Siku ya Kimataifa ya Waathirika wa Kupotea kwa Lazima 2025: Ukweli, Uponyaji, na Utu

Siku ya Kimataifa ya Waathirika wa Kupotea kwa Lazima 2025: Ukweli, Uponyaji, na Utu

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Leo, Agosti 30, ulimwengu unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Waathirika wa Kupotea kwa Lazima (Enforced Disappearance). Siku hii, iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 2010, inalenga kuongeza uelewa kuhusu ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu na kutoa wito wa uwajibikaji. Mwaka 2025, kaulimbiu inaangazia "Ukweli, Uponyaji, na Utu," ikisisitiza umuhimu wa kufichua hatima ya waliopotea, kutoa msaada kwa familia, na kurudisha heshima kwa waathirika kupitia uwajibikaji.

Mwelekeo wa Kimataifa​


Kupotea kwa lazima kunabaki kuwa tatizo kubwa ulimwenguni kote. Mara nyingi, hutumiwa na Utawala kama chombo cha ukandamizaji ili kuzima upinzani, kutia watu hofu, na kukwepa mkono wa sheria. Kikosi Kazi cha UN kinacho jihusisha na kesi za Upotevu wa Lazima au Usio wa Hiari (WGEID) kimerekodi takriban kesi 61,500 katika nchi 115 tangu mwaka 1980.
Kati ya Mei 2024 na Mei 2025 pekee, kesi mpya 1,278 ziliripotiwa kutoka nchi 38, ikionyesha kuwa tatizo hili linaongezeka. Maelfu ya watu wametoweka, huku waathirika wengi wakiteswa, kuuawa kinyume cha sheria (extrajudicial killings), au kutengwa na kuwa kizuizini kwa muda mrefu.

Hali Halisi Barani Afrika​


Barani Afrika, upotevu wa lazima hutumiwa mara kwa mara na serikali kupitia vikosi vya usalama ili kunyamazisha wanaharakati, wapinzani, na wakosoaji, hasa katikati kipindi cha misukosuko ya kisiasa, migogoro ya kivita, au utawala wa kijeshi.
Ingawa takwimu kamili za bara zima ni ngumu kuzipata, Tume ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu (ACHPR) na UN zimebainisha ongezeko la kesi kwenye nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mfano, Afrika Magharibi, serikali za kijeshi za nchi kama Mali, Guinea, Burkina Faso, na Niger zimetumia utekaji na kupteza watu kama zana ya ukandamizaji.
  • Amnesty International ilirekodi visa kadhaa mwaka 2024-2025, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara wa wanaharakati wawili wa Guinea, Mamadou Billo Bah na Oumar Sylla mnamo Julai 2024.
  • Nchini Kenya, kesi za upotevu wa lazima ziliongezeka kwa kasi, na visa 55 viliripotiwa mwaka 2024, ongezeko la 450% kutoka visa 10 mwaka 2023. Hali hii ilionyesha uhusiano wa karibu na maandamano ya Gen-Z na ukatili wa polisi.

Screenshot 2025-08-30 095336.png

Screenshot 2025-08-30 095131.png


​

Hali ilivyo Tanzania​


Nchini Tanzania, visa vya kupotea kwa lazima vimeongezeka, hasa vikiwalenga wanasiasa wa upinzani, wanaharakati, na wakosoaji kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimerekodi matukio 100 kuanzia Januari 2015 hadi Februari 2025.
Ongezeko lilionekana zaidi miaka ya hivi karibuni:
  • Mwaka 2021: visa 12
  • Mwaka 2022: visa 14
  • Mwaka 2023: visa 15
  • Mwaka 2024: visa 63 (kati ya hivi, 33 vilidhaniwa kuwa vya kupotezwa kwa lazima)
Screenshot 2025-08-30 094813.png


Screenshot 2025-08-30 095603.png

Mkoa wa Dar es Salaam uliathirika zaidi, ukichangia 35% ya kesi zote tangu 2015, ukifuatwa na Arusha (26%). Baadhi ya matukio mashuhuri ya 2024 ni pamoja na utekaji nyara, kuteswa, na mauaji ya kiongozi wa upinzani wa CHADEMA, Ali Mohamed Kibao, na kutoweka kwa Edgar Mwakabela (Sativa), ambaye baadaye alipatikana akiwa ameteswa Mkoani Katavi.

Wataalamu wa UN wameripoti visa zaidi ya 200 tangu 2019, wakiihimiza serikali ya Tanzania kusitisha tabia hii na kufanya uchunguzi. Siku ya leo inatoa wito kwa Tanzania na nchi nyingine kuheshimu mikataba ya kimataifa na kuhakikisha uwajibikaji ili wale waliopotea wapate ukweli, familia zao zipate uponyaji, na waathirika warudishiwe Utu wao.


Kutowajibishana kunuongeza mateso na maumivu. Chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu, familia na jamii zina haki ya kujua ukweli kuhusu kilichotokea kwa ndugu zao. Ninaomba nchi wanachama kutimiza wajibu huu.
António Guterres

Sources
Amnesty
France Diplomacy
Missing Voices
LHRC
Special Rapporteur for Freedom of Expression and Opinion
 
Back
Top Bottom