Uchaguzi 2020 Siku kumi za kuamua

Uchaguzi 2020 Siku kumi za kuamua

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Leo nitazungumza sana siasa za Ubunge. Ukicheza vibaya hasa katika siku kumi za mwisho unaweza kuambulia 0 na ukicheza vizuri unaweza kushinda sana.

Siasa ni sawa na masomo ya darasani hasa kwa wanafunzi wa sekondari. Unapoanza unakuwa na masomo wastani kumi. Lakini ukifikia kidato cha tatu unaweza kuchagua kuendelea nayo kumi au kupunguza. Unaamua kumpunguza kwa kuwa unaona uwezo wako wa kwenda nayo yote 10 ni mgumu na unaweza kufeli vibaya.

Hata kwenye siasa, vyama vilipotangaziwa siku 70 za kampeni wapo waliokwenda na majimbo yote, wapo waliochagua majimbo 200 na wapo waliochagua majimbo 100. Lakini kadri Kampeni zinavyoendelea mtu anaanza kupata majibu kuwa haya niliyoenda nayo 100 ninayamudu au yamenizidi? Ukiona yamekuzidi ndipo kanuni inatupa nguvu ya kuchagua machache siku kumi za mwisho ili kuyafanyia mashambulizi.

Tunakuwa na tathmini ya siku kumi za mwisho kwa kuwa bila tathmini unaweza kukosa hata jimbo ambalo ulipaswa ushinde. Kwa mfano mwanafunzi anayesoma masomo saba hawezi kusoma masomo yote kwa nguvu sawa. Katika masomo saba yapo ambayo hata asiposoma sana anapata B, lakin yapo ambayo hata akikesha anapata C. Sasa ili Mwanafunzi huyu afaulu vizuri anapaswa kusoma sana somo analofaulu na somo ambalo hafaulu sana anaweza akawa anasoma ili asipate F. Lakini akitumia nguvu kubwa kusoma somo analofeli basi kuna uwalakini hata somo alilokuwa akipata B akapata D kwa kuwa alitumia akili nyingi kusoma somo analofeli.

Hata kwenye siasa tunajua. Kuwa jimbo hili na hili ni la chama fulani, vinginevyo nitumie nguvu kubwa. Lakini wakati mwingine unaweza kutumia nguvu kubwa kukomboa jimbo X na ukafanikiwa. Lakini kwa kuwa ulitumia nguvu kubwa kukomboa/ kutafuta jimbo X na majimbo mengine ukawa unatumia nguvu ya kawaida basi kuna hatari Unaweza kufanikiwa kupata jimbo X lakini ukapoteza majimbo y, Z, K, M, T n.k.

Siku kumi za mwisho ni mhimu sana. Hizi zinaweza kukufanya ukalia baada ya matokeo au ukacheka . Siku kumi za mwisho ni za kuamua ninakufa na majimbo yapi na yapi ninaamua kuyaacha ili tu upate uwakilishi kwenye vyombo vya dola. Mwanafunzi asiyeweza kuchagua masomo anayoweza kusoma na kufaulu basi huyo anajiandaa kushindwa.

Tafakuri njema.
 
Kura kwa Chadema na Lisu

CCM, Ndugai na Magufuli wamepora haki za Wafanyakazi wanyonge.

FAO la kujitoa...

Bring back Fao la kujitoa
 
Back
Top Bottom