Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh aisee kumbe haya mambo yapo..unaweza dhani utani. Kwenye simu hakusema chochote baada ya kujitambulisha?Ilikua 2016 nilikua kwenye kipindi na simu ilikua silent nilivyo toka kwenye kipindi nikakuta missed call ina kama zero sita katika ILA sikuwaza chochote nikaamua kupiga ile namba ILI kujua alo nipigia ile simu inaita nasikia vyuma vinagongana yaani kelele kibao na ilivyo pokelewa nikasikia sauti ya kiume nikamuuliza nani akajibu me jini basi me nikajua ni mtu ananifaham ILA ananitania nikauliza tena nani? Akajibu jini nikaona anazingua tu nikakata na huku nikijisemea mjinga GANI huyu ananichora [emoji57]BASI nilivyo fika home nikapiga tena mwito wa ile simu nasikia vyuma tena na ikapokelewa BADO nikawa NASIKIA kelele za vyuma tu sisikia mtu akiongea hapo nikaogopa nikakata weeee varangati lilianza usiku alikua jini anatembea kama moshi mweusi hapo sielewi nilikua naota au nilikua macho ILA nilijipa UJASIRI nikaanza kukemea badae yule jini akaingia uvungun mwa kitanda mi nikaendelea kukemea KWA nguvu na hasira baadae akatokea dirishani nikasitua yaani chumban kama kuna kitu kilikua kinaendelea na nimesweat mwili mzima yaani siwezi hata kusogeza mikono BASI nikakata hapo kitandani kama dk 20 then nikaamuka na kuanza kuomba ni baadae nikalala siku ya pili tena akaja yaani moshi mweusi ule ule nilipambana nae akakimbia siku ya tatu tena alikuja nikapambana naye akakimbia akatokea dirishani na nikaendelea kufunga na kuomba na hakuja maisha yakaendelea ILA siku zile tatu zilikua chungu kwangu japo nyumban hakujua mtu
Hakusema chochoteDuh aisee kumbe haya mambo yapo..unaweza dhani utani. Kwenye simu hakusema chochote baada ya kujitambulisha?
Mhhh Wewe umesema ni Fundi lakini ulienda kununua kitanda cha inch 4 kwa 5 ......Fundi maiko kweli muda mwingine hata waandishi wa habari wanafanya tafiti kabla ya kuandika
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwa hiyo mkuu sasa hivi mpaka unaandika haya huna akili zako za awali , unazo akili alizokupa fatuma , [emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwel kazi ipo[emoji1][emoji1]pombe mkuu pia ni mazingira yamebadilishwa na fattuma ww ngoja utaelewa alikuwa ashanibadili akili
Sent from my SM-J260T1 using JamiiForums mobile app
Leta kisa mkuuWe usiwaseme hao viumbe me yalishawahi nikuta sina hamu hata
Mkuu bei inaendana na eneo husika na ubora wa kitu,kwahiyo isikupe shida.Naweza nisijue kila kitu ila bei ya kitanda na godoro nazijua mkuuu
Kuna jamaa anasema you are one of them.We usiwaseme hao viumbe me yalishawahi nikuta sina hamu hata
Kuwa mkweli na kauli zako mkuuu.watuchosha...blaa blaaa nyingi kuliko matendo.Yaani acha tu mkuu yaliyonipata ni makubwa kuanzia leo nitakuwa natoa vipindi viwili kila siku leo nashusha kipindi kingine saa tatu halafu saa tano nashusha kingine mkuu
Sent from my SM-J260T1 using JamiiForums mobile app
kudadek, laki nne ikaku supriseSEHEMU YA 03
****************
SIKU ile ilikuwa siku nzuri sana kulionja penzi la Fatumah ni mwanamke mzuri sana kuwahi kumuona katika hii dunia ya watoto wa Adam na Hawa[emoji18]
Basi tuliongea mengi sana na Fatmah siku hiyo alinionyeshea mahaba mazito hadi nikawa najisimemea sasa mke si ndio huyu nimepata kumbe sikujua kuwa nilikuwa nimepatikana[emoji29]
Tulionjoi sana nakumbuka usiku wa siku hiyo ya kwanza ya Fatmah kuja kwangu alinipika wali na kabichi na alinionyeshea upendo mmoja sijawahi pata kwanza alikuwa muda wote yupo kifuani kwangu amejilaza ananiambia maneno matamu mume wangu nashukuru mungu nimekupata wewe ni wangu nitakupa mahaba mazito maneno yake yalikuwa yakinipa faraja nikujua kuwa sasa nimepata mke
Nilihisi dunia ni yangu kufupisha stori siku hiyo ndio ikawa mwanzo wa mapenzi yangu mimi na Fatmah ambae ni jini bila kumjua basi usiku ukapita asubuhi nikiwa nimelala na Fatmah aliniamsha mume mimi leo naondoka naenda kwa dada nikamwambia mbona mapema hapo ilikuwa mida ya saa moja asubuhi nikamwambia kwa dadaako ungeenda hata mchana Fatmah akajifikiria basi akanijibu sawa basi ngoja mimi niamke nioge nikufanyie usafi leo
Basi akaamka pale kitanda ni mwanamke mrembo aisee yaani ukiambiwa kuwa ni jini unaweza bisha mazima basi mimi nikiwa kitandani pale nimejilaza Fetty akawa anaosha vyombo punde si punde akaanza kupika chai katika kitu ambacho kilikuwa kinanipa furaha ni jinsi Fatmah alivyokuwa akifanya kazi yaani ilishukua dk 30 kashapika chai kashaosha vyombo kashaoga kamaliza kila kitu akaja kuniambia amka uoge chai tayari nilishangaa sana nikamuuliza aisee umenishangaza sana yaani wewe mchapakazi mno dk 30 ushamaliza kila kitu akawa anacheka
Basi nikaenda bafuni kakuta maji nimeekewa na sabuni kila kitu kinaoga niliporudi sebuleni nilimkuta amekaa kwenye kitu akawa anatabasamu akaniambia mume umependeza ulivyoloana na maji alikuwa akiniangalia garden love zangu basi nikavaa nguo pale basi Fetty akaniambia mume nina zawadi nataka nikupe nikamwambia nipe tu akaniambia nina hii perfume ni kwaajili yako akanipa nilipoipuliza pale ilikuwa ni perfume yenye manukato makali mno yaani inanukia vizuri sana yeye Fetty akawa anafurahi tu nikamwambia ni nzuri mno ndio maana wewe unanukia vizuri kumbe unatumia perfume hii akasema ndio basi tukanywa chai pale huku tukipiga stori Fetty aliniambia swali moja ambalo lilinipa hofu aliniuliza......
Mimi nataka nizae na wewe watoto halafu nije niishi na wewe hivi karibuni upo tayari?
Swali lake lilinishtua mno ukiangalia na maisha yangu ya kuunga unga ningewezaje kuishi na Fatmah walihali sina kitu nikamjibu natamani niishi na wewe hata leo nizae na wewe pia ila sasa maisha yangu ndio bado najitafuta nilipomjibu hivyo akatabasamu halafu akaniambia usijali kuanzia sasa maisha yako yameshakuwa mazuri niamini mimi na kesho utapata dili la hela nyingi ambalo haujawahi kupata
Maneno yake yalinipa furahaa na kunipa wasi wasi pia nikamuuliza umejuaje?
Akacheka halafu akaniambia nimeota tu jana jambo ndoto sio lazima itimie muda mwingine inaweza kutokea kweli au isitokee jibu lake likanifanya nicheke nikamvuta karibu yangu na kumwambia nakupenda sana ni mwanamke wa kipekee sana huku nikamshika na kumpiga busu moja zito mdomoni mwake utamu wa busu langu ulimfanya Fatmah kulalama na kunishika kwa nguvu huku akiendelea na yeye kujivinjali utamu wa mate yangu mdomoni mwake kitendo kilichofanya wote kuangukia kitandani na sasa game kati ya yanga na simba ikaanza rasmi dimbani kwa mkapa stadium huku refa wa mchezo akiwa ni martin saanya ilipigwa mechi ya karibia masaa 2 bila mapumziko huku sauti ya chaga za kitanda zikisikika kwachuuu kwachuuu kachwuuuu baaada ya muda wote tukajikuta tupo hoii hooi tumechoka
Tukiwa tumetulia kitandani Fatmah akaniambia nakupenda sana nitahakikisha nakupa kila kitu kinachokiweza nikamwambia nitafurahi basi ikabidi twende kuoga na Fatmah asikwambie mtu mahaba tuliyokuwa nayo ni zaidi ya Julliette na Romi basi kufupisha stori baada ya kuoga tukavaa then Fattuma akaniambia sasa anataka kwenda kwa dadaake ila alinisisitiza nisije kumsaliti kwani ananipenda sana aliniambia kuja kwangu tena itachukua siku 3 atakuja tena basi nikamsindikiza hadi mtaa wao anapoishi na dadaake Sakina yule fundi msusi wa saloon maarufu kipindi hicho mtaa x.... Chanika tukaagana na mimi nikawa nimeenda kumcheki mwanangu Juma ni kama kakaangu kwani tumekuwa tukisaidiana kwenye shida na raha alikuwa hakai mbali na mimi bahati nzuri nimefika kwake nimekuta ndio nae amefika kutoka mizunguko yake
ooh kaka mambo vp adimu sana kaka sema una balaa ww juma aliniambia huku anacheka akinikalibisha ndani nikamwambia mimi nipo vp balaa gani tena akacheka sana akaniambia nimepata taarifa zako mtaani sasa hivi una bonge moja la demu mtoto shombe shombe, akaongezea haya buana dunia yako hii sema watoto wazuri wanataka hela nikamwambia ndio ni kweli nimepata tu demu kizali zali bro basi akaniambia ni jambo jema basi tukawa tunapiga stori zingine za kawaida,
Bro juma akaniambia vp madili yako ya ufundi yanaendeleaje?
Nikamwambia daah madili magumu sasa maana nilishagombana fundi mkuu akasema pole sana ila tuzidi kupambana basi tulipiga piga stori pale na bro basi ikabidi nimuage niende magetoni
Basi nikiwa nipo njiani naelekea ghetto nikaona sms imeingia kwenye simu yangu sms ilisomeka ni Fatmah hello mume wangu kwa mapenzi uliyonipa jana na leo nimekuachia zawadi ila ni surprise sikukwambia ipo kwako nenda angalia kitandani kwenye ule mto wa mwekundu utaiona nakupenda,
Sms hiyo ilinishtua sana nikajaribu kumpigia fatmah simu yake haipatikani nikawaza zawadi gani hiyo ikabidi nipige mguu wa haraka kurudi nyumbani huku maswali mengi kichwani nilipofika nyumbani kitu cha kwanza nilipofungua mlango ni kwenda kitandani kuutafuta huo mtu mwekundu kujua kuna nn sikuamini nilipotoa foronya ya mto ndani nilikutana na kitita cha elfu 10 kumi tupu ikabidi nizichukue niziesabu zilikuwa ni shs laki 4 nikashangaa sana ikabidi nijiulize hizi hela zote Fatmah amenipa kwaajili ya nini na kazitoa wapi nikiwa katika wimbi la mawazo nilipigwa na mshangao nilipoona mlio wa simu yangu ikimaanisha kuna sms imekuja ikabidi niusome huo ujumbe alikuwa ni fatmah ujumbe ulionishtua...
Itaendelea usikose sehemu ya 04 kujua nn kiliendelea baada ya kuziona laki 4 nilizopewa na fattmah na je nilipatwa na mshangao gan baada ya kusoma ujumbe ...
Halafu Chifu Hangaya kasema kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake, watu wanaanza kutoa povu... ndo muone sasa uhalisia huu. Mwana hapa anaishi Chanika, zari lililomdondokea ni kukutana na jini mpanda daladala!Moja ya kitu ambacho sitaweza kukisahau katika maisha yangu ni siku niliyokutana na jini kwenye dala dala nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2019 wakati nipo chanika nilikiwa natoka kariakoo narudi ghetto
[emoji15][emoji23][emoji23][emoji23] ... nimecheka kwa sauti mpaka boss wangu kashtuka ....duuh jamaa kaishauawa au mbona kimya
Inategemea mkuu..kudadek, laki nne ikaku suprise
maisha magumu sana
mkuu ni laki nne au milioni mia nne