Siku ya Afya ya Akili Duniani: Serikali yasema Watanzania Milioni 7 wana matatizo yanayohusiana na Afya ya Akili

Siku ya Afya ya Akili Duniani: Serikali yasema Watanzania Milioni 7 wana matatizo yanayohusiana na Afya ya Akili

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Wakati Dunia ikiadhimisha Siku ya Afya ya Akili kesho Jumapili Oktoba 10,2021, imeelezwa kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni saba wenye matatizo yanayohusiana na afya ya akili.

Hata hivyo, sababu mbalimbali zimetajwa kusababisha matatizo ya afya ya akili huku Jiji la Dar es Salaam limetajwa kuwa na idadi kubwa ya wenye matatizo hayo.

Miongozi mwa sababu zilizotajwa kuchochea tatizo hilo ni msongo wa mawazo, ugumu wa maisha na matamanio ya kuwa na maisha bora.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa magonjwa yasiyoambukiza, Dk Shedrack Makubi amesema sababu ya Dar es Salaam kuwa na wagonjwa wengi ni kutokana na wingi wa watu katika jiji hilo ambalo lina mkusanyiko kutoka mikoa mbalimbali.

Pia, mazingira na harakati za kutafuta maisha kwa wakazi wa jiji hilo, zimetajwa kuwa kichocheo cha watu wengi kujikuta kwenye matatizo hayo ya kiafya.

Dk Makubi alitaja sababu nyingine ni matumaini ya watu mbalimbali kuwa Dar es Salaam kuna fursa nyingi za maisha na ajira hivyo, wanakuja kwa ajili ya kutafuta lakini, wanapofika mambo huwa tofauti na matarajio.

Alisema kuwa mambo yanapokuwa tofauti na matarajio, baadhi hujikuta kwenye wakati mgumu na kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa likiwemo matumizi ya dawa za kulevya.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kufikia mwaka 2020 watu bilioni moja walikuwa wanaishi na magonjwa ya akili huku wengi walio katika hatari ni wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 39.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Magonjwa ya afya ya akili ya Mirembe, Dk Paul Lawala alisema ugonjwa wa afya ya akili ni tatizo kubwa duniani kwani takwimu zinaonyesha watu milioni 300 duniani wanakabiliwa na tatizo la afya ya akili, ambapo wanahitaji msaada wa kisaikolojia na waliofikia viwango vya juu wanahitaji matibabu.

Undani magonjwa ya akili

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dk Omary Ubuguyu, amesema kuna magonjwa zaidi ya 340 ya akili yaliyogawanywa katika makundi tofauti.

“Kwa kiasi kikubwa magonjwa ya akili yanahusishwa na kupotea kwa nguvukazi, kwa kuwa magonjwa haya yasipotibiwa kwa wakati, wagonjwa wengi hushindwa kurudi kwenye uwezo wao na hivyo, kuathiri uwezo wa uzalishaji.

Kwa jumla magonjwa ya akili yanachangia kwa zaidi ya asilimia 40 ya athari za kiafya kwa mtu mmoja mmoja na jamii,’’ amesema.

“Hii inamaanisha kuwa, jamii yetu inapaswa kuwekeza kwenye afya ya akili kwa kiasi kikubwa zaidi. Uwekezaji katika afya ya akili haulengi tu katika kutibu wale wenye mahitaji, lakini unalenga katika kuimarisha afya ikiwamo udhibiti kwenye matumizi ya vilevi kama pombe na sigara, kufanya mazoezi, lishe bora na kuimarisha uhusiano kwenye jamii,” amesema Dk Ubuguyu.

Chanzo: Mwananchi
 
Usikute hao ndio wameshika nchi sasa, mbona tutakoma, 2025 tukapige kura jamani, tusifanye mzaha
 
Hii inatokana na idadi ya watu wengi wanaotoroka umaskini na dhiki mikoani na kuhamia Dar wakitegemea watakuta ahueni, ila wanakuta hali mbovu hata kuzidi huko wanakotoka...

=====================================

World Health Mental Day is being marked today across the globe as the City of Dar es Salaam takes the lead in having the highest number of people with mental health complications.

The head of the mental health and substance use division of the Health ministry, Dr Shadrack Makubi, said many people from upcountry to the city were the major cause to make Dar es Salaam have the high number of mental health sufferers. Dr Makubi revealed this on behalf of the head of the uncommunicable diseases division at the ministry.

He also said life hardships resulting from the hope by people migrating to the city to look for jobs only to find things were different was another factor, as such people would lose direction and indulge illicit drugs abuse.

The Word Health Organisation (WHO) statistics indicate that as of 2020 a million people were living with mental health complications while the majority of those at risk of falling victims were aged between 15 and 39.

Speaking Dodoma yesterday, Mirembe Psychiatric Hospital director Paul Lawala said the mental health complications were the major problem in the world.

He said the statistics showed three million people were facing the challenge of the mental health complications, needing psychological support and those most affected would need treatment.

He said Tanzania was facing the two major challenges of treating such people including a shortage of psychiatric hospitals and those healed were facing the challenge of not being accepted by society.

According to Dr Lawala, Dodoma’s 95-year-old Mirembe Hospital has 590 beds, but as of yesterday it had 400 mental health patients.

“The challenge that they face is when they are healed as society would hardly accept them in the streets and as a result they continue to be dogged by stress, leading them to continuously be perceived as mental health sufferers,” said Dr Lawala.

Depression is a mental health disease that affects people around the globe at the highest level as it is approximated that five percent of adults and 5.7 per cent of people aged over 60 suffer from the condition in the world.

Youth are mentioned as having been at the highest risk of falling victim because they are at their prime age of having many thoughts, facing life challenges, getting involved in relationships and starting to earn a living.

According to the 2017/2018 report of the WHO, 2,727 people out 100,000 in Tanzania were sufferers of mental health complications.

Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY) director Rustika Tembele revealed this and urged society to love people who were seen to have been affected by mental health issues.

“We should not brand them names that make them fee bad like ‘satellite dish has swayed’, all this is part of unsuitable phrases that stigmatize them as it could make them get discouraged and kill themselves.

“There is a need of bringing love back and as well humanity in society, the system of living has considerably changed as some people don’t care about the problems faced by others. This is very dangerous,

“We need to have the hearts of listening to others and addressing their problems and if possible giving advice,” said Ms Tembele.

In marking the Day, the Tanzania Psychological Association (Tapa) says there is a need to rewrite the existing policies in the country in order to improve mental health, particularly in the area of vaccines.

ngori sana. wananchi wanaishi kama mandondocha Ndani ya dSm
 
Maisha mashambani ni nafuu ila illusion ya migorofa inadanganya wana vijiji kukimbilia Dar na hawana frame to survive in the city, hence they get disillusioned and stressed, reason 80% ya Dar ni low life look, makazi ambao ndio ukubwa wa jiji ama zimejaza mji ni standards za kizamani, village type housing, majority are surviving., In Kenya majimbo imesaidia sana, County system is good, pia several towns have vibrant economic activities, sio lazima kuenda Nairobi ama Mombasa to make it.., though it's a problem in Africa, pia sisi hatujafika bado.., ila ya uendazimu hii ya Tanzania ni ya kipekee., pengine ni ushirikina.., never heard before.
 
Afya ya akili sio lazima uwe kichaa ndugu zangu, ni tatizo linawakuta watu wengi tu, hata humu jf Kuna ambao tayari wana hio shida..

Wengine humu ukisoma hata michango yao utagundua wana hili tatizo, Karibu kupitia jukwaa la mahusiano..
Unaweza kujiona upo vizuri kumbe una tatizo..
 
Wakati Dunia ikiadhimisha Siku ya Afya ya Akili kesho Jumapili Oktoba 10,2021, imeelezwa kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni saba wenye matatizo yanayohusiana na afya ya akili.

Hata hivyo, sababu mbalimbali zimetajwa kusababisha matatizo ya afya ya akili huku Jiji la Dar es Salaam limetajwa kuwa na idadi kubwa ya wenye matatizo hayo.

Miongozi mwa sababu zilizotajwa kuchochea tatizo hilo ni msongo wa mawazo, ugumu wa maisha na matamanio ya kuwa na maisha bora.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa magonjwa yasiyoambukiza, Dk Shedrack Makubi amesema sababu ya Dar es Salaam kuwa na wagonjwa wengi ni kutokana na wingi wa watu katika jiji hilo ambalo lina mkusanyiko kutoka mikoa mbalimbali.

Pia, mazingira na harakati za kutafuta maisha kwa wakazi wa jiji hilo, zimetajwa kuwa kichocheo cha watu wengi kujikuta kwenye matatizo hayo ya kiafya.

Dk Makubi alitaja sababu nyingine ni matumaini ya watu mbalimbali kuwa Dar es Salaam kuna fursa nyingi za maisha na ajira hivyo, wanakuja kwa ajili ya kutafuta lakini, wanapofika mambo huwa tofauti na matarajio.

Alisema kuwa mambo yanapokuwa tofauti na matarajio, baadhi hujikuta kwenye wakati mgumu na kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa likiwemo matumizi ya dawa za kulevya.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kufikia mwaka 2020 watu bilioni moja walikuwa wanaishi na magonjwa ya akili huku wengi walio katika hatari ni wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 39.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Magonjwa ya afya ya akili ya Mirembe, Dk Paul Lawala alisema ugonjwa wa afya ya akili ni tatizo kubwa duniani kwani takwimu zinaonyesha watu milioni 300 duniani wanakabiliwa na tatizo la afya ya akili, ambapo wanahitaji msaada wa kisaikolojia na waliofikia viwango vya juu wanahitaji matibabu.

Undani magonjwa ya akili

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dk Omary Ubuguyu, amesema kuna magonjwa zaidi ya 340 ya akili yaliyogawanywa katika makundi tofauti.

“Kwa kiasi kikubwa magonjwa ya akili yanahusishwa na kupotea kwa nguvukazi, kwa kuwa magonjwa haya yasipotibiwa kwa wakati, wagonjwa wengi hushindwa kurudi kwenye uwezo wao na hivyo, kuathiri uwezo wa uzalishaji.

Kwa jumla magonjwa ya akili yanachangia kwa zaidi ya asilimia 40 ya athari za kiafya kwa mtu mmoja mmoja na jamii,’’ amesema.

“Hii inamaanisha kuwa, jamii yetu inapaswa kuwekeza kwenye afya ya akili kwa kiasi kikubwa zaidi. Uwekezaji katika afya ya akili haulengi tu katika kutibu wale wenye mahitaji, lakini unalenga katika kuimarisha afya ikiwamo udhibiti kwenye matumizi ya vilevi kama pombe na sigara, kufanya mazoezi, lishe bora na kuimarisha uhusiano kwenye jamii,” amesema Dk Ubuguyu.

Chanzo: Mwananchi
Yule wa Bungeni aliyejitangaza naye yumo kwenye hii orodha?
 
Back
Top Bottom