Asalaam Aleykum wana JF.
Moja kwa moja niingie kwenye mada.
Kila siku mambo yanazidi kuwa magumu kwa walio wengi kutokana na gharama za maisha kupanda kila uchao ilhali kipato kikiwa palepale au kikipungua. Hii inawahusu hata wafanyakazi wa umma na sekta binafsi ambao kiukweli hawajaongezewa mshahara kwa muda mrefu.
Ninapoongelea gharama za maisha ni kuanzia gharama za kununua chakula, mavazi, kodi ya nyumba, tozo, usafiri, gharama za matibabu n.k.
Kiukweli ndani ya muda wa miaka 2 hadi 3 kumekuwa na mfumko wa bei ambao hatujawahi kuushuhudia kwa miaka mingi huku viongozi wetu wakituaminisha sababu mbalimbali ambazo kwa sehemu kubwa nyingi hazina mashiko.
Nchi nchi yetu ina vyanzo vingi sana vya mapato kurokana na wingi wa raslimali tulizo nazo mfano ukiwa ni bandari, madini, mbuga za wanyama n.k.
Lakini pia kuna mashirika mengi ambayo kama yangekuwa na usimamizi mzuri, basi Tanzania ingekuwa katika viwango vya juu sana kimaendeleo. Lakini cha kusikitisha ni kwamba haya mashirika badala ya kuingiza faida, yamekuwa kinara kwa kuiingizia serikali hasara! Yaani badala ya yenyewe kutoa fedha kwa serikali, serikali ndo inatoa fedha kuyahudumia tena kwa kodi za wananchi wanyonge kabisa wa nchi hii!
Hii haikubaliki kabisa. Kwa sehemu kubwa ya wanaotusababishia maisha kuwa magumu ni wale ambao tumewaamini na kuwapa mamlaka ya kutusimamia.
Hivyo, siku tukijitambua na kuwaambia ukweli, hapo ndipo hali yetu ya maisha pia itabadilika kwa wema kuliko ilivyo sasa.
Mungu ibariki Tanzania,
Amin.