Kila mtu anakwambia yeye ameguswa na kazi ya raisi anataka kumsaidia kwenye jimbo atukatai Magufuli kafanya kazi nzuri.
Lakini hakuna mwenye agenda ya wananchi sana sana utasikia wanaongelea mahitaji ya barabara tu ina maana hakuna social issues zinazowagusa wakati kila uchao huko you tube mke kapigwa, bibi kaporwa mali zake, mtoto kalawitiwa, mama kanyang’anywa mtoto, mzazi ataki kutoa hela za matunzo, maiti imezuiliwa, bidhaa hazina bei ya ushindani monopoly; yaani kuna mambo kibao yanayotaka serikali kubadili sheria au kuboresha utaratibu wa kupunguza matukio yenye kugusa jamii na usikii ndio wana siasa gani hao.
Vyama vya siasa wajue bunge lilioisha lilipeleka watu ovyo sana kiasi kwamba dhana ya uwakilishi imepotea bunge limekuwa sehemu ya ushambenga wa vyama badala ya sehemu ya uwakilishi kupigania maslahi ya wananchi na kuisimamia serikali. Na ukiwa mwakilishi mzuri aina ya Bashe unageuka adui wa mtu kiazi kama kibajaji.