Kuna boss mmoja kastaafu juzijuzi tu hapa yani ni anatia huruma. Amestaafia kwenye nyumba ya serikali alikuwa anajenga ila sidhani kama alishamaliza kwa sababu kaomba anedelee kubaki kwenye nyumba ya serikali. Halafu alikuwa boss mkubwa tu yani CEO. Mpaka amestaafu alikuwa hana biashara yeyote ile. Kuna siku nimekutana nae kakonda ghafla yani kaishaa na uzee ndio unaonekana dhahiri sasa.. wakati huo alikuwa anaftwa na V8 nyumbani sasa hivi anaendeshwa na harier
Wakati akiwa kazini alikuwa hakai ofisini yani hizo safari zake zilikuwa ni balaa.. kama ni pesa alipata sana ila sijui kafanyia nini.. Na alikuwa akikuchukia anakuhamisha anakupeleka sehemu nyingine ukafe njaa. Alihamisha sana watu ofisini na alikuwa hapendwi. Sasa hivi anaishi maisha ya unyonge na hata mwaka bado hajamaliza tangu astaafu.
Tujifunze kuishi na watu vizuri tukiwa kazini..