mahusiano na Vyama tujadili bila itikadi.
cabinet-ministers-lined-up-for-execution-after-a-coup-in-liberia-1980_1.jpg
 
AISEE MBONA KADRI SIKU ZINAVYOKWENDA FUNUNU ZA UDIKTETA ZINAZIDI KUSHAMIRI???!!MLENGWA NI NANI LAKINI
Zinazidi kutokana na Mkandamizo wa Haki za Binadamu, Kuna matendo na kauli nyingi mbovu kutoka kwa viongozi ngazi mbalimbali hazijawahi hata kukemewa.
 
Mtoa post una akili mbilikimo na fikra mfu.unafkr watu woote ni mbulula km wewe?.acha upoyoyo,huyu rais ndie tulimwomba mungu atupe, na ametoka ametupa kweli.
 
Mtoa post una akili mbilikimo na fikra mfu.unafkr watu woote ni mbulula km wewe?.acha upoyoyo,huyu rais ndie tulimwomba mungu atupe, na ametoka ametupa kweli.


Ulimuomba peke yako , Sisi wengine tulimuomba Mungu atupatie Raisi BCM..
 
  • Thanks
Reactions: prs
Mtoa post una akili mbilikimo na fikra mfu.unafkr watu woote ni mbulula km wewe?.acha upoyoyo,huyu rais ndie tulimwomba mungu atupe, na ametoka ametupa kweli.
Mkuu Wapi nimemtaja Rais kwenye mada? 😂
Nimesema Viongozi kwa ujumla,ila kama huyo uliyemtaja naye ana sifa tajwa hapo juu tumjadili pia,

Mkuu Viongozi wa Kisiasa wanapatikana kwa kura si maombi 😂
 
Wewe jamaa tunaijua vyema historia ya Sgt Samuel Doe hivo uclete matango pori humi kwa chuki zako. Lakin punguza kichwa maji
 
Liberia wana Rais mwingine pia Taylor nae kaishia kubaya
 
  • Thanks
Reactions: prs
Back
Top Bottom