mara nyingi kwenye vipindi vya redio au tv mwishoni mtangazaji anamaliza kwa kusema 'tukutane tena kwa kipindi kingine siku na muda kama huu''. je, hii ni sahihi kweli maana muda huo ndio kipindi kinaisha hivyo!
Mfano, kipindi kinaitwa "Habari kutoka mikoani", kinaoneshwa au kutangazwa kila siku ya Jumatatu saa 2.30 usiku. Kwa hivyo wanaposema siku na muda (wakati) kama huu ni kuwa kitaoneshwa (siku) Jumatatu inayofuata (na muda) saa 2:30. Utata uko wapi?
Neno linalosaidia kuondoa utata ni kama. Ingesemwa tu "tukutane tena siku na muda huu" utata ungekuwa mkubwa. Tungo ni sahii kisarufi.
Ila kwa mantiki kuna utata mdogo: siku na muda kama huu haujaweka wazi kama ni juma lijalo, mwezi ujao au mwaka ujao.
Vilevile muda anaoutaja mtangazaji ni muda wa kufunga kipindi; hivyo ukimfuata kimantiki mtangazaji utakuta kipindi kinaisha.
Utata wote unaondolewa na ukweli kwamba lugha na matumizi yake hutegemea sana makubaliano na muktadha ama mazingira ambamo jambo hutokea; hivyo kuelewana kati ya msemaji (mwandishi) na msikilizaji/msomaji/hadhira hakutegemei sana mantiki ila makubaliano (ambayo wenzetu wataita "convention").
Tusemeni ukweli jamani ! Katika matumizi ya lugha tuepukane na maneno tata ambayo yatawachanganya wasikilizji au wasomaji wa taarifa zetu. Hivyo tuwe makini tunapochagua maneno ili tueleweke vema, pasi kuwa na mkanganyiko wa kifikra! :fish2:
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.