Siku watu wakikutana watakimbiana humu!


Kwa sasa itakuwa ngumu. Labda watu wasijitambulishe ID zao za mitandaoni!. La sivyo itakuwa sherehe kwa ccm. Mavuno kivulini.

BTW, si watu wote hapa ukiangalia wana tabia za kujisifia. Ninachotegemea ni kuona aina mbalimbali za watu kama:-

1) Wazee wakike na wa kiume, wastaafu waliofanikiwa maisha na wanaojutia uaminifu wao.

2) Viongozi wa juu wenye busara na hekima wasiopenda kujulikana na viongozi wa kati wenye viherehere.

3) Wasichana na Vijana wa kiume watanashati waliotulia na wasio na majigambo yoyote ya uzuri wao, pamoja na wanaojitahidi kutafuta kuonekana na kujionyesha kwa uzuri wa kulazimisha.

4) Vijana wa kiume na wakike waliofanikiwa maisha wakiwa wadogo kutoka familia bora na waliotoka familia duni na za kati.

5). Vijana wa kike na wakiume waliomaliza chuo wenye ndoto lakini wanapata shida kufikia ndoto zao kwa kukosa connections na opportunities huku wengine wakikata tamaa na wengine wakijitia nguvu za kusonga mbele.

6). Mashushu wa ccm na wasiojulikana wakilazimisha kujichanganya huku waki pay attention kwa kila kitu kinachoendelea hata kama si cha muhimu bila kujali kwamba hiyo inatakiwa kuwa sehemu huru ya watu ku relax.

7). Walevi na waropokaji na waborekaji haraka wenye kuzira na kuondoka.

8). Ninategemea watu wakimzunguka na kumtazama kwa hisia mchanganyiko mtu mmoja mzee kuliko wote, alilyejaa mvi kichwani, mrefu mwenye miwani, asiyekuwa na meno ya mbele, mwenye udadisi chanya, atakayewahi kufika na kuchelewa kuondoka kwenye tukio, ambaye ataanz akuomba lift kwa wajumbe saa sa kuondoka kwa kuwa hana gani wala baiskeli pamoja na kuwa mfanyakazi wa umma muda mrefu, anayejulikan akwa ID ya Mzee Tabby.

9), Wafanya biashara wa kati na wajasiria mali wakijitahidi kuuza ama kutangaza bidhaa zao waki socialize na watu wambali mbali.

10). Watu wakipeana namba za simu na anuani za mawasiliano, huku wengine wakimwogopa mshana jr !.

Mwingine aongezee orodha.
 
Hata tukikutana watu wengi wanatumia avatar sio zao hvyo hawata jitambulisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…