Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Acha kuongopea watu hakuna jini mwema.
Kwa akili yako ya kizwazwa ni sawa na kusema hakuna wanaadamu wema!!! Vua hicho kiatu cha ujinga.Majini nj viumbe wameumbwa na Mungu ..wapo wema na wabaya...Majini wabaya hupata sifa ya kuitwa MASHETANI. USHETANI ni sifa haya binadamu akiwa muovu ,muasi huitwa Shetani.
 
Mbona iko wazi? Wewe kisa kirefu kama hiki utakaa ukiandike kwa siku moja? Huna kazi nyingine za kufanya? Hata wewe najua hushindi jf muda wote sasa iweje mtu ashinde jf muda wote kisa anahadithia kisa cha maisha yake. Hata redioni huwa hawamalizi kuhadithia kwa siku moja na hapo wanaongea tu,je kuandika!?
 
Ila kuna watu ni wazuri ktk kuandika imagine mtu kesha pangilia kabisa itakuwa sehem 28? .... kwahiyo kwa luga rahisi anatusisitiza tuendelee kupiga mtori nyama tutazikuta chini
 
Dah una bahati sana mkuu,jini kakupa gari,simu janja n.k lakini kazingua sehemu Moja ,ni kwanini akupe million 1 tu wakati ana uwezo wa kupata Kila kitu?

Million moja unafanya biashara gani.[emoji1787][emoji1787]

Sema nini ,inaonekana mlishaachana kwahiyo jini Fetty ni ex wako si ndiyo?

Na Mimi naitaka hiyo nafasi kwa jini fetty.kwasababu we muoga halafu siyo mjanja we Smart phone tu huwezi kutumia ndiyo maana ukawa unampa tabu jini wa watu,oooh sorry jini wa majini [emoji23][emoji23][emoji23]

Je, kwenye faragha yenu jini alikuwa akipendelea style ipi?

Ya tozo,ya Ndugai kujiuzulu,au ya presenter Mina ally? Na Kuna hii mpya ya wema kukosa private car akitumia sana Uber.

Jini Fetty alipendelea ipi ?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]

Mimi namtaka Fetty japo Nina sura ya Robert Mugabe siyo kesi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]

Maana mwenzangu ulipendewa uhandsome
 
Nimeogopa eti
 
Sema mie ntashindwa hapo kwny gambe dadeki yan anipe mpunga afu nisilewe weekend ntakua nafanya nini sasa....
 
Una kitu mnajimu
 
Brother una kitu, kuna vitu umesema inafikirisha endelea kutufungua
 
Mkuu noma sana dah masimulizi yanaleta hadi msisimuko this shit kumbe ipo aisehhh dah, je baada ya kuachana nini kilighalimu hasa
 
Inaonekana huyo jini alikua danga yaan katembea na Babu Hadi mjukuu???? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] Mbona inanitisha hii. Na inaonekana mliachana baada ya kugundua ni jini danga
 
SEHEMU YA 10
****************************************
Ilipoishia ni pale nimepewa gari na fetty pia ndani ya gari nikakuta begi jeusi kubwa ndani lilikuwa na shs millioni moja pamoja na simu kubwa aina ya samsung smartphone,
Na pia ni pale nilipoongea na fetty akaniambia kesho anakuja na tunahama tunaenda kuishi masaki huku pia akisema kuwa tupo katika vita kubwa na salome sasa endelea,

#####
Simu ya salome ilinishtua sana nikasema salome ananipigia nn tena?
Ikabidi nipokee hallow mambo vp aliniambia salome,
Salama sijui ww huko?

Nilimjibu akaendelea kusema rafiki kuna mambo makubwa kila siku mungu ananionyesha juu yako upo katika wakati mbaya sana nikamuuliza kvp akaendelea kusema maisha yako yapo mikoni mwako kama utaniamini achana na fetty mrudie mungu wako anza kwenda kanisani hau ukiruhusu mimi nije hapo kwako nikuombee nitakwambia kila kitu,
Maneno ya salome yalinishtua sana lakini ghafla nikaona namzarau tu nikamwambia kata umekosa cha kuongea naomba usije nitafuta tena ukaongea huo ujinga wako wa kila siku nikata kata simu na kushusha pumzi ndefu huuuuuh leo tena huyu salome anataka nn kwangu?

Nikawa najiuliuza moyoni basi nikajisemea moyoni huyu mwanamke ananitaka kilazima huyu ndugu msomaji unajua mda mwingine nadhani yule jini fetty kuna vitu alinifanyia kwenye akili yangu yaani nilikuwa naona kama salome ananiambia maneno ya kijinga mno nikawa nahisi ananitaka kilazima tu,

Basi siku hiyo kwangu ilipita vizuri na kama kawaida usiku tulikuwa tunawasiliana na fetty alinipigia simu usiku wa siku hiyo tuliongea sana mambo mbali mbali nakumbuka usiku wa siku hiyo fetty aliniambia kesho tunahamia masaki rasmi nitakuja asubuhi mapema nikamwambia sawa ila nikamuuliza masaki tunaenda kwa nani akasema ondoa shaka mimi kesho nikija utajua kila kitu nikasema sawa,
Kweli asubuhi nimeamka pale nikawa nasalimiana na wapangaji wenzangu pale nikawa nawaaga kuwa sasa nahama hapo daaah wapangaji wengi walijawa wana masikitiko sana ila mmoja wa wapangaji wenzangu akaniuliza unahamia wapi nikawambia masaki akasema duh ongera sana masaki ni pakishua huko naona mambo sasa sio mabaya[emoji1]

Basi baada ya masaa kidogo wife akawa amekuja na safari hiyo fetty alikuja akiwa ameongozana na dada mmoja hivi nisiemfahamu akafika pale akasalimia wapangaji pale akawa ameingia ndani na yule mgeni ambae baadae alijitambulisha kuwa huyo ni rfk ake alikuwa ni mdada mmoja mzuri kweli nae alikuwa amevaa kiostadhat yeye alikuwa mweusi ila ana weusi flani wa kung,aa basi akaniambia fetty leo ndio tunahama hapa inabidi uchukue vitu vyako vya muhimu vingine unaweza wapa tu wapangaji suala lililonishangaza sana akaendelea kusema unaenda sasa kuishi maisha mengine kwahiyo sidhani kama kuna ulazima wa kubeba vitu vyote kama kitandani sijui vyombo hau godoro nikasema sasa hivi vitu tunaviweka wapi akacheka kidogo akaendelea kwani hauna rfk?

Umpe tu hapo nikamkumbuka broo mussa nikampigia nikamwambia bro. Njoo nyumbani kweli muda sio muda akafika ikabidi nimwambie kila kitu mimi nahama hapa ww kuna vitu nakuachia hapa kama kitanda na godoro na vyombo vyombo vichukue tu maskini bro mussa ni kijana nae anaepambana na maisha akuamini kuachiwa vitu kama hivyo alifurahi sana kweli nilichukua vitu vya muhimu pale na maelekezo yote nilimuachia bro mussa na funguo za chumba nilimpa yeye amkabidhi baba mwenye nyumba kuwa mimi nimeshahama kweli tuondoka kwa lile gari aina ya v 8 ambalo alinilitetea fetty alikuwa akiendesha gari lile tukaondoka sasa maisha yangu ya kuanza kuishi mjini masaki yakaanza tulifika baada ya masaa kadhaa masaki sikuamini niliposhuhudia tukifunguliwa gheti lilikuwa ni bonge moja la jumba kubwa niliposhuka kwenye gari fetty akanibusu

Akaniambia karibu kwangu hii nyumba nilijenga mda mrefu hapa alikuwa anakaa huyu rafiki angu kwa muda wote nikamwambia sawa ila ndugu msomaji sikuwahi kuwaza ipo siku nitakuja kukaa kwenye jumba kubwa kama lile basi tukaingia ndani ilikuwa ni nyumba ambayo unapanda kwa ngazi bonge moja la jumba nilikuwa naona kama naota mule ndani ya nyumba kulikuwa na vyumba sita nilikuja kuvijua baada ya kuelezwa na fetty katika vyumba sita chumba kimoja alikuwa akiishi huyo rfk ake fetty ambae baadae baada ya kuzoeana nae nilikuja kugundua yeye hakuwa jini ni binadamu kama mimi tu na alikuwa akiitwa mwajabu hapa kwa mwajabu kukutana na fetty ni stori ndefu mno tena sana kwann mwajabu binadamu kama mimi ameweza kuwa na urafiki na jini na aliniambia wana urafiki wa miaka 10 sasa na fetty amemsadia vya kutosha haya yote niliyajua baada ya kuzoeana na mwajabu katika kupiga piga stori kwa leo niishe hapa sehemu inayokuja utajua kila kitu na sasa simulizi imefika sehemu patamu sana

Muendelezo leo usiku

MUENDELEZO Soma Siku niliyokutana na jini kwenye daladala
 
Daaaah .... Jitahidi usiku mkuu
 
Mkuu Mungu akuongezee hekima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…