Siku Rais Nyerere alipotinga kizimbani akituhumiwa Kuvamia Uganda kijeshi

Siku Rais Nyerere alipotinga kizimbani akituhumiwa Kuvamia Uganda kijeshi

Nzuri sana. Wadau isomeni yote najua mmezoea udaku.
Mwandishi wa hii makala atunge kitabu kabisa
 
Mwalimu J.K. Nyerere si tu alikuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri pia alikuwa msikilizaji mzuri wa hoja na hilo lilimsaidia sana kuweza kujipanga na kuzijibu kwa mashiko. Hakuwa mkurupukaji. Na pia alikuwa na uwezo mkubwa sana wa ushawishi. Wakati ule wa vita baridi, mwalimu alikuwa akionekana kuwa ndiye aliyekuwa msemaji mkubwa wa wanyonge wasiokuwa na sauti. Aliweza kuwa kinara kwenye lile kundi la nchi zisizofungamana na aidha mabepari au wakomunisti lilijulikana kama kundi la nchi za NAM (Non aligned movement). Hakuwa mnafiki na hakuwa fisadi au mpenda mali. Lakini kama binadamu mwengine yeyote, hakukosa mapungufu.
 
Mzee alikuwa jasiri sana na hakujali yupo eneo gani na watu wapi
 
Historia muhimu hii.

Ila mleta mada naona posti imejirudia, nadhani unge delete hiyo page ya pili.
 
Sioni yupo au yuaja mtu kama Mwalimu Nyerere. Hawezi kupatikana katika mazingira ya kuishi kwa amri kutoka juu, kudhibiti akili ya kufikiri independently na kuruhusu mpanuko wa TUNU za Taifa, kuishi kwa kudhibiti kukosoa viongozi wasioheshimu utu wa wananchi na sheria za nchi zaidi ya matamko, uongozi wa visasi na ubaguzi wa kibabe. Hapatikani mtu kama JKN. Tumepoteza tu, huo ndio ukweli mgumu kumeza.

Mi naamina wapo na watatokea tu siku moja, hayo mazingira uliyoyataja sio tofauti kabisa na mazingira yaliyokuwepo enzi za ujana wa kina Nyerere....hawa wamekuwa chini ya mkoloni ambaye hakutaka kuona wala kusikia fikra zinazompinga lakini pamoja na yote kina Nyerere walitokea!! iweje kwa hawa wa sasa ishindikane!?
 
Leo ni mwendo wa amri kutoka juu, watu wasiojulikana na gulio la wanasiasa. Ndicho runners.
 
Back
Top Bottom