Siku ya Baba Duniani: Kwanini katika familia nyingi akina baba hutangulia kufariki?

Siku ya Baba Duniani: Kwanini katika familia nyingi akina baba hutangulia kufariki?

Weee jamaa umechemsha! Nafasi ya utawala na uongozi kapewa mme! Mme akichemsha kwishinei! Mme akifa familia itaendeshwa kwa neema na fadhila za Mungu. Hakuna hayo mambo ya kwamba mme akifa mke anakuwa kichwa. Mme akifa Yesu (Mungu) ndo anakuwa kichwa na mke kuwa "mjane". Ndo maana Mungu anaitwa "mume wa wajane". Aliyefanyakosa wa kwanza la kula tunda bustani ya Eden alikuwa mwanamke lakini tendo hilo halikuhesabiwa kuwa dhambi mpaka Adam alipokula. Vile vile wakati Mungu anatoa maagizo ya kutokula tunda la mema na mabaya, mwanamke (Hawa) alikuwa hajaumbwa ndo maana kula kwake au kutokula kulikuwa hakumaanushi chochote mpaka Adam alipokula. Nakubaliana na wewe katika kipengere cha wanaume kulalamika kuhusu kuporomoka kimaadili na utii wa wanawake kwa wanaume ambapo kimsingi ni mwanaume!
Nafasi ya Mungu kuwa kiongozi hiyo haibadiliki hata mme akiwa hai au akiwa amekufa,na pia neema na fadhili zipo muda wote kwa kila mtu. Kuhusu kula tunda, mwanaume ndiyo alikuwa na hilo jukumu la kumwambia mke wake maagizo yote maana hata jina ni yeye alimpa,mwanamke kula tunda tayari ilikuwa ni dhambi ilikuwa inasubiriwa muda wa adhabu tu,we unafikiri kama mme angekataa kula tunda ingekuaje?
 
Nimeumizwa sana na hii mada!

Wanaume hatupendwi na jamii ,Bali tunahitajika tukishatatua kero zao au hofu zao hawatutaki Tena kama Greda linalotengeneza Barabara!

Sio mke wala watoto ukishamaliza KAZI ya kutengeza makazi,vitega uchumi na kusomesha watoto kazi imeisha unabaki alone huna ishu Wala hakuna anaekutaka tena,wanakuacha ufe kwa sonona na upweke!!!

Sababu kuu 3.

1.kijamii:-mtatuzi mkuu wa matatizo!
2.kichumi;-mfanyaji kazi ngumu na risk taker!
3.ki bayolojia:-uzazi anaendelea kushiriki mapenzi Hadi uzeeeni ili kuondoa upweke halafu anaongeza tatizo jingine la kiafya kukosa nguvu ya kupambana na maradhi!
Pole sana mwalimu,uzuri watoto wa kike wanavutwa upande wa baba na watoto wa kiume wanavutwa upande wa mama, na watoto wa kike wakishaolewa hawana tena nguvu sana upande wetu na hivyo kutuacha wapweke.
 
Wababa kuwalala mabeki tatu oyuuuuu

Hakuna baba asiyekula mschana wa kazi nasema hakuna
Kiroho yule anayekupikia,kukufulia na kazi nyingine huyo ndiye mke wako,mke ni "majukumu". Mke wako yeye atakaa na boss wake maana ndiye anamjali kuliko wewe. Lakini punguza msisitizo wa kila mwanaume kukaa na dada wa kazi!.
 
Unaongea hivyo labda Kwa sbb umekaa kwenye nafasi Yako km baba
Ila Kwa ambao baba wamekua vichomi hawatakuelewa
Baba mpk unajuta Kwann ndo baba ako[emoji26]
Yaani mama ndo ahangaike na familia na baba upo hela unayo inaishia Kwa wanawake wa nje watt ndani wanahangaika na mama, unafikiri huyo mtu atakuelewa?
Kwahiyo sio wa baba wote wanafaa wengine vimeo
Mwanamke ni mlinzi wa mwanaume,hivyo mke naye amepwaya hapo
 
Leo ikiwa ni siku ya Baba duniani, naomba tutafakari swali hili na kujijibu. Kwanza natoa angalizo kuwa huwa napenda sana kuangazia sababu za kiroho katika kila jambo, hivyo usipende sana kusoma mada zangu kimwili maana itakuwia vigumu kidogo kuelewa. Utangulizi; Ukifanya uchunguzi kama niliofanya mimi utagundua kuwa idadi kubwa ya wanaotangulia kufariki katika familia ni wababa.

Zipo sababu nyingi zinazochangia hali hii, na nyingi ni za kiroho. Nitaangazia chache za kimwili na za kiroho na nyingine wadau mtaongezea. KIMWILI. a) Kibaolojia. Ukiangalia kwa kawaida wanaume wengi hupenda kuoa wanawake wenye umri mdogo kuliko wao. Kibaolojia seli ambazo ndizo kiini cha uhai hutangulia kufa mapema kwa kadri umri wa mtu unavyozidi kuongezeka, na ukizingatia wengi wetu elimu ya lishe hatuna na hali ya uchumi pia si nzuri. b) Kisaikolojia. Wanawake wengi kisaikolojia hujiona duni mbele ya wanaume na hivyo huweza kulia hadharani (kulia ni tiba), kutoa maneno ya uchungu moyoni na kuwa na washauri wengi na watetezi hivyo kupata faraja zaidi ya mwanaume. C) Kiuchumi.

Hali ya uchumi ya mwanaume ikiwa mbaya ndani ya familia, maneno ya mkewe na malalamiko ya watoto yanatosha kukupa mawazo ambayo yanaweza kukumaliza mapema sana. KIROHO. Hapa jibu ni moja tu, mwanaume kushindwa kusimama katika NAFASI yake. Kwa kawaida mwanaume ni kiongozi na mtawala wa mwanamke katika kila kitu ( kumbuka tunazungumzia kiroho).

Mwanaume ukishindwa tu kushika hii nafasi vizuri na zana zote za utawala upewa, kama akili za juu, maono na maneno yenye mamlaka, basi tambua kabisa itakupasa tu ufe mapema ili uondoe kikwazo katika nafasi hiyo na mwingine aitumie kuitawala. Nafasi hii inatawaliwa vizuri kwa kutumia AKILI. Ukiona mwanaume anatawala nafasi hii kwa kutumia nguvu (udikteta) tambua kuwa akili zake zimeharibika.

Kwa nini nakazania sana "akili!?", Ni kwa sababu akili nzuri za mwanaume ndizo pekee zenye uwezo wa kumshepu mwanamke kadri unavyopenda wewe mume wake. Huwa nashangaa sana kuona wanaume wanalalamikia wake zao kuwa hawapo vizuri kitabia au kimuonekano!, sijui kama huwa wanajua kuwa wanajishangaa wenyewe na kujilalamikia!, yaani wewe unamshepu mke wako kadri unavyopenda wewe alafu uanajishangaa tena!

Ni sawa na kumlalamikia mwanamke kwa nini anapata watoto wa njisi moja tu wakati wewe ndiye mwenye gameti XY na yeye ni mpokeaji tu ( ina maana kiroho ya kuwa mwanamke kazi yake ni kupokea tu uongozi kutoka kwako). Mwanamke ameletwa kwako kula raha tu na kukusaidia kukubebea watoto unaotaka na uwezo wa kuwalea na kukusaidia katika ushauri na kwenye mambo madogo madogo.

Laiti wanaume tungeitambua na kusimama katika nafasi hii ya dhahabu tuliyopewa, hakika hakuna mwanamke angetamani kuwa mwanaume na kutudharau. Sasa tunaitimisha mada kwa kusema kuwa, nafasi ni "majukumu", endapo mwanaume utashindwa kutawala nafasi hii ( majukumu yako), mwanamke kazi yake ni kupeleka malalamiko yake mbele ya "KITI KIKUU" kwa kujua au kutokujua kuwa anakuombea ufe mapema huku akisindikizwa na watoto kama mashaidi.

Endapo ushaidi ukithibitika ni wa kweli, basi ataulizwa swali moja tu mara tatu kwa nyakati tofauti, ya kuwa "tukimwondoa huyu wewe utaweza kushika hii nafasi kuendesha familia?" akijibu ndiyo, tunakupoteza kweli. Ukiona mwanamke ameweza kuendesha familia baada ya mume wake kufa, tambua kuwa huyo mwanaume siku yake sahihi ilikuwa imefika au alipenda tu yeye atangulie au alikuwa kikwazo kweli kwa mkewe. Ukiona mwanamke ameshindwa kuendesha familia baada ya mumewe kufa, tambua kuwa huyo mwanamke alikurupuka kumshtaki mumewe kwa tamaa ya hiyo nafasi akifikiri ataweza kuitumia kirahisi. Naomba nikuulize hili swali, "wewe unafikiri kati ya mtawala na mtawaliwa yupi kikawaida angepaswa kutangulia mapema?".
Wanaume wengi hutangulia kufariki
  1. Frustration wanazosababishiwa na wake zao
  2. Kuuawa ili wanawake wafanye yao
 
Mikikimikiki yote ya dunia hii anapambana nayo Baba, angalia hapo Dar es salaam idadi ya wapiga debe na makondakta wa daladala wanaume ni wangapi na wanaume ni wangapi

JWTZ wamepeleka jeshi DRC kupambana na M23 angalia idadi ya akinamama Vs akinababa.

Mida hii tunavyoongea huko baharini deep sea mameli yanapigwa na mawimbi kaangilie idadi ya akina Baba Vs idadi ya akinamama.

Mida hii jua kali linawaka nenda chini ya migodi kaangalie akina mama ni wangapi na akinababa NI wangapi?

Kifupi Wanaume ndio wapo exposed kwenye hatari nyingi zinazowafanya miili yao kuchoka au hata kuumia na kufa mapema.

Gari inayotembea 1000km kwa siku na lile linalotembea 5km kwa siku sijui ni lipi litachoka mapema na kuwa scrap.
Umemaliza mkuu,hii ndiyo jawabu sasa
 
Wanaume wengi hutangulia kufariki
  1. Frustration wanazosababishiwa na wake zao
  2. Kuuawa ili wanawake wafanye yao
Hii ya pili ni kutokana na kubanwa kutekeleza ndoto zao na hivyo kutafuta uhuru wa kutekeleza,ila mara nyingi hufeli na kuharibu kabisa.
 
Aaah yaani KE anisumbue nianze kuweka mambb kifuani,ya nini kuteseka. Si tumeambiwa tuishi nao kwa akili,hawa viumbe ni kuwapa adhabu ya kisaikolojia tu na sio kutumia minguvu
 
Nafasi ya Mungu kuwa kiongozi hiyo haibadiliki hata mme akiwa hai au akiwa amekufa,na pia neema na fadhili zipo muda wote kwa kila mtu. Kuhusu kula tunda, mwanaume ndiyo alikuwa na hilo jukumu la kumwambia mke wake maagizo yote maana hata jina ni yeye alimpa,mwanamke kula tunda tayari ilikuwa ni dhambi ilikuwa inasubiriwa muda wa adhabu tu,we unafikiri kama mme angekataa kula tunda ingekuaje?
Kama Adam angekataa dhambi isingeingia duniani
 
Unasema andiko lako la kiroho sana wakati liko kimwili asilimia zote

Elewa Mungu anapambania wanaume ili msimamo wake uonekane lkn shetani anasimamia wanawake ili atawale, nb ujue siyo kila mwanaume anayekufa huwa kweli amekufa rahasha ukiwa rohoni utanielewa
Wengine hupotea kimazingira tu mnadhani kafa vita ya mwanaume ni kubwa na shubiri yake si ya kitoto lzm ujue hili
 
Aaah yaani KE anisumbue nianze kuweka mambb kifuani,ya nini kuteseka. Si tumeambiwa tuishi nao kwa akili,hawa viumbe ni kuwapa adhabu ya kisaikolojia tu na sio kutumia minguvu
Hiyo njia usijaribu maana imeua wengi,bora kuachana nao na kukaa mbali kimya
 
Unasema andiko lako la kiroho sana wakati liko kimwili asilimia zote

Elewa Mungu anapambania wanaume ili msimamo wake uonekane lkn shetani anasimamia wanawake ili atawale, nb ujue siyo kila mwanaume anayekufa huwa kweli amekufa rahasha ukiwa rohoni utanielewa
Wengine hupotea kimazingira tu mnadhani kafa vita ya mwanaume ni kubwa na shubiri yake si ya kitoto lzm ujue hili
Mchango mzuri,ila naona upo rahoni sana kuliko rohoni yenyewe
 
Back
Top Bottom