JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Viongozi wa dunia wameahidi kutokomeza ukeketaji ifikapo mwaka 2030, lakini wanaharakati wanasema utamaduni huo hatari na uliopitwa na wakati bado umekita mizizi katika maeneo mengi.
Tarehe 6 Februari ni siku ya Kimataifa ya kupambana na ukeketaji dhidi ya wasichana na wanawake, lengo likiwa kuangazia juhudi zinazofanywa za kutokomeza desturi hiyo ambayo inawaathiri takriban wasichana na wanawake milioni 200 kote duniani.
Ukeketaji unaaminika ulianza miaka 2,000 iliyopita na unafanywa na makabila na dini mbali mbali duniani.
Kulingana na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, ukeketaji unafanyika katika mataifa yasiyopungua 30, mengi yakiwa ya Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.
Ukeketaji unamaanisha baadhi ya viungo vya sehemu za siri za msichana au mwanamke ama zinakatwa kwa sehemu fulani au zinanyofolewa kabisa. Katika baadhi ya makabila huwa wanashona sehemu hizo au kuzichanja.
Upvote
0