Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
1. Siku Moja Utastaafu
.
Hautakua ukienda kazini, hautakua na madaraka tena, hautakua na nguvu ya ushawishi, mzunguko wako wa pesa utapungua kabisa!
Chunguza/fuatilia tarehe yako ya kustaafu kwenye risiti yako ya malipo ya mshahara.
2. Tumia Vizuri Siku Zako za Likizo ya Mwaka.
Chochote utakachokifanya Likizo ndio utakachokifanya ukistaafu.Kama unatumia likizo kulala au kuagalia Luninga ndicho utakachokifanya ukistaafu.Tumia wakati wako wa ziada kujifunza kitu, kitakuja kuwa na manufaa ukistaafu.
3. Wekeza Kwa Ajili ya Kustaafu Kwako.
Watoto wako sio uwekezaji kwa ajili ya kustaafu kwako. Usiwategemee watoto, ndugu, au marafiki kama benki yako. Utapoteza heshima na utu wako.
4. Tafuta Shughuli Unayoipenda/Unayoifurahia wakati bado upo kazini ikuongozee katika kustaafu kwako mfano kufuga kuku au miliki duka pata ujuzi unaojiuza (sio vyeti visivyo na matumizi)
5. Utastaafia Wapi?.
Jijengee nyumba. Usistaafu ukiwa bado unapanga nyumba.
Usigome kutoka kwenye nyumba ya serikali.