Wakati Tanganyika inapata Uhuru, barabara zote za mitaani Kinondoni,Ilala,Temeke na Ubungo zilikuwa za lami. Na sio Dar tu, karibia mikoa yote mijini kulikuwa na lami mitaani. Njoo leo miaka 60++ baada ya uhuru ushangae. Wakati mwingine huwa nahisi ni Bora Nyerere angewaacha waingereza waendelee kukaa nchini mpaka leo tungekuwa mbali, wangewaambia wakaitane kwa wingi wapangilie makazi yao, mpaka leo 2026 tunahangaika na machinga na raia kujenga bonde la msimbazi na jamgwani😂😂 Kuna kisiwa kinaitwa Grand Cayman kiligoma kupewa uhuru wakasema waendelee kuwa chini ya muingereza, mpaka leo kina maendeleo makubwa sana. Mtu mweusi kujitawala ilikuwa bado. South Africa wamekuwa huru 1994 angalia wanachofanya ANC kushibisha matumbo tu😂