Siku Rais Nyerere alipotinga kizimbani akituhumiwa Kuvamia Uganda kijeshi

cha1509

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
258
Reaction score
402
WAKATI akiondoka Dar es Salaam kuelekea nchini Liberia kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Wakuu wa nchi Huru za Kiafrika (OAU) uliopangwa kufanyika Julai 17, 1979, Rais wa Awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifahamu fika, kwamba pasingekuwa na vigelegele kwake mjini Monrovia kwa kushinda vita dhidi ya nduli Idi Amin wa Uganda, aliyevamia nchi yake Oktoba 30, 1978, na yeye Mwalimu akalazimika kuingia vitani bila kupenda.

Mwaka 1975, Mwalimu aliwapasha viongozi wa nchi huru za Afrika, kwamba chombo hicho (OAU) kilikuwa kikitumika vibaya kwa njia ya kubagua, kuhusu dhana ya nchi wanachama “kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine”, pale Idi Amin alipoanzisha kwa mara ya kwanza, chokochoko dhidi ya Tanzania bila kukemewa na umoja huo, kama ulivyofanya kwa matukio kama hilo kwa nchi zingine barani.

Katika taarifa kwa Umoja huo, Mwalimu alikuwa amesema, “Umoja huu ulistahili laana ya dunia na ya watu wa Afrika kuonekana Umoja wa (viongozi) wanafiki kwa kuridhia au kuonesha kuridhia mauaji yaliyokuwa yakifanywa na Serikali ya (Amin) Uganda kwa Waganda, na kwa uchokozi dhidi ya Tanzania”.

Mwaka 1975, majeshi ya Amin yalivuka mpaka kwa uchokozi na kuua watu, akiwamo Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Hans Poppe, na Amin akatangaza wameua askari wa kichina wa kukodiwa na Nyerere. Hans Pope alikuwa Mtanzania suriama wa Kijerumani. Amin alidai Jeshi lake lilivuka mpaka kufukuzia wavamizi waliotumwa na Nyerere kwa kushirikiana na Waganda waliokimbilia na kuhifadhiwa Tanzania.

Mwaka 1979, Mwalimu aliamua kukomesha udhalimu wa Amin, baada ya kushindwa kwa juhudi za kimataifa kumfanya ajirudi, na kwa nchi wanachama wa OAU kushindwa kuchukua hatua kwa pamoja.

Kwa kusaidiwa kidogo sana na Wanaharakati wa Ukombozi wa chama cha “Uganda National Liberation Front” (UNLF), Mwalimu alitangaza vita kwa maneno machache lakini yenye nguvu akisema: “Uwezo wa kumpiga tunao; nia ya kumpiga tunayo, na sababu za kumpiga tunazo. ……ameua watu wetu, ameharibu mali nyingi; tutampiga mshenzi huyu”.

Na hapo hapo, maandalizi ya mapambano mapana ya kijeshi dhidi ya Amin yakaanza hima na bila msaada kutoka nje.

Wakati huohuo, hapakukosekana watetezi wa Mkataba wa OAU, waliotaka kuona mmoja wa waasisi wa OAU, Julius Kambarage Nyerere, akipandishwa “kizimbani” kujibu tuhuma za kukiuka misingi miwili muhimu ya umoja huo, yaani, kwanza: “Kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine”, na pili, “Kuheshimu uhuru na mipaka ya nchi mwanachama”.

Siku hiyo, Julai 17, 1979, Mwalimu Nyerere alichukua kiti chake kwenye ukumbi huo wa Mkutano – Unity Conference Centre (UCC) jijini Monrovia, akiwa amedhamiria kutokubali kutolewa kafara kama mhalifu au mtu mwovu, kama ambavyo tu, kwa tabia na haiba yake ya kutokuwa na majivuno, mapokezi ya kishujaa yangemuudhi vivyo hivyo.

Miezi mitatu kabla ya mkutano huo, juhudi za mtandao wa kidiplomasia wa Mwalimu hazikulala usingizi katika kuzishawishi na kuzihakikishia nchi jirani kwamba nchi yake haikuwa na lengo la kunyakua ardhi ya Uganda, wala kutaka kuiingiza nchi hiyo ndani ya ushawishi na udhibiti (sphere of enfluence) wa Tanzania.

Numeiry apanga kumsulubu Nyerere
Mapema Mei, 1975, mtandao wa kidiplomasia wa Tanzania, ulinasa taarifa za nchi moja ya Afrika Magharibi kushawishiwa kulileta suala la Uganda lizungumzwe mkutanoni; mtandao ukaingilia kati kwa kasi, na nchi iliyoandaliwa kwa hilo ikalegea hima na kutupilia mbali ushawishi huo.

Lakini Sudan ya Rais Jaffaar El-Numeiry ilikuwa kichwa ngumu, ikaendelea kupiga filimbi ikijigamba ingefanya hivyo kwa madai kwamba, vita vya “Tanzania – Uganda” viliathiri kikubwa nchi yake kwa kufurika wakimbizi zaidi ya 2000 kutoka Uganda.

Kwa hiyo, wakati akiondoka Dar es Salaam, Mwalimu alijua jambo gani rafiki yake wa zamani (Numeiry) angezua mjini Monrovia; wala hakulegea, kwa kufahamu nini Nigeria, nchi nyingine yenye msimamo mkali, ingevurumisha dhidi yake mkutanoni. El-Numeiry na Mwalimu walikuwa maswahiba dhidi ya Idi Amin alipochukua madaraka kwa kupindua Serikali ya Rais Milton Obote, mwaka 1972.

Pia Mwalimu alifahamu mapema kwamba, Serikali ya Nigeria ya Rais, Jenerali Olusegun Obasanjo, mapema mwezi Aprili mwaka huo, ilichapisha taarifa fupi dhidi ya Nyerere, kulaani mfano uliooneshwa na Tanzania, wa kubadili Serikali ya Uganda kwa kutumia nguvu ya kijeshi kutoka nje, lakini (Nigeria) ikaamua baada ya hapo kucheza karata zake kwa kubania kifuani.

Hadi jioni ya Julai 16, 1979 mjini Monrovia, kulikuwa na matumaini makubwa kwamba, mgogoro kati ya Tanzania na Sudan juu ya Uganda ungeepushwa au kuepukika. Hata hivyo, matumaini hayo yalififia kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo ya dakika 90 jioni hiyo bila kutoa tamko la pamoja, kwenye hoteli ya Numeiry, kati ya viongozi hao wawili juu ya Uganda.

Pale mkutano ulipofunguliwa, Julai 17; mstari wa mapambano ya kivita tayari ulikuwa umechorwa, ingawa mapambano hayo yalitokea baadaye kidogo na bila kutarajiwa.

Numeiry, kwa nafasi yake ya Mwenyekiti aliyekuwa amemaliza muda wake, alikuwa akiwasilisha taarifa yake. Kikao kilikuwa kimefunguliwa na hali ilikuwa tete. Hadi anamaliza kusoma robo tatu ya hotuba yake, hakutaja neno juu ya Uganda. Shauku ikafifia; kwenye chumba kirefu cha Wanahabari (Press gallery) mshangao wa nguvu ukasikika kwa kutotokea kilichotarajiwa.

Chale zamcheza Mwalimu
Katikati ya ukumbi, Nyerere, ambaye kwa mkao alitenganishwa na Swaziland na Sudan, alikuwa tayari ameondoa chombo cha kusikilizia (earphones) masikioni na alikuwa akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa msafara wake, ghafla akarejesha masikioni chombo cha kusikilizia; Numeiry alikuwa ameanzisha mada juu ya Uganda.

Nyerere, huku akionesha kutofadhaika, alisikiliza kwa makini na kwa udadisi mkubwa. Kisha Numeiry, kwa maneno ya kuhesabu na kwa kujiamini, alishusha nyundo iliyomuumiza Nyerere akisema: “Mgogoro kati ya Uganda na Tanzania ambazo ni nchi mbili ndugu, ni wa kujutia na matokeo yake ni mfano mbaya na wa kusikitisha kwa Afrika”.

Numeiry akaendelea kukandia, akisema: “Naamini, sote tunawajibika kuheshimu na kuzingatia Mkataba wetu wa OAU, unaozuia nchi moja kuingilia mambo ya ndani na uvamizi wa mipaka ya nchi nyingine kwa njia za kijeshi…..”.
Mashitaka ya Numeiry dhidi ya Nyerere yalikuwa wazi na pevu. Kama vile kutaka kumkomoa zaidi Mwalimu, Numeiry akakaribisha na kuruhusu kusomwa kwa kile alichokiita “Waraka mfupi” kutoka kikundi cha “Ugandan Action Convention” kwenda OAU.

Naibu Katibu Mkuu wa OAU, Peter Onu akisoma: “Sisi wa Ugandan Action Convention… tunapenda kuweka wazi, na tunafanya hivyo hivyo kwa sasa; ulaghai na usaliti mkubwa wa Rais Nyerere kwa watu wa Uganda na dunia nzima, kwa kutwaa kwa nguvu nchi yetu ya Uganda kwa kisingizio cha kumpindua Idi Amin….”.

Kitendo hiki kilimuudhi mno aliyekuwa Rais wa Uganda, Godfrey Binaisa, akang’aka akisema: “Kama mkutano huu utatumika kwa lengo la kusoma barua zote za matusi na kupakana matope wakati waheshimiwa viongozi wamo humu……. Je, hii ni sahihi?”, alihoji, kisha akasusia mkutano na kuondoka yeye na ujumbe mzima wa nchi yake.

Kwamba tuhuma na kashfa zilikuwa tayari zimeelekezwa kwa Nyerere; je, angeweza kuzipuuza hivi hivi?. Hapana; si kwa mtu kama Nyerere, hasa ilipohusu jambo ambalo misingi inayofahamika ilikuwa imevunjwa.

Wawili hao (Numeiry/Nyerere) wakatazamana kwa nyuso za shari, hasira zikisomeka dhahiri machoni mwao; kamera zikafunguka kwa nuru ya muwako wa radi.

Ikawa kwamba Mwalimu hatakwenda mbele kwenye mimbari (rostrum) kujibu “mashitaka” mithili ya kizimba cha mtuhumiwa; atatumia haki yake ya kujibu tuhuma akiwa kwenye kiti chake. Lakini pamoja na yote hayo, hakufahamu kwamba viongozi wenzake wa Mataifa, hukosa raha anapokuwepo; yeye hufikiri kwa haraka sana, kwa uthabiti mkubwa na kwa kuelezea mawazo yake kwa kina na umakini mkubwa.

Aliwahi kuonesha uwezo huo kwenye mkutano kama huo kabla ya hapo, katika kipindi cha aibu kwa Taifa lake, pale Jeshi lilipoasi mwaka 1964; akalazimika kuomba msaada wa kijeshi kutoka kwa Wakoloni walioondoka, Waingereza; badala ya kuomba msaada kutoka kwa viongozi wenzake wa nchi za kiafrika. Kwa hilo akatuhumiwa kubeza uzalendo wa Kiafrika kwa “kuabudu” vya Wakoloni.
Mara ya pili ilikuwa mwaka 1965 katika pambano la malumbano ya maneno, maarufu kama “The Cairo Encounter”, kati yake na Rais wa Ghana, Kwame Nkrumah; hao wawili walipotofautiana kimtizamo juu ya ipi njia bora ya kufikia “Shirikisho la Afrika”.

Wakati Nkrumah alitaka kuona nchi za Kiafrika zinaungana mara moja; Nyerere alitaka Muungano huo uanze kwa miungano ya nchi kikanda (kama vile Shirikisho la Afrika Mashariki, Afrika Magharibi n.k.) kabla ya kufikia Shirikisho la Afrika nzima.

Hoja ya Nyerere ilishinda.
Mwalimu aliitisha akilini kumbukumbu hizo katika kutetea msimamo na maadili (principles) ya msingi bila kujikweza wala kubeza huruma aliyotarajia kutoka kwa iongozi wenzake. Angeanzaje kucheza mchezo huo wa sataranji?.

Alitakiwa kuonekana mwanzo kutoelewa jambo na mnyenyekevu kwa sauti na toni. Akasema, alikuwa na “Tatizo dogo na hati (document) ndogo” ya kuwagawia wajumbe kabla ya kuanza kujibu tuhuma dhidi yake; lakini ilikuwa lazima kwanza aombe kibali cha Mwenyekiti kufanya hivyo.

Hati hiyo ndogo ilikusudia kuelezea ukweli juu ya chimbuko la mgogoro kati ya Tanzania iliyoongozwa na yeye, na Uganda “iliyoongozwa na ndugu yangu Idi Amin”, alisema.

Akasema, alitarajia kuona tamko la Numeiry kubeba ukweli wa mambo lakini ilikuwa kinyume chake; akasikitishwa na kauli yake yenye kuhukumu.

Nyerere amshushua Numeiry
Baada ya kuweka msingi wa hotuba yake, sasa aliendelea na lile “tatizo dogo” alilosema mwanzo, na ambalo tayari lilikuwa kubwa kuhitaji kuchanwachanwa vipande vipande ili mkutano umwelewe.
Hati hiyo ndogo aliyowagawia wajumbe, ilielezea, pamoja na mambo mengine mengi kwamba; Oktoba 30, 1978, Idi Amin alivamia Tanzania kijeshi na kujitangazia kunyakua, kukalia na kutawala sehemu yote ya Mkoa wa Kagera ng’ambo ya Kaskazini ya Mto Kagera, maarufu kama “Kagera Salient”.

Mwalimu akasema, OAU haikulaani kitendo hicho cha Amin; na kwamba kama OAU ingemlaani Amin na kumtaka aondoe majeshi yake, hakuwa na sababu ya kupeleka Majeshi Uganda.

Akasema, Majeshi ya Amin yalirudi nyuma kwa shinikizo; yalipora mali na kuchoma vijiji, yaliua mamia ya raia na kuteka nyara raia wengine 200 na kuongeza kuwa alilazimika kufunga Mpaka na Uganda na kuvipa kipigo vikosi vya Amin vilivyokalia nchi kwa madhara makubwa kwa Tanzania.

Alijitetea kuwa, Jeshi la Tanzania halikukusudia kwenda zaidi ya mji wa Masaka nchini Uganda; lakini shangwe zilizowapokea wapiganaji wake kutoka kwa Waganda zilikuwa kubwa kumfanya Amin aape kuwaua wote walioshangilia Majeshi ya Tanzania muda si mrefu kwa kile alichokiita “kutenda kama marafiki wa Adui”.

Akasema, wanajeshi wa Libya walipoingia kumsaidia Amin, kulifanya Tanzania iingiwe na hisia za ubinadamu kwa Waganda waliotishiwa uhai, kwamba bila jeshi kumdhibiti Nduli huyo, wangeangamizwa kwa maelfu.

“Kuwaondoa askari wa Tanzania kungemaanisha kuruhusu Waganda wauawe kwa maelfu na majeshi ya Amin….”, jambo ambalo hatukupenda kuona linafanyika”, alisema Mwalimu.

Mwalimu akabadili kasi ya kusema na kuwa kubwa, kwa kutamka vyema mawazo yake, neno baada ya neno, alisema: “Hatutendi haki kwa kudai au kutoona ubaya wa nchi moja kuvamia na kukalia ardhi ya nchi nyingine; na nchi iliyovamiwa inapoitaka OAU kulaani kitendo hicho, inasemekana eti huko ni kuvunja Mkataba wa OAU….. huo ni unafiki wa kiwango cha juu usioweza kuvumilika”, alifoka Mwalimu.

Kufikia hapo, hoja ya Numeiry ikaanza kupwaya, kulegeana kushindwa; mkutano ukapiga makofi kwa kumshangilia. Mwalimu akaona, sasa karibu wote walikuwa upande wake kumwezesha kusema kwa ukali zaidi; akakemea akisema: “Ukimya wa kijinga kama huu wa OAU chini ya Numeiry, na kwa OAU kushindwa kumkemea mchokozi (Amin) baada ya kulalamika kwa Mwenyekiti huyo wa OAU, ni ishara mbaya na unahatarisha amani kwa Afrika”.

Mwalimu akamaliza hotuba yake kwa kumshutumu, kumshushua na kumlaani moja kwa moja Mwenyekiti (Numeiry) aliyekuwa anamaliza kipindi chake, na “kumpongeza” kwa kutaka suala la uvamizi wa Amin lijadiliwe kwenye OAU “sio na mvamizi, bali na mhanga wa uvamizi huo akiwa kizimbani”.

Ilikuwa ni hotuba yenye msisimko mkubwa, ya kukumbukwa, iliyojaa hekima na busara kubwa kufanya baadhi ya wajumbe kusimama wakipiga makofi kwa kushangilia bila kujijua.

Usiku huo, kwenye jumuiko la pamoja baada ya kikao kuahirishwa hadi siku iliyofuata, Marais Waandamizi walifanya kazi kubwa kupoza hasira za mahasimu hao wawili Nyerere na Numeiry, na makubaliano yakafikiwa kwamba suala la Uganda lisiibuliwe tena hadharani na mkutanoni.

Kwa jabari la Afrika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; kama ilivyokuwa kwa “The Cairo Encounter”, ukawa ushindi kwa aibu ya mahasimu wake na kuzidi kuipasha Tanzania katika siasa za Kimataifa, kimsimamo, uwazi, ukweli na kwa uadilifu usiohojika juu ya haki za binadamu.

Tunapotazama nyuma kuona nafasi na uwezo wa Tanzania katika “mimbari” ya kimataifa; ni muhimu tujiulize: nani kama Mwalimu Nyerere kwa waliomo madarakani na wajao katika kinyang’anyiro cha kuongoza nchi, atakayerejesha fahari ya Taifa inayopotea?.

Chanzo; JUL 15, 2015 by RAIA MWEMA
 
Last edited by a moderator:

JUL 15, 2015by RAIA MWEMAin

Hii kitu imenikumbusha mbali sana!...itoshe kusema tu kuna watu waliyoa uhai wao na miili yao ikawa handaki ya Risasi na ardhi ya vyuma vya mabomu yaliyolipuka ili Tanzania ibakie kuwa Tanzania!

Leo wengi wa watu hao leo hawatamaniki!....anyway ni kazi waliyoichagua!
 
Sioni yupo au yuaja mtu kama Mwalimu Nyerere. Hawezi kupatikana katika mazingira ya kuishi kwa amri kutoka juu, kudhibiti akili ya kufikiri independently na kuruhusu mpanuko wa TUNU za Taifa, kuishi kwa kudhibiti kukosoa viongozi wasioheshimu utu wa wananchi na sheria za nchi zaidi ya matamko, uongozi wa visasi na ubaguzi wa kibabe. Hapatikani mtu kama JKN. Tumepoteza tu, huo ndio ukweli mgumu kumeza.
 
Ki ukweli pamoja na mapungufu machache aliokuwa nayo Mwal tukubali tusikubali MWALIMU alikuwa Jabali
Kumbe kulikuwa na jabali,sasa hivi kuna jiwe,sifa nyengine bhana!!
 
Sioni yupo au yuaja mtu kama Mwalimu Nyerere. Hawezi kupatikana katika mazingira ya kuishi kwa amri kutoka juu, kudhibiti akili ya kufikiri independently na kuruhusu mpanuko wa TUNU za Taifa, kuishi kwa kudhibiti kukosoa viongozi wasioheshimu utu wa wananchi na sheria za nchi zaidi ya matamko, uongozi wa visasi na ubaguzi wa kibabe. Hapatikani mtu kama JKN. Tumepoteza tu, huo ndio ukweli mgumu kumeza.
With all due respect mbona Nyerere hakua mtu wa kuruhusu fikra mpya kihiiivyo,rejea wakina tumbo walivyofanyiwa.

Though all in all mzee alikua ni kichwa sana kwny nyanja nyingi saana.
 
alitawala kipindi cha ujinga totoro ndio maana hakukuwa na ulinganifu.
 
Last edited by a moderator:
alitawala kipindi cha ujinga totoro ndio maana hakukuwa na ulinganifu.

Mkuu hapana, sio kipindi cha ujinga ila kipindi kile kilikuwacha hatari sana kumbuka kulikuwa na nguvu ya west na east na nchi za Africa na viongozi wake walijikuta kwenye CROSSFIRE. Bila ya kufanya hivyo kwa mtazamo wangu leo hii nchi inayoitwa Tanzania huenda isinge kuwepo. Kambona, Kasanga Tumbo,James Maparara et al. walikuwa vibaraka wa west na walikuwa wakitumika kumuondoa mwalimu kama ilivyokuwa kwa nchi zilizokuwa na mapinduzi.
Mwalimu alikuwa na uwezo mkubwa na alikuwa na spy wenye kuweka mslahi ya taifa mbele na sio hawa wasasa
 
Hii kitu imenikumbusha mbali sana!...itoshe kusema tu kuna watu waliyoa uhai wao na miili yao ikawa handaki ya Risasi na ardhi ya vyuma vya mabomu yaliyolipuka ili Tanzania ibakie kuwa Tanzania!

Leo wengi wa watu hao leo hawatamaniki!....anyway ni kazi waliyoichagua!
Ndio maana naithamini sana jwtz
 
Mimi na mawazo yangu mabovu napata hisia Numery mwarabu fake alikuwa hatetei waganda au nchi yake kwa kupata wakimbizi wengi bali aliumia ndugu yake wa dini yake kung'olewa madarakani.

Maana jamaa(Idd Amin Dada) alisilimu na kuwaita waaarabu nduguze.

Kitu ambacho Numeiry na Ghdaffi walisahau ni kwamba Nyerere alikuwa mtetezi wa Palestine kiasi cha kujitenga kushirikiana na Israel.
 
Back
Top Bottom