Siku nilipokikataa cha ukucha.

Siku nilipokikataa cha ukucha.

Mr the dragon

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2017
Posts
1,937
Reaction score
3,718
Since day one maraia walinimanya kwa gambe na harakati za ku exist na mali.Kuna manzi aliniletea hesabati za kidenzi nikamaindi sana.Ndio mara ya kwanza nikaenda kutafuta cha ukucha bablai nimeditate nigani.

Tokea hiyo siku ikawa kama dozi kwa fasi.Nikiamka asubaa naibuka kwa sadari nachukua mapinchi ya kushi napanda nakaa chimbo alone navinyonga kisoro si unajua ndo mwanzo tena wa kula ma kaya nini.

Mamaeee siku moja nimeingia chimbo na machizi wawili,mmoja alikuwa sadari akawa anavitengeneza ili vipushiwe.Siku hiyo mali ilikuwa una exist bila kumuachia madusiko kwa sababu mzigo ndo unatoka.Ni kama msosi ndio unaandaliwa.Siku hiyo nilikula vipande kama vyote nikaanza kuona wenge,nashindwa kupumua nikaamua niwatoroke wale machizi nisepe.

Nikawa narudi bwenini nikakutana na mchizi mmoja nikaanza kumtukana namwambia kaungua ana ngoma na niaje.Mchizi akamaind kikatokea kisanga fulani mixer ugomvi nikapelekwa kwa ofisi ya headmaster.Ikawa kesi kubwa mpaka bi mkubwa akaja skuli.Alipoambiwa mwanao ameanza kula kushi mazaa alitoa chozi kinyama.Iliniuma sana tokea siku hiyo nikaachana na cha ukucha.

Maraia Cha ukucha kwa sadari ni kwere asee.
 
Kuna tafauti kubwa kati ya baNGI na BaNGE,wengi bongo wanatumia Mibange wakidhani ni Bangi
 
Back
Top Bottom