Askarimaji
JF-Expert Member
- Jan 28, 2016
- 269
- 651
Mimi umri wangu ni miaka 40 na zaidi kidogo, naish Dar es salaam na nimezaliwa hapa hapa Dar japo mie sio mzalamo,
Siku moja miaka 10 iliyopita nilipokea taarifa kuwa dada yangu wa mwisho kuzaliwa kwenye tumbo letu ni mjamzito na mimi kaka mkubwa kwenye familia nafichwa, sababu dada alikuwa kidato cha pili, nilienda home kwa mama nikathibitishağŸ˜ğŸ˜•
Hasira nilizokuwa nazo nikataka nimfate aliyempa mimba nimuweke ndani miaka 30, mwishowe nikapuuzia kuchukua hizo hatua japo mie ndio nilikuwa nalipa ada ya shule, ndoto za masomo kwa dada zikakatika hapo hapo, akawa mzazi, akaniletea mjomba ambae ni kipaji maalum kichwani,
Dada na baba mtoto wake wakazinguana wakawa hawana mawasiliano mazuri, kipindi icho mtoto ana miaka mitatu,
Dada akaja kuchumbiwa na Askari polisi mmoja hivi ambae tuna ujamaa nae, Dada akaolewa.
Askari polisi akaamishiwa kigoma kikazi, wakaondoka na dada, Dada akaenda na mtoto wake uyo wa miaka mitatu ambae ni kichwa sana yan, wakiwa kigoma dada hakutaka mawasiliano yoyote na mzazi mwenzie maana waligombana then tayari amekuwa mke wa mtu, hivyo bas yule baba mtoto aliishia kujua tu kuwa mwanae kaenda kigoma ila hakuwa na mawasiliano nae wala hakuhusika kwenye huduma za mtoto, mtoto akaanza shule chekechea mpaka shule ya msingi, dada akajifungua mtoto mwingine wa kike na yule askari kumbuka yule mtoto wa kwanza ni wakiume,
Mtoto wa pili akafikisha miaka miwili dada akashika mimba nyingine ya mtoto wa tatu ila yule askari anakuwa mtoto wake wa pili, mumewe askari anaenda masomoni wakati huo anamuacha dada pekeyake nyumbani na watoto pia na kitumbo,
Mumewe anampa wazo nenda Dar kwa mama tumbo lina miezi mitano.... Nenda mpaka utakapojifungua ndo urudi na mimi nitakuwa nishahitimu mafunzo, Dada anapokea wazo anatimba Bongo Dar es salaam, sijamuona dada yangu takriban miaka mitano, anakuja mtoto wake wa kwanza Junior akiwa darasa la nne, Familia tunafurahi kumuona tena, anaenda nyumbani kwa mama, mimi niko kwangu na familia yangu,
Dada anamchukulia uhamisho wa muda mfupi mwanae, anampeleka shule moja ya msingi ya karibu na pale nyumbani magomeni kwa Bi mkubwa, lengo lake akishajifungua atarudi tena kigoma na familia yake.
Junior alipopelekwa ile shule akapendwa sana na walimu wa shule nzima hasa mwali wa darasa na mwalimu mkuu, akawa maarufu kwa walimu wote wa ile shule kwasababu ya umaridadi wake katika kuzungumza na pia akili darasani, anashika namba moja kila siku yan. Akiwa anaongea utasema uko na mtu mzima mwenzio, anajiamini sana kupitiliza, hana ule uwoga wa kitoto kwa walimu pia ata kwa mkubwa yoyote akiwa anazungumza nae,
Baba yake ni bodaboda pale kariakoo na mimi mjomba shughuri zangu ni fundi computer pale kariakoo, hivyo bas shemeji huwa tunaonana sana pale kariakoo, mara kadhaa shemeji alishanilalamikia kuhusu kutomuona mwanae na ugomvi wake na sister, bas bwana sikumoja nakutana na shemeji pale kariakoo nikamwambia.. "Shemeji mwanao na sister wamekuja wapo home kwa bi mkubwa.. Nenda kamuone mwanao", Shemeji akafurah akaenda kumuona mwanae baada ya miaka takriban mitano, shemeji akawa akauki shuleni kwa dogo, walimu wote wakamjua kuwa ndo baba Junior, akifika shuleni anatoa ela za soda kwa walimu pale shuleni, walimu wakampenda baba na mtoto pia,
Shemeji akawapa story fupi walimu ya yeye na mama mtoto, pia jinsi alivyoondoka na mtoto, na mwishowe akawaambia walimu kuwa hapa uyu mtoto amekuja kwa muda mfupi tu, mama yake akijifungua atarudi kigoma pamoja na uyu mtoto... Ivyo bas nitatenganishwa tena na mwananguğŸ˜shemeji akaonyesha huzuni kwa walimu,
Walimu wakamwambia usikubali aondoke nae, uyu mtoto ameshakuwa mkubwa, ana miaka tisa mpaka kumi unastahili kukaa na mwanao, usikubali... Sisi walimu tutakusaidia usijali.
Wale walimu walimpenda sana mtoto jinsi alivyo kichwa, hawakutaka aondoke ile shule, Pia wakampenda baba jinsi anavyomfatilia mtoto wake kwa karibu, wakamfundisha baba vitu vya kufanya mtoto asiondoke, mara kadhaa dada yangu alienda pale shule walimu walimuonyesha chuki ya wazi wazi, hawakumpenda mama kwa sumu alizozieneza baba junior pale shuleni kwa walimu,
Muda ukafika dada akajifungua, baada ya miezi miwili dada anajiandaa kurudi kigoma na familia yake,
Anafika shuleni kufata uhamisho wa mtoto walimu wanamgomea, wanampigia simu baba mtoto, Baba junior akafika shuleni fasta na bodaboda yake, ukazuka mzozo mkubwa, walimu wanamfundisha baba junior aende fungua kesi polisi dawati la jinsia wapate barua kutoka pale kwenda ustawi ngazi ya kata, wakampa moyo utashinda kesi mtoto ameshakuwa mkubwa, kweli bwana kesi ikaenda polisi dawati la jinsia na mimi mjomba nikaenda kumpiga kampani dada yangu siku iyo,
Kesi ikapelekwa ustawi wa jamii ngazi ya kata,nahisi kuna vitu alifanya baba junior pale, dada akashauriwa amuachie mtoto baba yeye aende kwenye ndoa yake kigoma, Dada alikuwa anakataa akisema baba mtoto hana mke na kule kwao mazingira yake sio mazuri lakini haikusaidia kitu mwishowe dada akaacha mtoto akaenda kigoma.
Baba junior kumbe tayari anawatoto wawili, Junior ana mdogo wake wa chekechea ambae nae kachukuliwa kwa mama yake then hawa wawili wote wakatafutiwa mama wa kambo ambae hana mtoto hajawai kuzaa ndo akawa anawalea pale tabata, wanakaa tabata,
Uyo mama hajaolewa anaish tu na baba Junior, ivyo bas analea watoto wawili ambao sio wakwake, baba mtu anatoka nyumbani saa moja anarudi saa tatu usiku.
Baada ya siku kadhaa Junior akakatazwa na baba yake marufuku kwenda kwa bibi mzaa mama yake, Bibi ambae anapokaa nyumba inaangaliana na shule anayosoma Junior pale magomeni, bibi akafanya jitihada za kumtafuta mjukuu pale shule... Alipompata mjukuu akamwambia baba amenikataza nisije kwako atanipiga, Bibi akashangaa mbona hivi... Mjomba nilipomtembelea mama pale home nikaambiwa lile jambo🤔
IItaendelea.............