Siku moja kabla ya Uhuru: Tanganyika nini kilitokea tarehe 8 December 1961?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Leo tunajua kwamba tarehe 9 December 1961 Tanganyika ilipata Uhuru.

Tunajua Nyerere alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza. Tunajua bendera ilishushwa na ya Tanganyika ikapandishwa. Lakini kuna swali moja ambalo historia ya vitabu mara nyingi hailisimulii kwa undani:

Tanganyika ilikuwaje siku moja tu kabla ya Uhuru?

Kiufupi, tarehe 8 December 1961, mtu wa kawaida aliishi katika nchi ambayo bado ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza, lakini kesho yake ingekuwa taifa huru.

Dar es Salaam ilikuwa ikijiandaa kwa sherehe kubwa, wageni walikuwa wanaingia, viongozi walikuwa wakijiandaa, na mamilioni ya Watanganyika walikuwa wakisubiri ukurasa mpya wa historia.

Hebu turudi nyuma kwa saa 24, tuone Tanganyika kabla haijawa nchi huru

Wangapi mlikuwepo siku hiyo?
 
Wakati Tanganyika inapata Uhuru, barabara zote za mitaani Kinondoni,Ilala,Temeke na Ubungo zilikuwa za lami. Na sio Dar tu, karibia mikoa yote mijini kulikuwa na lami mitaani. Njoo leo miaka 60++ baada ya uhuru ushangae. Wakati mwingine huwa nahisi ni Bora Nyerere angewaacha waingereza waendelee kukaa nchini mpaka leo tungekuwa mbali, wangewaambia wakaitane kwa wingi wapangilie makazi yao, mpaka leo 2026 tunahangaika na machinga na raia kujenga bonde la msimbazi na jamgwani😂😂 Kuna kisiwa kinaitwa Grand Cayman kiligoma kupewa uhuru wakasema waendelee kuwa chini ya muingereza, mpaka leo kina maendeleo makubwa sana. Mtu mweusi kujitawala ilikuwa bado. South Africa wamekuwa huru 1994 angalia wanachofanya ANC kushibisha matumbo tu😂
 
😅ah mkuuu!
 
Back
Top Bottom