B Prosper
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 2,527
- 4,097
Habari wana jukwaa.
Hiki kisa kila nikikumbuka huwa nacheka sana lakini kimenifanya nimwamini sana mke wangu.
Mnamo mwezi wa pili mwaka huu, ilikuwa siku ya ijumaa nikiwa nyumbani maeneo ya bustanini majira ya saa moja kasoro jioni, mke wangu alinifuata pale bustanini na kuniambia baba Prosper mimi najiandaa naenda kwenye mkesha kanisani.
Nilivyosikia hivyo moyo ukapiga paaa nikafikiri kama sekunde tano kisha nikamwambia Sawa nenda. Alivyoondoka pale bustanini sikuwa na mzuka tena wa kuendelea kumwagilia, nilikuwa na mawazo sana, vitu nilivyokuwa nawaza ni hivi
Roho yangu, moyo wangu na akili yangu vyote kwapamoja vikaniambia fanya haraka mfukuzie nyuma mdogo mdogo angalia atakakoenda.
Chapu kwa haraka nikaondoka pale bustanini nikaja home, wakati huo yeye alikuwa ameshamaliza kujiandaa, nilivyoona bado hajatoka nikazuga kwenda tena bustanini ili kupoteza kamuda kidogo
Baada ya dakika chache nikaja tena nyumbani na muda huo alikuwa ameshaondoka, nikazunguka nyuma ya nyumba ili nimchungulie nikamwona anapandisha kimlima kuelekea kanisani, hapohapo nikakimbia bombani nikanawa maji miguuni nikavaa njumu(viatu) zangu na prova jeusi huyo nikaanza safari
Nilitembea mbiombio ili nihakikishe namkuta na kumwona kwa karibu lakini sikumkuta, mapigo ya moyo yalienda kasi sana siku ile nikiwa njiani nikawa nawaza nikimwona anaingia kwenye nyumba ya mtu nitafanyaje? Je nigonge mlango? Au nisubirie nje ili nimsubiri hadi muda atakao toka nimdake? Sikupata majibu.
Baada ya kutembea sana bila kumwona nikasema au ameingilia ile njia niliyoiacha ambayo haiendi kanisani?? Au na yeye alikuwa anatembea kwa kukimbia ili awahi huko kanisani??? Sasa nafanyaje hapa!!
Nikaamua kutembea hadi mbele kidogo then nikaingia kinjia cha shortcut ambacho unapitia kwenye mapori hadi unaenda kuikuta ile main road niliyoiacha, baada ya kuikuta ile barabara nikaendelea kupiga tizi hadi mbele kidogo lakini sikumwona. Nikajiuliza tena au alikutana na boda ikambeba??? ghafla nikaona pikipiki inatoka nyuma yangu ikiwa imewacha taa nikaamua kuingia kwenye majani fulani ili kujificha isije ikawa hiyo pikipiki imembeba mke wangu halafu anione niko hapa wakati aliniacha nyumbani.
Basi, baada ya ile pikipiki kupita niliona ipo na jamaa wawili wa kiume, nikajiuliza sasa nifanyaje hapa nizidi kutembea?? Akili ikanijia nimtumie message, basi nikaamua kumtext 'Vipi umeshafika kanisani' akanijibu bado, nikamuuliza saizi uko wapi akasema nipo karibia kwa mzee(.....) alivyonitajia ile sehemu nikasema aaah kumbe yupo mbele yangu tena nikikimbia dakika mbili tu namkuta. Nikaamua kutoka kwenye yale majani na kuanza kupiga tizi la nguvu ghalfa nikamwona mtu kwa mbele ila sikuweza kumjua ni nanj kwasababu ya giza nikasema ngoja nimwandikie tena txt nikiona anashika simu nitajua ni yeye.
Basi nikamtext "mkesha mwema mimi nalala" ghafla nikaona mwanga wa simu akiwa ameshika mkononi naye akajibu mbona unalala mapema sana? Nikamjibu sina mishe ya kufanya ngoja nipumzike tu, naye akajibu sawa.
Sasa hapo nikawa ninauhakika kuwa aliye mbele yangu ni yeye, mara tena gari likatokea nyuma yangu ule mwanga ulikuwa mkali sana hivyo niliweza kumwona mke wangu tangu nywele hadi raba alizovaa nikasema hapa sawa, lakini ni lazima nihakikishe namfuata hadi mwisho wa safari yake, maana huko mbele kuna gesti nyingi huenda akachepuka huko mbele.
Yaale maeneo yenye guesthouse hakuchepuka akawa ananyosha barabara tu, alivyopita yale maeneo ya gesti bila kuchepuka nikajisemea huyu ni mwanamke ambaye sipaswi kumwacha. Basi kwakuwa alishakaribia kanisani na mimi nikajibanza kwenye ukuta wa nyumba fulani ili nione mwisho wa safari yake, alivyikaribia lile kanisa pale nje alikutana na wamama wengine wakasalimia wakapiga story kidogo kisha wote wakaingia kanisani.
Baada ya hapo, nikawaza tena isiwe ikawa amefika tu kuzuga hapa dakika chache halafu aondoke aende kwenye agenda zingine, nikaamua kujibanza kwenye miti ya pale kanisani ili nione kama atatoka, aisee nilikaa pale hadi mida ya saa saba usiku hakutoka nikasema wacha tu nirudi, basi nikarudi zangu mdogomdogo hadi nyumbani nikalala hadi alipofika mida ya saa moja hivi asubuhi.
Kwakweli hili tukio sitakuja nilisahau kamwe iliniongezea imani kubwa sana ya kumwamini.
Ni hayo tu wadau

- Tangu nimwoe huyu mwanamke huu ni mwaka wa 5 mbona hajawahi kwenda kwenye mkesha iweje leo?
- Mbona kaniambia kwa ghafla sana why?
- Kanisa liliko ni mbali sana ni mwendo wa lisaa na nusu hivi kweli anaenda huko tena na giza hili?
- Au anaenda kukutana na mwanamme sehemu? Lakini mbona hana tabia kama hizo au alikuwa anafanya kwa siri na leo wanataka wakajiachie usiku kucha??