.
Nyambala, nitakukumbusha kurudia maneno yako hayo hapo juu baada ya mshindi kupatikana. Hizi ni ndoto za mchana tena kabla hujapata usingizi, ukiota kwamba Dr Slaa atamshinda kikwete. Matumaini yangu kwa Slaa ni 2015 ambapo pia itategemea nguvu ya atakayekuwa mgombea kupitia tiketi ya CCM.
Maumivu ya kichwa yanaanza polepole..... meza tembe za Hedex mbili kutwa mara tatu (2x3) hadi kufikia tarehe hiyo utakuwa umepata nafuu. Sikulazimishi kufuata tiba yangu kama utakuwa na tiba mbadala kama vile Alovera au mwarobaini.
Naamini baadhi ya majimbo yanaweza kuchukuliwa na wapinzani lakini si Urais. Na hii haina maana kwamba nambeza Dr Slaa la hasha ni imani yangu tu.
You are both right and wrong my friend!
1/ Where you are wrong:
Kwenye ballot box nina uhakika Dr Slaa atamshinda JK (50% vs 40% or thereabouts).
2/Where you are right:
JK anaweza "kutangazwa mshindi" bila kujali kilichotokea kwenye uhalisia wa matokeo.
Hapa ninaongelea rigging (refer masanduku ya kuibia kura kule Tunduma ambayo yasemekana sasa yako Ngerengere).
Najua utajifanya kuniuliza: hizi fake votes zitaingiaje kwenye final ballot count?
Ngoja nikupe nyeti ndogo......kuna jirani yangu kada mkubwa wa CCM, ana kijana wake ambaye ni Chadema through and through na pia ni wakala kwenye kituo mojawapo.
Huyu kijana ame-confide kwangu kuwa baba yake anataka kum-corrupt. Apparently amemwambia kuwa kuna $$ nyingi zinamsubiri akikubali kushirikiana na CCM (hajamwambia kushirikiana kivipi lakini my 6th instinct tells me ni possibly kushiriki katika ku-swap masanduku ya kura baada ya upigaji kwisha).
Kijana alikuja kuniomba ushauri - I have tried my best to properly counsel him against this devious ploy and he seems to understand but huwezi kujua atafanya nini eventually.
Kwenye eneo hili sincerely nawashauri sana (kama walivyoshauri wengine wengi) watu waliopo kwenye intelligence ya Dr Slaa wawe makini.
Mimi si Chadema lakini kwa Dr Slaa nimejitolea kuwa kwenye hiyo intelligence - nitaifanya ki-vyangu-vyangu na ninajua mwenyewe cha kufanya nikiona uovu ukitendeka.
Enough is enough!