Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji: Ukeketaji ni nini na unafanyika wapi?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124


Viongozi wa dunia wameahidi kutokomeza ukeketaji ifikapo mwaka 2030, lakini wanaharakati wanasema utamaduni huo hatari na uliopitwa na wakati bado umekita mizizi katika maeneo mengi.

Tarehe 6 Februari ni siku ya Kimataifa ya kupambana na ukeketaji dhidi ya wasichana na wanawake, lengo likiwa kuangazia juhudi zinazofanywa za kutokomeza desturi hiyo ambayo inawaathiri takriban wasichana na wanawake milioni 200 kote duniani.

Ukeketaji unaaminika ulianza miaka 2,000 iliyopita na unafanywa na makabila na dini mbali mbali duniani.

Kulingana na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, ukeketaji unafanyika katika mataifa yasiyopungua 30, mengi yakiwa ya Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.

Ukeketaji unamaanisha baadhi ya viungo vya sehemu za siri za msichana au mwanamke ama zinakatwa kwa sehemu fulani au zinanyofolewa kabisa. Katika baadhi ya makabila huwa wanashona sehemu hizo au kuzichanja.
 
Upvote 0
...
Viongozi wa dunia wameahidi kutokomeza ukeketaji ifikapo mwaka 2030, lakini wanaharakati wanasema utamaduni huo hatari na uliopitwa na wakati bado umekita mizizi katika maeneo mengi.
...
"... utamaduni huo hatari na uliopitwa na wakati"; kwa hiyo wanaharakati watushawishi kuachana na utamaduni hatari na ULIOPITWA NA WAKATI na kutuletea utamaduni mpya wa HOMOSEXUALITY sio? Miongoni mwa madhara ya ushoga:-
  • Hudhalilisha ubinadamu; binadamu hutenda yale ambayo hata mbwa hajawahi wala kuwaza kutenda.
  • Hatari ya magonjwa - HIV, UTI, Cancer, etc.
  • Kizazi kupotea - hakuna kuzaliana; kila jinsia ikiamua "kujioa" yenyewe, existence ya binadamu itakuwaje?
  • Ni DHAMBI mbele za Mungu.
Siutetei UKEKETAJI ila ukiweka kwenye mizania, UKEKETAJI ni mwepesi by far kuliko USHOGA. Sasa hawa wanaharakati badala ya kuhangaika na maboriti wanahangaika na vibanzi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…