Siku tukiacha kuchagua Wabunge Wafanyabiashara tutaona Mapinduzi Makubwa ya Bunge

Siku tukiacha kuchagua Wabunge Wafanyabiashara tutaona Mapinduzi Makubwa ya Bunge

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Amini usiamini hili bunge letu ni la Wafanya Biashara siyo Bunge la wananchi. Asilimia 80 ni Wafanya Biashara wakubwa and not start ups.

Mfanya Biashara ni mtu ambaye all the time anawaza cash flow kwenye business zake. Always thinking ways to maintain his/her wealth...

At the same time mtu huyo huyo tunamtegemea aje atembee jimbo kuangalia Matatizo ya watu.. IMPOSSIBLE. Yaani akija huko jimboni most of the time atakuwa anaagalia fursa Tu za kutengeneza pesa Zaidi....

Tumeona Trump alipokuwa Raisi Ali declare public mtu atakayesimamia Biashara zake ili yeye afanye Kazi za Taifa. Hao wa kwetu wanapiga kushoto na kulia huwezi kutumika mabwana wawili

Kiuhalisia mfanya Biashara siyo mtu sahihi wa kutunga Sheria Kwa maslahi ya Taifa. Matokeo Yake wanapitisha Sheria amabazo zinawapa favor Wao kwenye Biashara zao.no Matter how mwananchi wa kawaida anaumia kiasi Gani ...


Wana conflict of interests nyingi Sana Hasa sheria za Kodi na uwekezaji na Wengi wao wanakimbilia jimboni kupata uongozi Ili kufanikisha mipango Yao. we jiulize Manji alikuwa mtu wa kugombea udiwani seriously?

Leo hii Tunashagaa eti lile azimio la Bandari limepitaje pale bungeni. Wale majamaa wote ni waigizaji wa mizigo kupitia hiyó bandari. Do you know which favour wataenda kupata baada ya ujio wa DP world...

Tuna. Watanzania wengi Sana amabao wanaweza kuwa wabunge na kusimamia Sheria za nchi Tofauti na hawa Wafanya Biashara mara zote wamekuwa wakiliangamiza Taifa...

WABUNGE WAFANYA BIASHARA SIYO WATU SAHIHI KUTUNGA NA KUSIMAMIA SHERIA ZA NCHI
 
Hakuna asiyependa kuwa mfanyabiashara, hata huyo asiyekuwa mfanyabiashara akipata chance atakuwa. labda itungwe sheria itakayowabana.
 
Back
Top Bottom